Tafuta

Papa kwa Jumuiya ya Congo:Muwe wanyenyekevu wa ushuhuda wa amani!

Tarehe 2 Julai Papa angekuwa katika ziara ya Kitume.Tukio hilo liliahirishwa kwa sababu ya kuumwa goti.Kwa ishara ya ukaribu na upendo kwa watu waliokuwa wanamsubiri kwa hamu,Dominika 3 Julai ameadhimisha misa akiwa na Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma.Katika mahubiri ametoa wito wa kuacha uchu,kuzima hasira,kuacha ufisadi na ikiwa amani inaanzia kwa kila moyowa jamii na nchi vinabadilika.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Nani angeweza kusashau maneno ya: “Tutaleta Kinshasa hadi Mtakatifu Petro na hapo tutasherehekea na Wakongo wote wanaoishi Roma, ambao ni wengi!? Kumbe ni ahadi ya Papa Francisko aliyoitoa mnamo tarehe 13 Juni iliyopita, katika kujibu uamuzi mchungu wa kuahirisha ziara yake ya kitume ya kwenda barani  Afrika kwa sababu za kiafya, na hatimaye imetimizwa Dominika  tarehe 3 Julai 2022. Katika siku ya tarehe 2 Julai, alikuwa anatarajiwa kuwepo katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambako angeongoza Misa Takatifu kama ratiba ilivyokuwa imepangwa. Kwa niaba yake  Dominika asubuhi huko Kinshasa, kwa kupeleka upendo na ukaribu wa dhati, alikuwa  ni Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, na kwa kuwakumbatia Waafrika wapendwa, Wakongo na pia Sudan Kusini ambao walikuwa watembelewe na Papa, tendo hilo limefanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Misa ya Papa kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma

Ndani ya kanisa zilikuwa zikionekana rangi, kusikia sauti, maombi kwa  ibada ya Kizaire jina la zamani la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo ni  ibada ya kipekee iliyoongozwa katika Kanisa la kuu la Kilatini, ambalo limejazwa na furaha kubwa. Kulikuwa na Kwaya ya Bondeko, lugha nne za kitaifa za nchini DRC katika usomaji wa masomo na sala ambazo zimeelekezwa hata kuwaombea watawala, na watu waliokuwa wamevalia nguo za rangi tofauti, ngoma, sauti za ala za kiutamaduni. Kwa hakika sehemu ya  Afrika ilikuwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Misa kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma,Dominika 3 Julai 2022
Misa kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma,Dominika 3 Julai 2022

Pumzi ya Afrika tajiri, lakini ambayo mara nyingi inajeruhiwa na vurugu, chuki na uchoyo, imesikika pia Katika maneno ya Papa  Francisko wakati wa mahubiri yake ambapo ameiombea nchi amani na Wakristo wawe mashahidi wake. Papa amesema: “Kaka na dada wapendwa  leo tuwaombee amani na upatanisho katika nchi yenu, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliyojeruhiwa na kunyonywa. Tunaungana na Misa inayoadhimishwa nchini kulingana na nia hii na tunaomba kwamba Wakristo wawe mashuhuda wa amani, wenye uwezo wa kushinda hisia zozote za chuki, hisia zozote za kulipiza kisasi, kushinda jaribu la kwamba upatanisho hauwezekani, uhusiano wowote usiofaa na wao wenyewe, kwa kundi linalopelekea kuwadharau wengine".

Misa kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma,Dominika 3 Julai 2022
Misa kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma,Dominika 3 Julai 2022

Maneno ya mahuburi yaliyofunguliwa na kufungwa kwa lugha ya Kikongo na Papa Fransisko kwa kubadilishana na kusanyiko lililokuwa linashangilia na kudhihirisha furaha yote ya maadhimisho haya lilitoka katika Injili ya Luka (10.1-12.17-20) na jinsi ambavyo Yesu anawateua na kuwatuma wanafunzi wake, wawili-wawili mbele yake, katika utume ambao Papa amethibitisha kwamba una  sifa tatu au tuseme, maajabu matatu ambayo yanatushangaza. Kwanza  zana, ujumbe na mtindo ambao anawambia Wakristo wote jinsi ya kuishi na jinsi ya kujenga ulimwengu wa amani.

