Tafuta

Papa aelekeza hatua kuelekea ndoa,msalaba,msamaha,ukarimu na udugu!

Papa Francisko ametoa hotuba yake katika Tamasha la Ufunguzi wa Mkutano X wa Familia duniani 2022 lililofanyika katika Ukumbi wa Paulo VI vatican.Baada ya kusikiliza shuhuda za baadhi ya uzoefu wa familia ameshukuru na kuwalekeza hatua tano za kuelekeza zaidi katika:ndoa; ya kukumbatia msalaba,kuwa na msamaha,ukarimu na hatimaye hatua zaidi kuelekea udugu kwa kuzingatia shuhuda tano zilizotolewa.

Na Angella Rwezaula- Vatican

Katika Ufunguzi wa tamasha la Mkutano wa X wa  Familia duniani uliozinduliwa jioni Jumatano tarehe 22 Juni 2022 katika Ukumbi wa Paulo VI,  Vatican, Baba Mtakatifu ametoa hotuba yake mara baada ya kusikiliza ushuhuda, awali ya yote akiwaleza furaha kubwa ya kuwa nao mara baada ya matukio mbali mbali ambayo yamegusa maisha yetu, awali ya yote janga la Uviko, na sasa vita barani Ulaya, kwa kuongezea vita vingine ambavyo vinatesa familia ya kibinadamu. Papa amemshukuru Kardinali Kevin Farell  na kardinali  Angelo dDe Donatis na wote kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Walei Familia na Maisha na Jimbo la Roma na kwa kujitoa kwao kuwezesha na kufanikia  mkutano huo. Amewashukuru wote waliofika kutoka pande zote za dunia kwa namna ya pekee wale ambao wametoa ushuhuda. Sio rahisi kuzungumza mbele ya umati kuhusiana na maisha binafsi, matatizo au zawadi za kushangaza ambazo wamepewa kutoka kwa Bwana, maisha yao yamekuwa  kama kipaza sauti cha uzoefu wa familia nyingi katika ulimwengu kama wao, ambao wanaishi furaha na wasi wasi, mateso na matumaini. Papa Francisko ameshauri kwamba wawe namna hiyo ya Kanisa. Kuwa Msamaria mwema ambaye anakuwa karibu na wao na anawasaidia kuendelea katika mchakato wa safari yao na kufanya hatua ya zaidi, hata ile ndogo. Ili kuweza kufanya hivyo amependa kuelezea hatua fupi pamoja kwa kuangazwa na shuhuda ambazo wamesikiliza.

Tamasha la Ufunguzi wa Mkutano X wa Familia duniani jijini Roma 22-26 Juni 2022
Tamasha la Ufunguzi wa Mkutano X wa Familia duniani 2022
Tamasha la Ufunguzi wa Mkutano X wa Familia duniani 2022

Baba Mtakatifu ameanza ufafanuzi wa Hatua zaidi kuelekea ndoa. Amemshukuru Luis na serena baada ya kusimulia uzoefu wao, matatizo na matarajio. Amefikiria kuhusu suala la kutopata jumuiya ambayo ilikuwa tayari kufungua mikono kuwakaribisha. Na kwamba hii lazima iwafanye wote kutafakari. Lazima kuongoka na kutembea kama Kanisa kwa sababu katika majimbo yetu, maparokia yetu daima yageuke kuwa jumuiya za msamaria na ambazo zinafungua mikono yao.  Kuna haja kubwa na kwa neema ya Mungu wameweza kupata msaada kutoka kwa familia nyingine na ambazo kiukweli ni makanisa madogo. Papa Francisko amesema tunaweza kusema kwamba mwanaume na mwanamke wanapopendana, Mungu anatoa zawadi kwao ile ya ndoa. Zawadi ya ajabu ambayo ndani mwake inabeba nguvu ya upendo wa mungu, wa nguvu na wa kudumu, mwaminifu, wenye uwezo wa kuanza upya mara baada ya kushindwa au udhaifu. Ndoa sio kanuni tu za kutimizia. Sio kuoa kwa ajili ya kuwa wakatoliki, kuwa na  lebo, kwa kutii kanuni au kwa sababu Kanisa linasema; Kuoa ni kwa sababu ya kutaka kusimika msingi wa ndoa juu ya upendo wa Mungu ambaye ni thabiti kama mwamba. Katika ndoa Kristo anajitoa kwao, kama wao walivyo na nguvu ya kujitoa kwa pamoja. Papa Francisko amewaomba wawe na ujasiri, maisha ya familia sio utume mmoja usiowezekana! Kwa neema ya Sakramenti, Mungu anafanya safari ya ajabu ya pamoja naye na sio wao peke yao. Familia sio wazo tu ambalo haliwezi kifikiwa kiuhalisia. Mungu anahakikisha uwepo wake katika familia na si tu katika siku ya harusi lakini katika maisha yote. Ni yeye anayesaidia kila siku katika  safari yao ya maisha.

