Tafuta

2022.05.23 Papa Francisko amekutana na Watu wa Huduma ya Kujitolea wa Taifa la Italia. 2022.05.23 Papa Francisko amekutana na Watu wa Huduma ya Kujitolea wa Taifa la Italia. 

Papa:msaada wa kibinadamu na ukarimu nchini Italia,kwa wakimbizi kutoka Ukraine!

Papa Francisko amekutana na wafanyakazi wa kujitolea wa Ulinzi wa Raia wa Italia.Amewashukuru kwa kusaidia na kuwakaribisha nchini Italia wakimbizi kutoka Ukraine,hasa wanawake na watoto ambao wamekimbia vita hivi vya kipuuzi.Wema hauna kelele lakini huunda ulimwengu.Wito wa Papa Francisko ni kwamba Dunia inalia:“Tunapolazimisha mkono wetu,asili inaonesha uso wake wa kikatili"

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu 23 Mei 2022 amekutana na watu wa kujitolea katika huduma ya kitaifa ya Ulinzi wa Raia nchini Italia. Amemshukuru Rais wao kwa maneno na salamu zake kwa niaba ya wote. Papa anatambua vema juu ya shughuli yao na amependa kukumbuka wema ambao wamefanya kipindi chote cha janga la uviko hasa kwa wakati mgumu sana.  Wao walikuwa na uwezekano wa kusaidia familia zilizo dhaifu zaidi, walijikita katika huduma yao kusindikiza na usalama kuelekeza wazeee na watu walio katika mazingira Magumu. Waliwasaidia wengi ambao walikuwa wanaumwa, maskini au waliokuwa peke yako katika nyumba. Walishiriki katika kampeni ya chanjoa kwa umahiri  kwa njia za matendo ya kujitolea. Sawa sawa  na hiyo Papa amesema hapakukosekana na jitihada kwa ajili ya msaada wa kibinadamu na ukarimu nchini Italia, kwa wakimbizi waliotoka Ukraine, hasa wanawake na watoto waliokimbia vita hivi vya kipuuzi. Papa amewashukuru  kwa kile walichofanya na wanaendelea kufanya kwa ukimya.  Kwa papa ameongeza kusema:“Wema haupigi kelele lakini ni kujenga ulimwengu”.

Papa akutana na watu wa Huduma ya kujitolea kitaifa nchini Italia
Papa akutana na watu wa Huduma ya kujitolea kitaifa nchini Italia

Baba Mtakatifu Francisko amegusia juu ya ushuhuda wo wa jitihada. “Ni kweli kwamba hatuwezi kujiokoa wenyewe. Tunahitaji kueleza na kuona kwa hakika kuwa maisha yanategemeana na wengine na ambayo wema uambukiza. Kujifanya Ndugu kunaleta tija ya ubora, uwezekano  zaidi na mshikamano. Na wakati huo huo jamii yetu inageuka ya kushi”. Ulinzi wa kuhamasisha ni ule wa majanga ya mazingira. Papa Francisko amesema mara nyingi amekumbusha msemo mmoja kispanyola usemao: “ Mungu husamehe daima, watu wanasemahe mara chache, asili haisamehi katu”. Mabadiliko ya tabia nchi ya wakati wetu, yameongeza matukio mabaya sana. Athari hasa ni janga kwa watu wanaopoteza makazi yao kutokana na mafuriko ya njia za maji, vimbunga, kukosekana kwa utulivu wa kijiolojia. Dunia inalia! “Tunapolazimisha mkono wetu, asili inaonesha uso wake wa kikatili na mwanadamu anakandamizwa, analazimika kulia hofu yake. Kwa maana hiyo kuingilia kati kwa kikundi cha Ulinzi wa Kiraia pia ilikuwa muhimu katika tukio la matetemeko ya ardhi, kushuhudia wito wa kulinda watu walioathiriwa na majanga kama hayo. Ulinzi ni ishara ya utunzaji wa eneo unaloishi: “wewe ni ulinzi wa kuokoa maisha ya binadamu na kukuza jamii. Tumeitwa wote kuulinda ulimwengu na sio kuupora”.

Papa akutana na watu wa Huduma ya kujitolea kitaifa nchini Italia
Papa akutana na watu wa Huduma ya kujitolea kitaifa nchini Italia

Ulinzi pia ni kwa njia ya kuzuia. Baba Mtakatifu Francisko amesema kila mmoja anapenda na kutunza kwa uwajibikaji maalum wa adhi yake, na kushughulikia nchi yake, kama ilivyo kila mmoja na  lazima apende na kutunza nyumba yake ili isianguke kwa sababu haitatengenezwa na walio karibu. Hata wema wa dunia unahitaji kila mmoja alinde na kupenda ardhi yake(Fratelli tutti 143). Kulinda kwa maana hiyo ni kutunza. Kutambua  na kufanya kwa upole ikiwa tunatambua kuwa sisi tumelinda kwanza. Mungu ni Baba ambaye anatunza sisi sote na hakosi kamwe kutupatia upendo wake. Nabii Isaya anakumbusha kuwa Mungu alituchora katika viganja vya mkono wake (49,16), Yeye hatuachi kamwe, na daima anatuunga mkono, anatusindikiza, anatulinda na kutusaidia. Hata Zaburi inatukumbusha kuwa Bwana analinda watoto wake (116,6). Ikiwa tunahisi kulindwa na Yeye, basi tujifunze ukarimu kwa ulinzi kuelekeza kaka na dada, kama anavyofundisha wakati wote. Baba Mtakatifu Francisko amewaomba waendelee na shughuli yao ya wema kati ya walio na mahitaji , kwa mujibu wa ushuhuda angavu na kwa maombezi ya Msimamizi wao Padre Pio wa Pietralcina.

Papa akutana na watu wa Huduma ya kujitolea kitaifa nchini Italia
Papa akutana na watu wa Huduma ya kujitolea kitaifa nchini Italia

Hata hivyo  kabla ya kumaliza, amependa kusisitiza neno moja kuhusiana na kujitolea ambapo wao ni watu wa kujitolea. . Nilikutana na vitu vitatu nchini Italia ambavyo sijawahi kuona mahali pengine. Moja ya mambo haya matatu ni kujitolea kwa nguvu kwa watu wa Italia, wito wa nguvu wa kujitolea. Ni hazina: ihifadhi! Ni hazina yenu  ya kiutamaduni, itunze vizuri!” Papa amehitimisha kwa kuwasindikiza kwa sala zake na kuwabariki wao na familia zao. 

23 May 2022, 16:05