Tafuta

Papa Francisko:kama hakuna udugu na utume wa kiinjili haupo

Kabla ya sala ya Malaika wa Bwana katika Dominika ya kwanza ya mwezi Julai 2022,Papa Fransisko amekumbusha kwamba ili kuweza kuwapelekea wengine Injili la muhimu si kujifanya kuwa mhusika,ushindanima mantiki ya ufanisi. Jambo msingi ni uwezo wa kutembea na ndugu kwa kuheshimiana.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Fransisko kabla ya sala ya Malaika wa Bwana ameongozwa na Injili ya Luka kutoka Liturujia ya Dominika tarehe 3 Julai 2022, ambayo alikuwa tayari ametoa tafakari katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma akisisitizia juu ya mtindo wa Mungu katika utume wa uinjilishaji. Papa hata hivyo ametazamia mashaka ambayo wengine wanaweza kuwa nayo kwa kutafakari sababu za kuwatuma wanafunzi vijijini kumkaribisha Yesu. Lakini wao walitumwa 'wawili-wawili'. Je ni kwa sababu gani? Kwa kufikiri juu yake,  Papa amekubali kwamba tendo la kuwa na  msindikizaji ni chanzo cha uwezekano wa ugomvi, kwa mfano labda wa mwingine kwenda pole pole na kutokuwa na fursa.  Wakati, kwa upande mwingine, ukiwa peke yako, inaonekana kwamba safari inakuwa ya haraka na laini. Japokuwa Yesu, hata hivyo, hafikiri hivyo. Maagizo anayowapatia hayahusu sana kile wanachopaswa kusema bali kuhusu jinsi wanavyo paswa kuwa, yaani, si kuhusu kitabu kidogo ambacho wanapaswa kuzungumzia, hapana; juu ya ushuhuda wa maisha, au kutolewa zaidi ya maneno ya kusema. Kwa hakika, Yesu anawafafanua kuwa watenda kazi yaani, wao wameitwa kufanya kazi, kuinjilisha kupitia mwenendo wao.

Sala ya Milaika wa Bwana 2022
Sala ya Milaika wa Bwana 2022

Papa  Francisko alikuwa tayari amesema hayo katika Misa iliyotangulia kwamba , kamwe hakuna kutembea bila ndugu, kwa sababu hakuna utume bila ushirika na amerudia kufafanua hayo katika tafakari kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana kwamba wanafunzi hawatakiwi kuhesabiwa kuwa wapigiwa makofi huru na wahubiri ambao hawajui jinsi ya kutoa neno kwa mwingine. Kipaumbele, kwa mujibu wa mtindo wa Mungu, ni kujua  kukaa pamoja, kuheshimiana, kutotaka kujidhihirisha kwamba wana uwezo zaidi ya wengine na kuwa na marejeo ya pamoja kwa Mwalimu mmoja”. Na hapo, basi, ndiyo moyo wa ujumbe wa siku, ambapo umerudiwa mara mbili kwamba "Inawezekana kufanyiwa kazi mipango kamili ya kichungaji, mipango iliyofanywa vizuri kutekelezwa, iliyopangwa hadi maelezo madogo zaidi; unaweza kuita umati na kuwa na njia nyingi; lakini kama hakuna upatikanaji wa udugu, utume wa kiinjili  hausongi mbele".

Sala ya Milaika wa Bwana 3 Julai 2022
Sala ya Milaika wa Bwana 3 Julai 2022

Kwa kufafanua kuhusiana na hilo Papa amesimulia hstoria ya mmisionari mmoja Afrika ambaye, baada ya kutengana na mmoja wa wanashirika wake, aliishia kuwa  kama mjasiriamali kwa kiasi fulani, hata kama alikuwa na akili  na mwenye kuangaika na shughuli za ujenzi. Alikuwa amesahau jambo muhimu zaidi alilogundua tena mara baada ya kukutana naye tena. Jambo ambalo Papa Francisko alitaka kulitilia mkazo hasa ikiwa kweli tunaweza kufanya maamuzi pamoja na wengine, kuheshimu maoni ya wengine, au badala yake kama sisi ni wabinafsi! Baba Mtakatifu Francisko amefafanua kwamba "Utume wa uinjilishaji hautokani na uanaharakati wa kibinafsi, yaani, juu ya kutenda, bali ni juu ya ushuhuda wa upendo wa kindugu, pia kupitia shida zinazohusika na kuziishi pamoja. Kwa maana hiyo  tunaweza kujiuliza: Je, tunashiriki vipi habari njema ya injili na wengine? Je, tunaifanya kwa roho na mtindo wa kindugu, au kwa namna ya ulimwengu, kwa kutaka kuongoza, ushindani na ufanisi?

Sala ya Milaika wa Bwana 3 Julai 2022
Sala ya Milaika wa Bwana 3 Julai 2022

Wenyeheri wapya nchini Argentina

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana Papa Francisko aliwakumbuka Pedro Ortiz de Zárate na Giovanni Antonio Solinas, waliotangazwa kuwa wenyeheri wapya nchini Argentina,  ambao walikuwa ni wamisionari wawili waliouawa kikatili na Wahindi mnamo tarehe 27 Oktoba 1683.  Papa amesema, mfano wao  unaweza kutusaidia kuleta Injili ulimwenguni bila kuhaidi. Na baadaye kwa mara nyingine tena ameto wito kwa ajili ya amani nchini Ukraine. Kwa viongozi wa kisiasa kimataaifa Papa Francisko amesema: “Mgogoro wa Ukraine unaweza kuwa changamoto kwa watawala wenye busara”, alisema.

03 July 2022, 14:08