Tafuta

Kimbunga kikali Fiona kilichokumba Puerto Rico watu wengi hawana mahali pa kukaa. Kimbunga kikali Fiona kilichokumba Puerto Rico watu wengi hawana mahali pa kukaa. 

Papa Francisko anasali kwa ajili ya waathirika wa dhoruba Fiona

Hasira ya upepo wa nguvu tayari ilikuwa imevamia Karibiani na inaelekea katika masaa haya visiwa vya Bermuda.Wanahesabu uharibifu uliosababishwa na mafuriko katika Jamhuri ya Dominika na Puerto Rico,ambapo Papa anawatazama na mamlaka inaripoti vifo vitatu na maelfu ya watu waliokimbia makazi yao.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Uharibifu na waathirika ambao kupita Kimbunga Fiona kimacha  nyuma, msimu wa kwanza ambao tayari umevuma kwa upepo unaozidi kilomita 210 / kwa saa huko Santo Domingo na Puerto Rico, tukio ambalo limemhuzunika Papa Francisko na ambaye ametuma telegramu mbili zilizo sainiwa na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin kwa Makanisa mahalia, akikabidhi jumuiya za nchi zote mbili katika mikono ya upendo ya Bikira Maria.

Msukumo wa ukaribu wa kindugu  na mshikamano kwa Jamhuri ya Dominika

Akimwelekea Askofu Mkuu Freddy Antonio de Jesus Breton Martinez, wa Santiago de Los Caballeros na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Dominika, Baba Mtakatifu anawabariki wana na mabinti wote wa Jamhuri ya visiwa vya Karibiani huku akiwahakikishia maombi yake kwa sababu Bwana aweza  kuwafariji wapendwa wa Dominika ambao  wanaoteseka. Kwa upande wa Baba Mtakatifu pia  amaetoa wito kwa Jumuiya nzima ya Kikristo na kwa watu wenye mapenzi mema kufanya juhudi kubwa zaidi ya mshikamano na ukaribu wa kindugu kwa wale ambao ni wahanga wa janga hilo  analokabidhi kwa mikono ya upendo na ya kimama ya Mama Yetu wa Altagracia.

Papa amewakabidhi mikononi mwa Maria watu wa Puerto Rico

Katika  telegramu aliyoielekezwa kwa rais wa Baraza la Maaskofu wa  Puerto Rico, Askofu  Ruben Antonio Gonzalez Medina, wa Ponce anaomba salamu zake ziwafikie wapendwa wa Puerto Rico ambao wanaomboleza kwa sababu ya kupoteza maisha ya binadamu, na kurekodi uzito wa  uharibifu uliosababishwa na kimbunga Fiona. Nchini kulikuwa na hali ya dharura kutokana na maporomoko ya ardhi kuangusha miti na nyaya za umeme zilizopulizwa, pamoja na kuporomoka kwa miundombinu mingi. Kulingana na wataalamu, tukio la janga kutokana na matokeo ya mafuriko litabaki. Kwa ajili ya maafa"ya wakati huo Papa Fransisko anasali kwa Baba mwenye rehema ili awape faraja yake.  Papa Francisko anawatumia baraka yake huku akiwaweka katika mikono ya Mama Yetu wa Maongozi ya Mungu.

Kimbunga Fiona katika Jamhuri ya Dominika
Kimbunga Fiona katika Jamhuri ya Dominika

 

21 September 2022, 17:06