Misa kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma,Dominika 3 Julai 2022
Misa kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma,Dominika 3 Julai 2022

Baba Mtakatifu Francisko amesema kimsingi ni kwamba kama Wakristo hatuwezi kuridhika na kuishi katika hali ya wastani, ambayo ni ugonjwa wa Wakristo wengi, na hatari kwa kuzingatia fursa na urahisi wetu. Sisi sote ni wamisionari wa Yesu. Na ikiwa tunafikiri kwamba hatutoshi, tunaanza na zana ambazo Yesu anahitaji kwa wanafunzi wake, lakini sio miundo, pesa na mali  kwa sababu kadiri tulivyo huru, rahisi, wadogo na wanyenyekevu, ndivyo Roho  mtakatifu anavyoongoza utume.

Misa kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma,Dominika 3 Julai 2022
Misa kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma,Dominika 3 Julai 2022

"Ndugu, hatutegemei utajiri na hatuogopi umaskini wetu, mali na ubinadamu. Kadiri tunavyokuwa huru na rahisi, wadogo na wanyenyekevu, ndivyo Roho Mtakatifu anavyoongoza utume na kutufanya kuwa wahusika wakuu wa maajabu yake. Mwachie Roho Mtakatifu nafasi. Acheni  nafasi. Kwake Kristo, nyenzo msingi ni ndugu. Cha kushangaza hiki. “Aliwatuma wawili wawili,” Injili inasema. Sio peke yao, daima na ndugu, kuwa karibu naye. Kamwe bila kuwa na ndugu, kwa sababu hakuna utume  bila muungano”.

Misa kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma,Dominika 3 Julai 2022
Misa kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma,Dominika 3 Julai 2022

Mshangao wa pili wa utume ni ujumbe, uliomo katika vifungu vichache vya Yesu, anayewaomba wafuasi wake kuwa mabalozi wa amani na kutangaza kwamba "Ufalme wa Mungu umekaribia". Wakristo  hawajitambui kwa hotuba zilizoelezewa vizuri, lakini kwa sababu wanafanya bidii ili kuleta amani, kwa sababu Kristo ni amani. Hii ndiyo alama mahususi": Ikiwa, kwa upande mwingine, tunaeneza porojo na tuhuma, tunaunda migawanyiko, tunazuia muungano au kutanguliza mali yetu mbele ya kila kitu, hatufanyi kwa jina la Yesu. Na wala kuleta amani”.

Misa kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma,Dominika 3 Julai 2022
Misa kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma,Dominika 3 Julai 2022

Kwa maana hiyo Papa Francisko ndipo ametoa wito kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ili kushinda kishawishi cha chuki na kulipiza kisasi, na kwa Wakristo kuwa waendelezaji wa amani, kuanzia mioyo mwao wenyewe, ili kubadilisha jamii na nchi kwamba: “Ukiishi na amani yake, Yesu anafika na familia yako, jamii yako inabadilika. Zinabadilika kwanza ikiwa moyo wako hauko vitani , hauna silaha na chuki na hasira, haugawanyiki, sio ndumila kuwili na sio ya uongo. Kuweka amani na utulivu ndani ya moyo wa mtu, kupunguza uchoyo, kuzima chuki na hasira,  kukimbia ufisadi, kukimbia udanganyifu na hila na hapa ndipo amani huanza”.

