Tafuta

2022.04.11 Mkutano wa X ulimwenguni wa Familia 2022: Nembo ya Mkutano huo! 2022.04.11 Mkutano wa X ulimwenguni wa Familia 2022: Nembo ya Mkutano huo! 

Papa Francisko:Papa awashukuru wanandoa na familia kutoa ushuhuda!

Hatimaye maandalizi ya Mkutano wa X wa Familia Duniani unafikia ukingoni kwani Jumatano 22 Juni unafunguliwa rasmi jini Roma.Mkutano huo unaongozwa na kauli mbiu:“Upendo wa Familia: wito na njia ya utakatifu”Tukio hili lilianzishwa mnano 1994.Na Papa Francisko anawashukuru maaskofu mapadre katika shughuli za kichungaji na wanandoa na familia ambao watatoa ushuhuda wa upendo wa familia kama wito na njia ya utakatifu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Hatimaye tumefikia Juma tuliolisubiri la Siku ya X ya Mkutano wa Familia duniani unaoongozwa na kauli mbiu Mada ya Upendo wa familia: wito na njia ya utakatifu, mada iliyochaguliwa na Baba Mtakatifu kuongoza siku hizi kuanza Jumatano tarehe 22 -26 Juni 2022. Ni juma litakaoona matukio mengi ikiwemo makongamano la kitaamungu na tafakari mbali mbali pamoja na matembezi katika maparokia kwa washiriki wote mjini Roma.

Hata hivyo Papa Francisko akizungumza mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana Dominika 19 Juni 2022, kwa mahujaji na waamini waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican, alielezea juu ya Mkutano huo mjini Roma na wakati huohuo duniani kote. Na aliwashukuru maaskofu, mapadre wa parokia na wachungaji wa familia ambao wameita familia katika nyakati za kutafakari, kusherehekea na sikukuu. Papa alisema: “Zaidi ya yote, ninawashukuru wanandoa na familia ambao watatoa ushuhuda wa upendo wa familia kama wito na njia ya utakatifu. Muwe na  mkutano mwema!

Waamini wakisali pamoja na Papa
Waamini wakisali pamoja na Papa

Kaulimbiu  mbiu inayoongoza mkutano wa kumi wa familia duniani unaturudisha katika kumbukumbu ya miaka mitano ya Wosia wa kitume wa  Papa Francisko wa Amoris Laetitia na miaka mitatu baada ya kutangazwa kwa Gaudete et exsultate ambapo yote pamoja ni kutoa nuru ya  upendo wa familia kama wito na njia ya utakatifu, kwa  kuelewa na kushiriki maana ya kina na ya mahusiano ya familia katika maisha ya kila siku.   Mkutano huo umeandaliwa na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha  ambao ilikuwa umeahirishwa mnamo 2021 kutokana na janga la Uviko -19.

Waamini wakisali pamoja na Papa
Waamini wakisali pamoja na Papa

Ndugu msomaji na Msikilizaji wa Vatican News,  tunapenda kuwakumbusha kwamba ilikuwa mwaka 1994 ambapo ilitangazwa na Umoja wa Mataifa  wa Mwaka wa Kimataifa wa Familia. Hata kwa Kanisa Katoliki , Papa ambaye ni Mtakatifu Yohane Paulo II naye  alitaka Mwaka wa Familia uadhimishwe kwa wakati mmoja na hivyo  Mkutano wa I wa Familia Ulimwenguni ulifanyika jijini Roma mnamo tarehe 8 na 9 Oktoba 1994, ukaendelezwa, kama mikutano mingine yote iliyofuata kwa kuandaliwa na Baraza la Kipapa la Familia la wakati huo. Tangu wakati huo, kila baada ya miaka mitatu, katika sehemu mbalimbali duniani, kumefanyika Mkutano wa Familia wa Ulimwengu, ulioanzishwa na kongamano la kimataifa la kitaalimungu-kichungaji na kuhitimishwa, mbele ya Papa, kwa mkesha wa sikukuu ya familia na adhimisho kuu la Ekaristi Takatifu ambalo daima limeona maaudhurio ya waamini wengi, familia kutoka pande zote za dunia, ili kushehereke maana na furaha ya kuishi kifamilia.