Tamasha la Ufunguzi wa Mkutano X wa Familia duniani 2022
Tamasha la Ufunguzi wa Mkutano X wa Familia duniani 2022

Hatua ya zaidi kwa ajili ya kukumbatia msalaba. Papa amemshukuru Roberto na Maria Anselma ambao walisimulia historia ya kusisimua ya familia yao kwa namna ya pekee ya Chiara. Wamesimulia juu ya msalaba ambao ni sehemu yao maisha ya kila mtu na kila familia. Walishuhudia kwamba jaribu gumu la ugonjwa na kifo cha Chiara haukuharibu familia na wala kuondoa utulivu na amani mioyoni  mwao. Ilikuwa inaonesha hata katika nyuso zao. Wao hawakukata tamaa na wala kuwa na hasira ya maisha. Badala yake wanaonekana kuwa na utulivu na imani kubwa na hivyo utulivu wa Chiara iliwafungulia dirisha la umilele. Kuona jinsi alivyopitia majaribu ya ugonjwa huo inawasaidia kutazama juu na sio kubaki wafungwa wa maumivu, lakini kujifungulia kwa kitu kikubwa zaidi, miundo ya ajabu ya Mungu, umilele na Mbingu. Ninakushukuru kwa ushuhuda huu wa imani! Pia umenukuu msemo huo ambao Chiara alikuwa akisema: “Mungu huweka ukweli ndani ya kila mmoja wetu na haiwezekani kuuelewa vibaya”. Katika moyo wa Chiara Mungu aliweka ukweli wa maisha matakatifu, na kwa hiyo alitaka kuhifadhi maisha ya mwanawe kwa gharama ya maisha yake mwenyewe. Baba Mtakatifu Francisko ameongeza kusema kwamba “Na kama bibi arusi, pamoja na mume wake, alitembea njia ya Injili ya familia kwa njia rahisi, ya hiari. Ukweli wa msalaba pia uliingia ndani ya moyo wa Chiara kama zawadi binafsi:maisha yaliyotolewa kwa familia yake, kwa Kanisa na kwa ulimwengu wote. Daima tunahitaji mifano mikuu ya kutazama: Chiara awe msukumo katika safari yetu ya utakatifu, na Bwana awaimarishe na kuzaa matunda kwa kila msalaba ambao familia hujikuta wakiubeba.

Tamasha la Ufunguzi wa Mkutano X wa Familia duniani 2022
Tamasha la Ufunguzi wa Mkutano X wa Familia duniani 2022

Hatua ya mbele zaidi kuelekea msamaha. Paulo na Germaine, wamepata ujasiri wa kusimulia mgogoro walio uishi wa ndoa yao. Amewashukuru kwa hilo. Hawakutaka kuweka sukari katika hali halisi ili kuwa tamu. Waliita  hali hiyo kwa jina sababu za matatizo, ukosefu wa ukweli, uaminifu  matumizi mabaya ya fedha, miungu  ya uwezo na nafasi ya kazi, kuongezeka kwa hasira na ugumu wa moyo. Papa Francisko amebainisha kwamba,  wakati wao wanasimulia, Yeye alikuwa akifikiria wale wote ambao wameishi uzoefu wa uchungu mbele ya hali halisi zinazofanana na familia zilizotengana kwa sababu hiyo. Kuona familia ambayo inamegeuka ni janga ambalo haliwezi kuacha kujali. Tabasamu ya familia inapotea, watoto wanahangaika, utulivu wa wote unatoweka. Na wakati mwingine ni kutokujua nini la kufanya. Kwa maana hiyo historia yao inaonesha wazi matumaini. Paul alisema kwamba wakati wa giza la mgogoro, Bwana alijibu shauku ya kina ya moyo wake na kuokoa ndoa yao. Na ndiyo hivyo. Shauku ambayo imo ndani ya moyo wa kila mmoja wao ni kwamba upendo hauishi na kwamba historia iliyojengwa pamoja na mtu mpendwa isitikatike, na matunda yake yasipotee. Wote wanashaukuhiyo. Hakuna anayetamani upendo wa muda mfupi au wa kuisha.

