Tafuta

Papa ameomba msaada kwa ajili ya watu nchini Afghanistan waliokumbwa na tetemeko Papa ameomba msaada kwa ajili ya watu nchini Afghanistan waliokumbwa na tetemeko 

Papa ameonesha ukaribu kwa Afghanistan kwa sababu ya tetemeko

Waathirika na majeruhi wa tetemeko la Ardhi tarehe 21 Juni iliyokumba nchi ya Afghanistan,lakini hata uchungu kwa sababu ya mauaji ya Wajesuit wawili na Mlei mmoja nchini Mexico na ulazima wa kutosahau Ukraine nchi ambayo bado iko vitani ni mambo makuu yaliyosikika mara baada ya katekesi ya Papa Francisko Jumatano tarehe 22 Juni 2022.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko ameonesha ukaribu wake kwa wakazi wa  Afghanistan, waliokumbwa na tetemeko kubwa la ardhi tarehe 21 Juni 2022 usiku na kusababisha karibia waathirika  250. Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 5.9, kitovu chake ni kusini-mashariki mwa nchi hiyo, kwenye mpaka na Pakistan, huku makumi ya watu wamejeruhiwa. Serikali imeomba msaada wa haraka kutoka katika mashirika ya kibinadamu ili kuzuia janga la kibinadamu.  Hayo yameonesha na Papa Francisko mara baada ya Katekesi yake Jumatano tarehe 22 Juni 2022 kwa waamini na mahujaji , wakati wa salamu zake kwa lugha ya kiitaliano. Papa amesema: “Katika saa chache zilizopita, tetemeko la ardhi limesababisha waatika na uharibifu mkubwa nchini Afghanistan, Ninaonesha ukaribu wangu kwa waliojeruhiwa na wale walioathiriwa na tetemeko la ardhi, na ninawaombea hasa wale ambao wamepoteza maisha yao na familia zao. Ninatumaini kwamba kwa msaada wa mateso yote ya idadi ya watu wapendwa wa Afghanistan inaweza kupunguzwa”.

Majeruhi wa tetemeko la ardhi nchini Afghanistan
Majeruhi wa tetemeko la ardhi nchini Afghanistan

Papa Francisko baadaye ameonesha pia  uchungu na kusikitishwa na mauaji, huko nchini Mexico, siku ya tarehe 20 Juni  kwa  ndugu wawili wa Shirika la  Kijesuit na mlei. Papa amesema kwamba “ Ni mauaji mangapi huko Mexico! Niko karibu kwa upendo na maombi kwa jumuiya ya Kikatoliki iliyoguswa na janga hili. Kwa mara nyingine tena, ninarudia kusema kwamba jeuri halisuluhishi matatizo bali huongeza mateso yasiyo ya lazima.” Watawa wawili, Javier Campos na Joaquin Mora, waliuawa kwa kupigwa risasi ndani ya Kanisa hilo huko Cerocahui, Tarahumara, katika Serikaòio ya kaskazini mwa Chihuahua. Kwa sasa, utambulisho wa mwathirika wa tatu bado haujafafanuliwa. Mienendo ya mauaji hayo bado haijafafanuliwa pia. Kupitia Twitter, Padre Arturo Sosa Abascal, Mkuu wa Shirika la Wajesuit alisema: ameshtushwa na kuhuzunishwa sana na kile kilichotokea na kuwahakikishia ukaribu wake na washirika wake huko Mexico na kwa familia za waathirika, akiwataka kuacha vurugu katika ulimwengu wetu na mateso mengi yasiyo na maana.

Mapadre wawili wajesuit waliouawa nchini Mexico
Mapadre wawili wajesuit waliouawa nchini Mexico

Hatimaye, kwa mara nyingine tena, mawazo ya Papa  Fransisko yaligeukiwa kwenye vita vya Ukraine ambavyo kwa maoni ya watu vinahatarisha kufunikwa, kama ambavyo tayari alibainisha wakati wa sala ya malaika wa bwana Dominika tarehe 19 Juni 2022. Baba Mtakatifu Francisko Papa alisema: “Watoto ambao walikuwa nami katika kigali cha kuzunguka (Papamobile) walikuwa watoto wa Ukraine: tusisahau Ukraine. Tusipoteze kumbukumbu ya mateso ya watu hao wanaoteswa. Watoto wadogo kutoka Ukraine, waliingia kwenye gari la Papa, walikaribishwa na shule ya msingi Alberto Cadlolo huko Roma ili kuwaruhusu kuendelea na masomo yao.

Masikitiko ya Papa kwa waathirika Afghanistan na huko mexico lakini pia Ukraine
22 June 2022, 16:09