Tafuta

2022.08.26 Zaidi ya vijana elfu Moja wahudumu wa Alatreni nchini Ufaransa wamekutana na Papa 2022.08.26 Zaidi ya vijana elfu Moja wahudumu wa Alatreni nchini Ufaransa wamekutana na Papa  

Papa kwa wahudumu wa Altareni kutoka Ufaransa:Oneshini mfano kwa vijana wengine!

Akihutubia zaidi ya wahudumu 1,000 wa altareni kutoka Ufaransa ambao wako katika hija jijini Roma, Papa Francisko amesema wao ni kielelezo na mfano bora kwa vijana wengi wa rika lao na amewakumbusha kwamba utume wao hauishii kwenye Misa bali unaendelea mahali popote wanaoishi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 26 Agosti 2022 amekutana na wahudumu zaidi ya 1000 wa altareni kutoka nchini Ufarana katika fursa ya hija yao jiji Roma. Amemshukuru Askofu de Moulins-Beaufort kwa maneno yake kwa niaba ya wote na kwa niaba ya maaskofu waliokuwapo. Wao wameweza kupumzika katika likizo yao kwa kuchukua fimbo ya mahujaji, amesema papa na  wao wamejikita katika safari pamoja na wengine, kufuata nyayo za mashahidi wengi wa Kristo ambao, kwa karne nyingi, wamekuja Roma ili kujitengeneza kwa upya katika imani. Wamefika kwa wingi, kutoka parokia na mikoa mbalimbali ya Ufaransa, ili kujionea wakati huu wa kuchota baraka  ya kukutana, kushirikiana, kusali na kustarehe. Ni matumaini ya Papa kwamba wataweza kurudi nyumbani wakiwa wameimarishwa na uzoefu huu mzuri wa imani, katika moyo wa Kanisa. Mada ya hija yao inayowaongoza ni “Njoo, tumikia na uende!”  na kwamba ni nzuri sana na inajielezea.

Papa amekutana mjini Vatican na wahudumu wa altare zaidi ya 1000 kutoka nchini Ufaransa
Papa amekutana mjini Vatican na wahudumu wa altare zaidi ya 1000 kutoka nchini Ufaransa

Papa Francisko amesema: “Njoo”: Bwana anakuita. Anakuita kukutana naye, na kwa namna ya pekee  katika tukio muhimu ambalo ni la  Misa ya kila dominika”. Kwa kusisitiza amesema: “Kijana mpendwa, ninajua kwamba, pengine, kwenye Misa unajikuta wewe na rika lako tu, na kwamba jambo hilo linaonekana kuwa la kuhuzunisha kwako, au kwamba nyakati fulani hujisikii vizuri katikati ya wazee. Hakika unajiuliza maswali kuhusu Kanisa, unajiuliza jinsi ya kurejesha ladha ya Mungu kwa vijana wa rika lako ili waweze kuungana nawe. Lakini nakuuliza wewe binafsi: je unaonaje nafasi yako katika Kanisa? Je! unajisikia kama mshiriki wa familia hii kuu ya Mungu? Kuchangia ushuhuda wake?

Papa amekutana mjini Vatican na wahudumu wa altare zaidi ya 1000 kutoka nchini Ufaransa
Papa amekutana mjini Vatican na wahudumu wa altare zaidi ya 1000 kutoka nchini Ufaransa

Kwa maana hiyo Papa amebainisha kuwa wao wamechagua kuwa wahudumu wa altareni na hivyo amependa kuwakushukuru kutoka moyoni mwake kwa juhudi, na wakati mwingine kujikatalia, kwa sababu wanakubali kujitolea kwa ahadi hiyo kama wahudumu wa altareni wakati marafiki zao wengine wengi wanapendelea kulala. Dominika asubuhi, au kucheza michezo ... ni kiasi gani wanaweza kuwa mfano, kwa hatua ya kumbukumbu kwa vijana wengi wa umri wao. Na wanaweza kujivunia sana kile wanachofanya. Wasione haya kutumikia altareni hata ukiwa wako peke yao, hata kama wanakua. Ni heshima kumtumikia Yesu anapotoa maisha yake  kwa ajili yetu katika Ekaristi. Kupitia ushiriki wao katika liturujia, kwa kuhakikisha huduma yao, wanamtolea kila mtu ushuhuda thabiti wa Injili. Mtazamo wao wakati wa sherehe tayari ni utume kwa wale wanaowaona. Ikiwa wanafanya huduma yao altareheni kwa furaha, heshima na kwa mtazamo wa sala, hakika wataamsha kwa vijana wengine hamu ya kujitolea kwa Kanisa pia.