Misa kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma,Dominika 3 Julai 2022
Misa kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma,Dominika 3 Julai 2022

Wanafunzi wa Yesu na Wakristo wote pia ni watangazaji wa ukaribu wa Ufalme wa Mungu,  Papa amethibitisha  kwamba bado  ni kutazama Injili ya Luka na ulimwengu wa sasa ambapo ni muhimu kwa sababu ni kutoka hapo ndipo linafika  tumaini na uongofu, kutokana na kuamini kwamba Mungu yuko karibu na hutuangalia, Yeye ni Baba yetu sisi sote, anayetutaka sisi sote kuwa kaka na dada. “Ikiwa tunaishi chini ya mtazamo huo, ulimwengu hautakuwa tena uwanja wa vita, lakini bustani ya amani; historia haitakuwa mbio za kumaliza kwanza, bali itakuwa hija. Yote haya tuyakumbuke vizuri kwa sababu hayahitaji hotuba kubwa, lakini maneno machache na ushuhuda mwingi”.

Misa kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma,Dominika 3 Julai 2022
Misa kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma,Dominika 3 Julai 2022

Mshangao wa mwisho wa utume ambao sisi sote tumeitwa, unahusu mtindo wetu. Kwa mara nyingine tena mtazamo wa Papa Francisko umeelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambayo alipaswa kuitembelea kwa kuanzia tarehe  2 na 5 Julai.  Papa amesema “Ikiwa Yesu anabainisha kwamba anawatuma wanafunzi wake ulimwenguni kama kondoo kati ya mbwa mwitu, ina maana kwamba anataka tuwe huru dhidi ya ukuu na ukandamizaji, uchoyo, milki”. Anayeishi kama mwana-kondoo hashambulii, sio mlafi, yuko kundini, pamoja na wengine, na hupata usalama kutoka kwa Mchungaji wake, sio kwa nguvu au kiburi, sio kwa uchoyo wa pesa na mali ambayo pia husababisha, madhara mengi  hata kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Mwanafunzi wa Yesu anakataa jeuri, hamdhuru mtu yeyote, ni mwenye amani, anapenda kila mtu. Na ikiwa jambo hilo linaonekana kwake kuwa ni mpotevu, anamtazama Mchungaji wake, Yesu, Mwana-Kondoo wa Mungu ambaye aliushinda ulimwengu hivyo msalabani. Kwa maana hiyo, kukataa roho ya ulimwengu ambayo hufanya vita ambavyo vinaharibu na kumwomba Bwana  ndiyo  maneno ya Papa Francisko kwa kuhitimisha ili atusaidie kuwa wamisionari leo hii na  kwenda pamoja kama  kaka na dada; tukiwa na amani na ukaribu wa Mungu midomoni mwake;kwa kubeba moyoni upole na wema wa Yesu.

Misa kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma,Dominika 3 Julai 2022
Misa kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma,Dominika 3 Julai 2022

Asante sana ni salamu kutoka kw Sr.  Rita mara baada ya Misa Takatifu

Mara baada ya Misa na sherehe, ulikuwa ni mtazamo wa Baba Mtakatifu  Francisko kuelekea Afrika na hasa kwa wakazi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wasiwasi wake na wito wake wa amani, ulisukuma maneno ya shukrani kutoka kwa Sr  Rita Mboshu Kongo. Mwanataalimungu wa Congo wa Shirika la Mabinti wa Maria Mtakatifu aliyotamka na kusema ASANTE kwa niaba ya wote  kwa lugha nne za kitaifa kabla hajakumbuka upendo kiasi gani wa Papa ambao ameweza kuadhimisha Misa ya kwanza katika ibada ya Kongo mnamo tarehe 1 Desemba 2019.  Baadaye kupyaisha tumaini kwamba  safari inayotarajiwa ya Afrika inaweza kufanyika, mahali ambapo watu walikuwa wakimngojea kwa mikono miwili na kuendelea kuombea afya yake.

Misa kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma,Dominika 3 Julai 2022
Misa kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma,Dominika 3 Julai 2022
Misa kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma,Dominika 3 Julai 2022
Misa kwa Jumuiya ya Wakongo wanaoishi Roma,Dominika 3 Julai 2022
Misa ya Papa kwa Jumuiya ya Wakongo Roma 3 Julai 2022
03 July 2022, 14:00