Tamasha la Ufunguzi wa Mkutano X wa Familia duniani 2022
Tamasha la Ufunguzi wa Mkutano X wa Familia duniani 2022

Baba Mtamatifu alisema kwa  maana hiyo waliteseka ukosefu huo, kudharau na dhambi za binadamu ambazo zinatufanya kuharibu ndoa. Lakini hata katikati ya dhoruba. Mungu anaona kile kilichomo katika moyo Msamaha huponya kila jeraha, ni zawadi inayobubujika kutoka katika neema ambayo Kristo huwajaza wanandoa na familia nzima wanapomwacha atende, na wanapomgeukia. Ni vizuri sana kuwa wamesherehekea karamu yao ya msamaha, pamoja na watoto wao, wakifanya kwa upya nadhiri za ndoa katika adhimisho la Ekaristi. Papa amesema ilimfanya afikirie karamu ambayo baba alipanga kwa ajili ya mtoto mpotevu katika mfano wa Yesu(Lk 15,20-24). Wakati huu ndio tu wazazi waliopotea, sio mtoto! Lakini hii pia ni nzuri na inaweza kuwa ushuhuda mkubwa kwa watoto.

Tamasha la Ufunguzi wa Mkutano X wa Familia duniani 2022
Tamasha la Ufunguzi wa Mkutano X wa Familia duniani 2022

Kipengele cha nne ni hatua ya mbele zaidi kuelekea ukarimu. Papa Francisko amewashukuru Iryna na Sofia kwa ushuhuda wao. Wao wamewakilisha sauti kwa watu wengi ambao wamekumbwa na vita vya Ukraine. Kwa upande wao wanaonesha sura na historia za wanawake na wanaume wengi ambao wamelazimika kukimbia nchi zao. Amewashukuru kwa sababu hawakukatisha imani kutoka kwa Mpaji na waliona jinsi ambavyo Mungu anatenda wema hata kwa njia ya watu wa kweli ambao walikutana nao. Familia karimu, madaktari ambao waliwasaidia na watu wengi wenye moyo mzuri. Papa Francisko amesema kwamba vita vimetuweka mbele ya wasiwasi wa kibinadamu na ukatili, lakini pia umekutana na watu wa ubinadamu mkubwa. Mbaya zaidi na bora wa mwanadamu! Ni muhimu kwa kila mtu si kubaki umekodolea mabaya zadi  lakini kuthamini yaliyo bora, mazuri  ambayo kila mwanadamu ana uwezo, na kutoka hapo ni kuanza tena. Aidha Baba Mtakatifu amewashukuru Pietro ed Erika, ambao walisimulia ji ya ukarimu ambao waliwapokea Iryna na Sofia katika nyumba yao ambayo ilikuwa tayari ina idadi kubwa.  Wamewaaminisha kuwa walifanya kwa shukurani kwa Mungu na kwa roho ya imani, kama wito kwa Bwana.

Tamasha la Ufunguzi wa Mkutano X wa Familia duniani 2022
Tamasha la Ufunguzi wa Mkutano X wa Familia duniani 2022

Erica alisema kwamba ukarimu ulikuwa ni baraka kutoka mbinguni. Kiukweli ukarinu hasa ni karama ya familia na hasa ile yenye idadi kubwa! Wengine wanafikiria kwamba mahali am,bamo familia tayari ni kubwa ni  vigumu kukaribisha, kinyume chake sio hivyo, kwa sababu familia yenye watoto wengi imejifunza kupanua nafasi hata kwa ajili ya wengine. Kimsingi ndiyo mwenendo wa familia hasa. Katika familia wanaishi tabia ya ukarimu kwa sababu awali wanadoa walipokeana mmoja na mwingine na kama walivyosema pamoja siku ya kufunga ndoa: “Mimi ninakupokea wewe”. Na baadaye kuwaweka watoto ulimwenguni walipokea maisha ya viumbe wapya. Na wakati katika mutahda usiojulikana kuna walio wadhaifu zaidi ambao mara nyingi wametupwa, katika familia kinyume ni asili ya kukaribisha. Mtoto kwa ulemavu, mtu mzee mwenye kuhitaji utunzaji nzugu amwenye matatizo ambaye hana mtu. Haya ni matumaini. Familia ni mahali pa ukarimu, na ole ikikosekana! Jamii ingeweza kuwa barido na sio ya kuishi bila familia karimu.