Kwa maana hiyo tunaweza kusema kwamba Mtakatifu Yohane Paulo II aliweza kuhudhuria: Mkutano I wa Dunia: mnamo tarehe 8-9 Oktoba 1994,  jijini Roma (Italia). Katika muktadha wa Mwaka wa Familia  ambao uliongozwa na Kauli mbiu: “Familia: moyo wa ustaarabu wa upendo”;  Mkutano wa  II wa Familia Duniani mnamo tarehe 4-5 Oktoba 1997 huko  Rio de Janeiro (Brazil) ambao ulikuwa ikiongozwa na kauli mbiu: “Familia: zawadi na kujitolea, tumaini la ubinadamu”;  Mkutano III wa Familia ulimwenguni  wa mnamo tarehe 14-15 Oktoba 2000 mjini Roma (Italia) katika muktadha wa Jubilei  ya  2000  kwa kuongozwa na kauli mbiu: “Watoto, chemchemi ya familia na jamii”; na uwepo wake kwa mara ya mwisho wa Mkutano wa IV wa Familia duniani mnamo tarehe 25-26 Januari  2003 huko Manila (Ufilipino). Ulioongozwa na kauli mbiu: “Familia ya Kikristo: habari njema kwa milenia ya tatu”.

Papa Mstaafu Benedikto XVI

Na kwa upande wa  Papa Mstaafu Benedikto  XVI  alidhuria Mkutano wa  V wa Familia Duniani mnamo tarehe 8-9 Julai 2006 huko Valencia (Hispania) ukiwa unaongozwa na kauli mbiu “kurithisha imani kwa familia”; Mkutano VI wa Familia  Duniani mnamo tarehe 17-18 Januari 2009 huko mji wa Mexico,  nchini (Mexico), ukiongozwa na kauli mbiu: “Familia, mwalimu wa maadili ya kibinadamu na ya Kikristo” na hatimaye  Papa Mstaafu Benedikto  XVI, aliudhuria  Mkutano wa  VII wa Familia duniani  mnamo tarehe  2-3 Juni  2012  huko Milano (Italia), kabla ya kustaafu kwake uliokuwa unaongozwa na kauli mbiu: “Familia - Kazi na Siku kuu”.

Papa Francisko

Kwa upande wa Baba Mtakatifu  Francisko aliudhuria Mkutano wa VIII wa Familia  Duniani mnamo  tarehe 26-27 Septemba 2015, huko Philadelphia (Marekani)  ukiongozwa na kauli mbiu: “Upendo ni utume wetu, familia iko hai kikamilifu”;  Na Mkutano wa IX wa Familia duniani ulifanyika jijini Dublin (Ireland) kuanzia tarehe 22 hadi 26 Agosti 2018 kwa kuongozwa na kauli mbiu  iliyochaguliwa na Papa Francisko:  Injili ya Familia: Furaha kwa Ulimwengu, ikiwa chini ya kivuli cha Wosia wa Kitume wa baada ya Sinodi  “Amoris Laetitia” na kuratibiwa na Baraza Jipya la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, inayoongozwa na Mwenyekiti Kardinali Kevin Farrell.

Kauli mbiu ya Mkutano wa X wa Familia duniani

Kwa maana hiyo maandalizi sasa yanatupeleka katika Mkutano wa X wa Familia duniani ambao unafanyika jijini kuanzia Jumatano tarehe 22 - 26 Juni  2022 jijini Roma, Italia kwa kuongozwa kwa namna hiyo na kauli mbiu: “Upendo wa Familia: wito na njia ya utakatifu”. Washiriki kutoka duniani wameanza kuwasili, na wakati huo huo, mabaraza mbali mbali ya maaskofu wameandaa tukio hili kuliishi kwa pamoja.

Papa amewatangazia juu ya Mkutano wa X wa Familia duniani unaofanyika Roma 22-26 Juni 2022
20 June 2022, 17:02