Tafuta

2019.12.13  Uzinduzi wa kituo  makao ya Scholas Occurentes katika Jumbla la Mtakatifu Calisto mnamo 2013 2019.12.13 Uzinduzi wa kituo makao ya Scholas Occurentes katika Jumbla la Mtakatifu Calisto mnamo 2013 

Scholas Occurrentes imechaguiwa kuwa Chama cha waamini Kimataifa

Kwa maandishi ya mkono wake,Papa Francisko ameanzisha mfumo mpya wa kisheria wa Mfuko wa Kipapa.Tarehe 19 Mei katika Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana Papa atasindikiza uzinduzi wa Harakati ya Schola Occurentes.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Shughuli kubwa zaidi ya upendo wa Mfuko wa Kipapa wa Scholas Occurrentes, kama jumuiya ya jumuiya nyingine na harakati ya kielimu yenye tabia ya  watu wa kimataifa, leo hii inahitaji muundo wa kisheria unaoendana na ukweli huu mpya. Haya ndiyo yanasomeka katika  barua iliyoandikwa kwa mkono wake (chirografu) iliyotiwa saini na Papa Francisko, mnamo tarehe 19 Machi iliyopita, katika Siku kuu ya Mtakatifu Yosefu, ambapo Scholas Occurrentes inatambulika sasa kama harakati ya kimataifa ya elimu, inayodhibitiwa na Sheria zilizoidhinishwa na barua hiyo ya mkono wake.

Mwanzo wa Schola Occurrentes

Scholas ilizaliwa kutokana na programu za "Escuelas de vecinos" na "Escuelas hermanas", zilizoendelezwa katika jiji la Buenos Aires kwa mpango wa Kadinali Jorge Mario Bergoglio(Papa Francisko). Baadaye ilienea hadi katika mabara matano, ambapo iliimarishwa kama Mfuko wa kisheria wa kipapa, tarehe 15 Agosti 2015. Kwa maana hiyo Papa atazindua Harakati ya Kielimu ya Kimataifa ya Scholas Occurrentes wakati wa mkutano na vijana, tarehe 19 Mei 2022, saa kumi jioni katika Ukumbi Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana, Roma, katika  tukio ambalo linaweza pia kufuatiliwa kupitia  chaneli ya YouTube ya Vatican. Ni tukio ambalo litahudhuriwa na watu kutoka ulimwengu wa sanaa, michezo na teknolojia, wawakilishi wa asasi za kiraia kutoka nchi mbali mbali ambazo Scholas Occurentes ipo hai na vijana wengi ambao wameshiriki katika programu za kielimu ambazo shirika limeendeleza kwa miaka ya karibuni.

Mafundisho ya Papa Francisko

Papa Francisko anatarajia kutoa fundisho la uzinduzi wa Shule "Laudato Si'", ambapo washiriki 50 wanafunzi kutoka Argentina, Bolivia, Brasil, Chile, Colombia, Hispania, Haiti, Italia, Messico, Panama, Paraguay, Ureno na  Panama. Kwa mwaka, vijana hawa waliojikita katika utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja, wataendeleza mipango ya kijamii ya mazingira katika jumuya zao. Kiongozi wa U2 Bono Vox atakuwa mmoja wa wazungumzaji walioalikwa kuzungumza katika Shule. Hatimaye, hatua zilizopangwa kwa mwaka huu katika nchi mbalimbali ambako Harakati hiyo mpya wapo zitatangazwa.

18 May 2022, 16:07