Tafuta

Ujumbe wa Siku ya Maskini duninia 2022 unaongozwa na kauli mbiu:Yesu Kristo alijifanya Maskini kwa ajili yenu 2 Kor 8,9 Ujumbe wa Siku ya Maskini duninia 2022 unaongozwa na kauli mbiu:Yesu Kristo alijifanya Maskini kwa ajili yenu 2 Kor 8,9 

Ujumbe wa Siku ya Maskini Duniani 2022:Yesu Kristo alijifanya Maskini kwa ajili yenu!

Katika Ujumbe wa Siku ya VI ya Maskini Duniani 2022,Papa amerejea kunyanyapaa maafa ya vita nchini Ukraine:Nguvu kuu inakusudia kulazimisha mapenzi yake dhidi ya kanuni ya kujitawala kwa watu.Wito:Mbele ya maskini,hakuna kurudi nyuma,lazima kukunjua mikono:Onyo dhidi ya pesa,"kushikamana kupita kiasi kunatia ukungu wa mtazamo".Kauli ya Ujumbe:“Yesu Kristo alijifanya Maskini kwa ajili yenu 2 Kor 8,9.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Maskini na waliolazimika kuwa maskini kutokana na dhoruba ya janga la uviko, wafukara, wakimbizi na waliohamishwa na vita huko Ukraine, ambapo uingiliaji wa moja kwa moja wa nguvu kubwa inakusudia kulazimisha mapenzi yake dhidi ya kanuni ya kujiamulia kwa watu.  Hawa na wengine ndiyo Baba Mtakatifu Francisko anajikita kueleze katika Ujumbe wake wa Siku ya VI ya Maskini Duniani 2022  itayoadhimishwa tarehe 13 Novemba Ijayo na unaoongozwa nakauli mbiu kutoka kifungu cha Mtakatifu Paulo kisemacho: “Yesu alijifanya Maskini kwa ajili yenu”(2 Cor 8,9). Ni hati ndefu iliyochapishwa Jumanne tarehe 14 Juni 2022 na ambayo imetiwa saini katika siku kuu ya Mtakatifu Antony wa Padua tarehe 13 Juni.

Tayari ulianza kufunguliwa dirisha la uchumi kusaidia waliogeuka kuwa maskini

Katika ujumbe wake Papa Francisko anarudia tena kunyanyapaa tangu mistari ya kwanza moja ya sababu kuu za umaskini wa wakati wetu kwamba ni vita. Mkasa, ambao ulionekana miezi michache iliyopitia, wakati dunia ilikuwa inajaribu kuondokana na dhoruba ya janga, kwa kuonesha ishara za kurudisha uchumi ambao ungeweza kusaidia mamilioni ya watu waliogeuka kuwa maskini kwa sababu ya kukosa ajira. Papa anasema, ulikuwa unafunguliwa mtazamo wa utulivu ambao bila kufanya kusahau uchungu wa kupoteza ndugu binafsi, ulitoa matarajio ya kuweza kurudia hatimaye katika uhusiano binafsi, moja kwa moja na bila vizingiti vipya au kufungwa. Lakini tazama kwa balaa jingine lililo kwenye upeo ambao limependelea ulimwengu kuwa na hali tofauti hasa kwa wenye nguvu kutisha na kufunika kilio cha amani ya maskini.

Kila kona upuuzi wa vita unazalisha maskini wangapi?

Katika ujumbe wake  Papa Francisko amebainisha kuwa Mgogoro ambao umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya siku mia moja, umeongezea vile  vita vya kikanda ambavyo katika miaka ya hivi karibuni vimekuwa vikivuna kifo na uharibifu, lakini  picha inajidhihirisha kuwa ngumu zaidi. Matukio ya kumbukumbu ya kutisha yanarudiwa na kwa mara nyingine tena usaliti wa baadhi ya watu wenye nguvu unafunika sauti ya ubinadamu unaotamani amani. Wanyonge na wasio na ulinzi wamekumbwa. Papa Francisko anatoa mshangao kwamba: "Je, upuuzi wa vita unazalisha maskini wangapi! Popote unapotazama, unaweza kuona jinsi jeuri inavyoathiri wasio na ulinzi na dhaifu zaidi. Kufukuzwa kwa maelfu ya watu, hasa wavulana na wasichana, ili kuwang'oa na kuwalazimisha utambulisho mwingine. Mamilioni ya wanawake, watoto na wazee wanalazimika kukaidi hatari ya mabomu ili kujiokoa kwa kutafuta hifadhi kama wakimbizi katika nchi jirani. Wale ambao wamesalia katika maeneo ya migogoro, wanaishi kila siku kwa hofu na ukosefu wa chakula, maji, huduma za matibabu na zaidi ya yote mapendo kwa ndugu zao.

