Tafuta

Furaha ya Ndoa katika Familia. Furaha ya Ndoa katika Familia. 

Papa:Upendo wa familia ni wito na njia ya utakatifu

Baba Mtakatifu Francisko anawakumbusha waamini kwamba,Mkutano wa Kumi wa Familia Duniani ambo umepangwa kufanyika mjini Roma wiki kuanzia 22-26 Juni 2022

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko Dominika 19 Juni 2022 amewakumbusha Wakatoliki wota kwamba Mkutano wa Kumi wa Familia wa Ulimwengu (#WMOF22) utaanza mjini Roma mnamo Jumatano, tarehe 22 Juni. WMOF ni kifupi cha Mkutano wa Familia wa Ulimwengu, ulioanzisha na Papa Braza la Kipapa la  Walei, Familia na Maisha, mada inayoongoza ya mwaka huu  ni “Upendo wa Familia: Wito na Njia ya Utakatifu”.

Kila jimbo linaadhimisha siku ya familia na maaskofu wake

Badala ya mkutano wa hadhara duniani kote mwaka huu, imeamuliwa kuwa tukio hilo liadhimishwe katika kila  majimbo yote pamoja na maaskofu wa mahalia, kwa uzoefu maalum, wa ndani wa malezi, maombi na ushirika. Hata hivyo, wajumbe kutoka ulimwenguni kote watakuwepo kuanzia tarehe 22 hadi 26 Juni 2022 katika Ukumbi wa Paulo VI mjini  Vatican ambao watakuwa ni  wakiwakilishi wa familia za Kikatoliki duniani kote.

Kongamano, mkesha na tamasha

Kwa kuzingatia mapokeo, programu inajumuisha Kongamano la Kimataifa la Kitaalimungu-Kichungaji mwanzoni na mwisho mwa mkutano huo, mbele ya Papa Francisko, pamoja na mkesha na Tamasha la Familia litakalofuatiwa na  adhimisho kuu la mwisho la Ekaristi takatifu inayotarajiwa.

Mkutano mwaka huu unatofautiana na mikutano mingine ya kiutamaduni

Akizungumza mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana Dominika 19 Juni, kwa maana hiyo Papa Francisko amebainisha kuwa Mkutano huo utafanyika mjini Roma na wakati huohuo duniani kote. Na amewashukuru maaskofu, mapadre wa parokia na wachungaji wa familia ambao wameita familia katika nyakati za kutafakari, kusherehekea na sikukuu. Papa amesema:

“Zaidi ya yote, ninawashukuru wanandoa na familia ambao watatoa ushuhuda wa upendo wa familia kama wito na njia ya utakatifu. Muwe na  mkutano mwema!

19 June 2022, 15:40