Tamasha la Ufunguzi wa Mkutano X wa Familia duniani 2022
Tamasha la Ufunguzi wa Mkutano X wa Familia duniani 2022

Hatua ya mbele zaidi kuelekea udugu. Baba Mtakatifu amemshukuru Zakia kwa sababu ya kusimulia historia kati yake na Luka ambayo inabaki hai. Historia yake ilizaliwa na imesimika katika msingi juu ya ushirikishwaji wa mawazo ya juu, ambayo alielezea. Familia ya ilijikita juu ya upendo wa kweli, kwa heshima, mshikamano na mzungumzo kati ya viumbe. Hakuna lolote lililopotea na hata baada ya kifo cha Luka. Sio tu kiukweli mfano na urithi wa kiroho wa Luka unaobaki hai na kuzungumza katika dhamiri, lakini hata chama ambacho Zakia ameunda, kwa maana nyingine anapeleka mbele utume.  Zaidi ya hayo inawezekana kusema kuwa utume wa kidiplomasia wa Luka umekuwa sasa utume wa amani wa familia nzima. Katika historia yao inaonesha vizuri nini maana ya ubinadamu na kile cha kidini vinaweza kusukana pamoja na kutoa matunda mazuri sana. Kwa upande wa Zakia na Luka unapatikana uzuri wa upendo wa kibinadamu, na kile cha  maisha, shauku na hata uaminifu binafsi wa kuaminiana hasa tamaduni ya kidini, ambacho ni kisima cha kuchota na cha nguvu ya ndani. Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa katika familia yao inajifafanua wazo la udugu. Zaidi ya kuwa mume na mke, wao waliishi na udugu wa ubinadamu, wa ndugu katika uzoefu mbali mbali wa kidini, wa kuwa ndugu katika juhudi za kijamii. Hata hiyo ni shule ambayo inajifunza kuwa kaka na dada. Ni kujifunza kushinda migawanyiko, hukumu, kujifunga, na kujenga pamoja jambo kubwa na zuri kwa kuanzia na kile kinacho unganisha wote. Mfano wa uzoefu wa kuishi udugu kama ule wa Luka na Zakia, Papa amesema unatunapatia tumani na kutufanya kutazama kwa imani kuu ya udugu.

Tamasha la Ufunguzi wa Mkutano X wa Familia duniani 2022
Tamasha la Ufunguzi wa Mkutano X wa Familia duniani 2022

Papa Francisko amesema  kuwa kila familia yao ina utume wa kutumiza katika ulimwengu, na ushuhuda wa kutoa. Kama wabatizwa, kwa namna ya pekee wanaitwa kuwa ujumbe waRoho Mtakatifu anayeangaza utajiri wa Yesu Kristo na kutoa kwa watu wake (Esort. ap. Gaudete et exsultate, 21) Kwa maana hiyo Papa Francisko amependekeza kuwapa maswali: Ni neno gani ambalo Bwana anataka kuwambia katika maisha ya kila watu wanaokutana nao: Je ni hatua gani zaidi ambayo wanaombwa leo hii katika maisha yao?  Amewaomba wajiweke katika usikivu. Amewaomba waache wabadilishwe na Yeye kwa sababu hata wao wanaweza kubadilisha ulimwengu na kufanya  kuwa nyumba ambayo kwa yule mwenye kuhitaji anakaribishwa, kwa yule mwenye kuhitaji kukutana na Kristo na kuhisi anapendwa. Lazima kuishi na mtazamo kuelekea Mbinguni. Kama walivyokuwa wakisema Wenyeheri Maria na Luigi Beltrame Quatricchi kwa watoto wao, kukabiliana na ugumu na furaha ya maisha, kwa kutazama daima kuanzia paa hadi juu. Papa amewashukuru sana tena uwepo wao hapo na jitihada zao za kupeleka mbele familia zao. Amewaomba wasimsahaku katika sala zao.

Hotuba ya Papa kwa Tamasha la Mkutano wa X wa Familia duniani jijini Roma 22-26 Juni 2022
22 June 2022, 20:07