Kadiri mzozo unavyoendelea ndivyo idadi inazidi kuwa mbaya

Baba Mtakatifu anaeleza katika ujumbe huo kwamba katika hali hizi, sababu inafichwa na wanaopatwa na matokeo ni watu wengi wa kawaida, wanaokuja kuongeza idadi kubwa ya watu waliokuwa maskini tayari. Si hiyo tu, kwani kadiri mzozo unavyoendelea, ndivyo matokeo yanavyozidi kuwa mabaya zaidi. Msukumo, kwa hiyo, wa watu wote ambao katika miaka ya hivi karibuni wamefungua milango yao kuwakaribisha mamilioni ya wakimbizi kutoka Mashariki ya Kati,  Afrika na sasa Ukraine, pamoja na kujitolea kwa familia nyingi ambazo zimefungua nyumba zao ili kutoa nafasi kwa familia nyingine, inagongana na ukali wa ukweli usio na udhibiti,  kwa maana Watu wanaokaribisha wanazidi kujitahidi kutoa mwendelezo wa uokoaji lakini  familia na jamii zinaanza kuhisi uzito wa hali ambayo inapita zaidi ya dharura.

Sio wakati wa kukata tamaa bali kukamilisha kilichoanzishwa

Katika hivyo Baba Mtakatifu amesema kuwa, sasa ni wakati wa kutokata tamaa na kufanya upya motisha wa awali, kwa  kile ambacho tumeanzisha kinahitaji kukamilishwa na wajibu sawa. Mshikamano ni huu hasa wa kushiriki kidogo tulichonacho na wale wasio na kitu, ili mtu yeyote asiteseke. Kadiri hali ya jamii na ushirika inavyozidi kukua, ndivyo mshikamano unavyokua, amesisitiza Baba Mtakatifu. Zaidi ya hayo, katika ujumbe wa Papa anaandika, kwamba  lazima tuzingatie kuwa  kuna nchi ambazo, katika miongo ya hivi karibuni, kumekuwa na ukuaji mkubwa wa ustawi kwa familia nyingi ambazo zimefikia hali salama ya maisha. Hapa anataja kama  vile:  wanachama wa asasi za kiraia, na kwamba “tudumishe hai wito wa tunu za uhuru, uwajibikaji, udugu na mshikamano! Na kama Wakristo, daima tunapata katika mapendo, imani na matumaini msingi wa utu wetu na matendo yetu ambayo kiukweli, ndilo neno msingi”. Papa ameeleza kwamba “mbele ya maskini hakuna maneno, lakini mtu anakunja mikono yake na kuweka imani katika vitendo kupitia ushiriki wa moja kwa moja, ambao hauwezi kukabidhiwa kwa mtu yeyote”.