Papa amekutana mjini Vatican na wahudumu wa altare zaidi ya 1000 kutoka nchini Ufaransa
Papa amekutana mjini Vatican na wahudumu wa altare zaidi ya 1000 kutoka nchini Ufaransa

Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba lakini kutumikia Misa kunahitaji ufuatiliaji na uwajibikaji  ambao ni “Tumikia na uende!” Papa amethibitishwa kwamba wao wanajua kuwa Yesu yuko ndani ya watu na ndugu tunaokutana nao. Baada ya kumtumikia Yesu kwenye Misa, anawatuma ili wamtumikie kwa watu wanaokutana nao kwa siku,  hasa ikiwa ni maskini na wasiojiweza, kwa sababu Yesu anaungana nao hasa. Labda wana marafiki wanaoishi katika vitongoji vigumu au ambao wanakabiliwa na mateso makubwa, hata ukiritimba; wanajua vijana ambao wamehamishwa, wahamiaji au wakimbizi. Kwa maana hiyo Papa amewasihi wawakaribishe kwa ukarimu, ili kuwatoa katika upweke wao na kufanya urafiki nao. Vijana wengi wa rika lao wanahitaji mtu wa kuwaambia kwamba Yesu anawajua, anawapenda, anawasamehe, anashirikishna matatizo yao, anawatazama kwa upole bila kuwahukumu. Kwa ujasiri wao, shauku yao, hiari yao, wanaweza kuwafikia. Papa wameaalika kwa maana huyo kuwa karibu na kila mmoja na kwa kusisitiza juu ya hilo: amesema wafanye  “ukaribu kati yao, ukaribu na wanafamilia wao, ukaribu na vijana wengine” katika hali halisi.

Papa amekutana mjini Vatican na wahudumu wa altare zaidi ya 1000 kutoka nchini Ufaransa
Papa amekutana mjini Vatican na wahudumu wa altare zaidi ya 1000 kutoka nchini Ufaransa

Papa  lakini pia amewapa onyo la kuepuka kuangukia katika jaribu la kujiondoa ndani yao, la ubinafsi, la kujifungia katika ulimwengu wao, katika vikundi vidogo, katika mitandao ya kijamii ya kawaida. Ni bora kupendelea urafiki wa kweli, na  sio ule usio wa  kweli, ambao ni wa uwongo na unakufunga na kukutenganisha na ukweli. Jambo jingine muhimu pia ni uhusiano wao na wazee, babu na bibi zao. Je, mtazamo wao kwa wazee ukoje? Kwa wale walio na bahati ya kuwa na babu au bibi zao, ni thamani ya kuchukua fursa ya uwepo wao, ushauri wao, uzoefu wao. Mara nyingi ni wao wanao wasindikiza kwenye Misa na kuzungumza nao juu ya Mungu. Wazee ni nyenzo muhimu kwa ukomavu wao wa kibinadamu. Leo hii, hatari ni kutojua tena walikotoka, kupoteza mizizi yao, kupoteza mwelekeo wao. Je ni mpango gani wa kujenga maisha yao ya baadaye, kupanga maisha yao, ikiwa hawana mizizi imara inayowasaidia kukaa sawa na kushikamana na dunia? Ni rahisi kuruka mbali, wakati mtu hana pa kung'ang'ania, mahali pa kujirekebisha (taz. Wosia Christus vivit, 179). Papa ameomba kutafuta mizizi yao, wajifunze kujua na kupenda utamaduni wao, historia yao, kuingia katika mazungumzo katika ukweli na wale walio tofauti na wao, wenye nguvu katika jinsi walivyo na kuheshimu kile ambacho wengine walivyo.

Papa amekutana mjini Vatican na wahudumu wa altare zaidi ya 1000 kutoka nchini Ufaransa
Papa amekutana mjini Vatican na wahudumu wa altare zaidi ya 1000 kutoka nchini Ufaransa

Katika umri wao, ni wakati wa kuweka misingi imara ya maisha yanayokua ndani ya Kristo, kujenga urafiki wa ajabu, kuweka malengo ya kufikia. Katika umri wao, ni wakati ambapo unaota ndoto kubwa, na wanataka kushinda ulimwengu.  Papa ameahidi kwamba hataacha  kuwaambia vijana kamwe anapokutana nao na leo  amewaambia wao, kwa kila mmoja wao, hasa wahudumu wa altareni vijana kwamba : “Msikate tamaa juu ya ndoto zenu  na msisizike kamwe  wito (rej. Wosia wa Papa wa Cv 272). Na ni huduma hasa kwenye Altare  ambayo inaweza kuamsha ndani mwao  hamu ya kuitikia wito wa Bwana katika maisha ya kitawa au ya kikuhani. Kwa nini isiwe hivyo? Msiogope! Mwilisha wito huo  katika moyo wao na siku siku moja, wawe na ujasiri wa kuizungumza na mtu wanayemwamini. Inapendeza sana kuona vijana wakijitolea kwa ukarimu kwa Ufalme wa Mungu, katika huduma ya Kanisa! Ni tukio  zuri sana.

Papa amekutana mjini Vatican na wahudumu wa altare zaidi ya 1000 kutoka nchini Ufaransa
Papa amekutana mjini Vatican na wahudumu wa altare zaidi ya 1000 kutoka nchini Ufaransa

Hatimaye, Papa amewasihi sana wajikabidhi kwa Bwana kwa njia ya Bikira Maria. Kama msichana yeyote, yule alikuwa na ndoto zake, mipango yake. Lakini kwa wito wa Mungu, alijifanya kuwa mtumishi kwa “ndiyo” yake mkarimu, mwenye kuzaa matunda na mwenye furaha. Katika njia zao, wakati wa shida na upweke, wasisahau kujikabidhi kwake. Amehitimisha kwa bataka takatifu.

Hotuba ya Papa Francisko kwa wahudumu wa altare zaidi ya 1000 kutoka Ufaransa
26 August 2022, 17:09