Tafuta

2022.06.09 Papa na Taasisi ya Elimu ya Kikanisa  2022.06.09 Papa na Taasisi ya Elimu ya Kikanisa  

Papa akutana na mabalozi watarajiwa:muige Charles de Foucauld na Pietro Favre

Papa alitembelea Taasisi ya Kipapa ya Kikanisa Jumatano mchana,akazungumza na wanafunzi kuhusu habari za dunia na huduma ya kidiplomasia katika Kanisa.

Vatican News.

Kuna mtindo wa kuoneshwa wakati mtu ni mwakilishi wa Mfuasi wa Petro katika mataifa mengine. Mtindo ambao uhifadhi ndani na hali ya kiroho ya kipadre, unaolishwa na sala, na kwa nje nafsi thabiti ya kimisionari. Ni “mwalimu” maalum aliyetoa maelekezo haya muhimu kwa wanafunzi wa Taasisi ya Kipapa ya Kikanisa, shule ambayo inawawatayarisha watahiniwa kwa ajili ya huduma ya kidiplomasia ya Vatican. Papa Francisko aliitembelea taasisi hiyo siku ya Jumatano mchana, akikaribishwa na rais wa Taasisi hiyo, Monsinyo Joseph Marino, Mchumi na Mwadhiri wa masomo, Monsinyo Gabriel Marcelo Viola Casalongue, na Msimamizi wa kiroho, Padre  Mjesuti Orlando Torres.

Wanafunzi 36  wa Taasisi ya Kipapa ya Kikanisa na Papa Francisko
Wanafunzi 36 wa Taasisi ya Kipapa ya Kikanisa na Papa Francisko

Malezi na “mwaka wa kimisionari”

Waliokuwa wakimsikiliza Papa Francisko walikuwa ni Mapadre 36, ambao ni wanafunzi kutoka nchi 22 za mabara mbalimbali, ulimwenguni waliopata fursa ya kumuuliza Papa Francisko maswali mbalimbali kuhusu masuala ya sasa yahusuyo huduma ya kidiplomasia na matukio ya Kanisa na ulimwengu wa sasa kwa ujumla. Katika kuonesha vielelezo vya kipadre vya kuhamasishwa kwa ajili ya maisha ya kidiplomasia, Papa Fransisko aliwalekeza watakatifu wawili, Charles de Foucauld na Pietro Favre, wa kuigwa mfano pia akisisitizia umuhimu wa “mwaka wa kimisionari”, uzoefu ambao Papa aliuanzisha kama sehemu muhimu ya safari ya maandalizi ya wanadiplomasia wa Vatican. Na kwa maana hiyo ilikuwa na fundisho muhimu hasa kwa wanafunzi wanne wa kwanza ambao mwishoni mwa mwaka huu wa masomo wataondoka kwenda Brazil, Ufilipino, Madagascar na Mexico kutekeleza mafunzo yao ya umisionari.

09 June 2022, 17:26