Matumizi mabaya ya fedha ni hali zinazodhihirisha imani dhaifu na tumaini dhaifu

Papa ametazama juu ya matumizi mabaya ya pesa na kuandika kuwa wakati fulani, hata hivyo, aina ya utulivu inaonekana kuchukua nafasi, na kusababisha tabia zisizo sawa, kama vile kutojali kwa maskini. Inatokea kwamba baadhi ya Wakristo, kwa sababu ya kushikamana kupita kiasi na pesa, wanajiingiza katika matumizi mabaya ya bidhaa na urithi. Hizi ni hali zinazodhihirisha imani dhaifu na tumaini dhaifu na lisiloona mbali. Kwa maana hiyo amefafanua kwamba suala sio shida ya pesa yenyewe, ambayo ni sehemu ya maisha ya kila siku ya watu na uhusiano wa kijamii, lakini thamani iliyo nayo kwetu. Ushikamano kama huo wa kupita kiasi hutuzuia kutazama kwa uhalisi maisha ya kila siku na hutia ukungu wa upeo weru, kukuzuia kuona mahitaji ya wengine. Hakuna kitu kibaya zaidi kingeweza kutokea kwa Mkristo na jumuiya kama kushangazwa na muungu wa utajiri, ambao mwisho wake ni mnyororo kwa maono ya maisha yasiyo na mafanikio. Baba Mtakatifu katika ujumbe wake wa Siku ya Maskini duniani 2022 amebainisha kwamba “sio uanaharakati unaookoa, kwani hili  sio suala la kuwa na tabia ya ustawi kwa maskini. Sio uanaharakati unaookoa, lakini  ni kuwa na umakini wa dhati na ukarimu unaoturuhusu kumwendea maskini kama kaka anayenyoosha mkono wake kwa sababu nimeokolewa kutokana na dhoruba ambayo ilikuwa imeniangukia.

Kitendawili kinachopingana na mantiki ya kibinadamu

Katika hilo ndipo  mwaliko mpya wa Papa wa sera mpya za kijamii katika kutafuta haraka njia mpya zinazoweza kwenda zaidi ya uwekaji wa sera hizo za kijamii zilizochukuliwa kama sera kuelekea maskini, lakini sio kwa maskini, na kamwe kuwa  na maskini na kuingizwa kidogo sana mpango unaounganisha watu.  Papa Francisko ameongeza kusema “Kuna kitendawili ambacho leo hii kama hapo zamani ni vigumu kukubalika, kwa sababu kinapingana na mantiki ya kibinadamu.  Na hiki ni kwamba kuna umaskini unaokufanya uwe tajiri ... Uzoefu wa udhaifu na mapungufu ambayo tumeishi katika miaka ya hivi karibuni, na sasa janga la vita na athari za ulimwengu, lazima lifundishe jambo la kuamua kwamba sisi  hatuko ulimwenguni kuishi, lakini ili kila mtu aruhusiwe kuishi  maisha yanayostahili  hadhi na yenye furaha.

Umaskini unaoua ni taabu binti dhuluma,unyonyaji,vurugu na migawanyiko

Kuna umaskini unaoua, Papa Francisko, katika hilo amebainisha kuwa Yesu mwenyewe anaonesha kwamba kuna umaskini unaofedhehesha na kuua, na kuna umaskini mwingine, wake, unaoweka huru na kuwafurahisha watu. Umaskini unaoua ni taabu, binti wa dhuluma, unyonyaji, vurugu na mgawanyo usio wa haki wa rasilimali. Ni umaskini wa kukata tamaa, bila mustakabali, kwa sababu umewekwa na utamaduni wa kutupa ambao hautoi matarajio au njia za kutokea. Hapa ni wakati sheria pekee inakuwa hesabu ya mapato wa mwisho wa siku, basi hakuna tena breki katika kupitisha mantiki ya kuwanyonya watu na wengine ni nyenzo tu. Hakuna tena mishahara wa haki, saa zinazofaa za kazi, na aina mpya za utumwa zinaundwa, zinazotesa na watu ambao hawana njia mbadala na lazima wakubali dhuluma hii yenye sumu ili kuweza kukwangua angalau pamoja kiwango cha chini cha riziki.

Umaskini unaokomboa ni chaguo la uwajibikaji kwa yake yaliyo muhimu

Na umaskini unaokomboa kwa upande mwingine, ni ule unaojitokeza mbele yetu kama chaguo la kuwajibika ili kupunguza nguvu na kuzingatia mambo muhimu. Kukutana na maskini amesema Papa kuwa “kunatuwezesha kukomesha wasiwasi na hofu nyingi zisizo na maana, kufikia kile ambacho ni muhimu sana katika maisha na kwamba hakuna mtu anayeweza kuiba kutoka kwetu ule  upendo wa kweli na wa bure. Maskini, kwa hiyo, kabla ya kuwa walengwa wa sadaka zetu, ni watu wanaotusaidia kutukomboa kutoka katika minyororo ya kutotulia na ya kijuu juu.”

UJUMBE WA PAPA FRANCISKO WA SIKU YA MASKINI DUNIANI 2022
14 June 2022, 16:39