Tafuta

2022.05.19 Jumuiya ya Taasisi ya Kipapa ya Pio ya Romania. 2022.05.19 Jumuiya ya Taasisi ya Kipapa ya Pio ya Romania. 

Papa Francisko:makuhani wasiwe wa maabara ya kitaalimungu bali ukaribu na watu

Baba Mtakatifu amekutana mjini Vatican na Jumuiya ya Chuo cha Kipapa cha Pio cha Romania kikiwa kinaadhimisha miaka 85 tangu kuanzishwa kwake na kukumbuka miaka ya mateso ya kikomunisti katika nchi ya Ulaya Mashariki,ambayo ilishuhudia kwa ushujaa wa waamini wa Kikristo:imani inatokana na mizizi ambayo ni umaskini na utajiri wa Injili.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko Alhamisi tarehe 19 Mei 2022, amekutana na Jumuiya ya Taasisi ya Kipapa la Pio ya Romania katika fursa ya kuadhimisha miaka 85 ya kuanza taasisi hiyo. Amewasalimu Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki, Mapadre, wanafunzi na wafanyakazi wa Taasisi hiyo pamoja na Gambera kwa maneno ya hotuba yake kwa niaba ya wote. Papa amekumbusha miaka miwili iliyopita wakati aliadhimisha liturujia huko Blaj katika Kambi ya Uhuru na kuwatia moyo uvumilivu wa itikadi mpya huku wakitafuta kuondoa mizizi yake ambapo wakati mwingine zinapitia  njia ya hila, kutoka katika tamaduni zao za kidini na kiutamaduni. Kwa ujumla katika fursa hiyo ya Maadhimisho, hayo Papa aliwatangaza wenyeheri saba maaskofu wafiadini  kwa kuwataja kama mfano wa watu wa Romania.

Papa amekutana na Jumuiya  ya Taasisi ya Kipapa ya Pio ya Romania
Papa amekutana na Jumuiya ya Taasisi ya Kipapa ya Pio ya Romania

Baba Mtakatifu Francisko kwa wanafunzi wote hao amesema wakiwa katika mji wa Roma ambao unahifadhi ushuhuda wa Petro na Paulo, na wafiadini wengine, wanaweza kugundua kwa upya yale yaliyo timizwa katika mizizi yao kwa njia ya mafunzo na tafakari. Papa amesema wakati wa vita vya dunia, ambapo Kanisa la Kigiriki katoliki la Romania halikuwa na Maaskofu tena kutokana na kuuawa au kufungwa, Ioan Ploscaru wa Lugoj, akiwa gerezani kwa miaka 15 aliandika katika shajara lake: “Mapadre na Maaskofu wa Kanisa Katoliki la Kigiriki wanalikwa kwenye kipindi hiki kama tunu msingi ya maisha yao. Kwa maana hiyo ni neema ya kuweza kutoa kwa Mungu mateso binafsi na kushuhudia imani binafsi hata kwa gharama ya maisha”.  Papa  Francisko ameongeza, anayetoa maisha kwa ajili ya Injili anafikiria hivyo na anakumbatia jibu la Mungu kwa ubaya wa ulimwengu, anajikabidhi mwenyewe, anaishi upendo mnyenyekevu na wa bure wa Bwana ambaye alijitoa kwa ajili ya wa mbali na aliye karibu. Hiki ndicho kisima kilichoruhusu mizizi isimikwe kwa kina katika ardhi yao na kukua kwa nguvu sana na kutoa matunda. Kwa maana hiyo  wao ndio matunda hayo ya mizizi.

Papa amekutana na Jumuiya  ya Taasisi ya Kipapa ya Pio ya Romania
Papa amekutana na Jumuiya ya Taasisi ya Kipapa ya Pio ya Romania

Baba Mtakatifu Francisko amebainisha: “Mtazamo wa mipando wa kutaka kuwa na madaraka, kuwa na fedha kuwa na umaarufu, kuwa na starehe, kufanya kazi: hii ni kutaka kukua bila mizizi. Ni kweli kwamba kuna wengine wanakwenda kwenye mizizi kujificha huko, kwa sababu wanaogopa ukuaji, sivyo? Ni kweli. Unakwenda kwenye mizizi ili kupata nguvu, kupata juisi na kuendelea kukua. Huwezi kuishi kwenye mizizi na huwezi kuishi kwenye mti bila mizizi. Mila ma utamaduni ni sehemu ya ujumbe tunaoupokea kutoka katika mizizi: ndiyo inakupatia nguvu ya kusonga mbele leo bila kurudia katika mambo ya jana, lakini kwa nguvu sawa na msukumo wa kwanza”. Baada ya kuzungumza juu ya mzizi ameongeza ameendelea kutzzama wao na kwamba wao  wanasimika mizizi, na  wasisahahu ardhi nzuri ya imani. Ndiyo ilifanyiwa kazi na babu na bibi zao, wazazi wao na watu wao watakatifu wa Mungu.

Papa amekutana na Jumuiya  ya Taasisi ya Kipapa ya Pio ya Romania
Papa amekutana na Jumuiya ya Taasisi ya Kipapa ya Pio ya Romania

Wakati wanajiandaa kueneza imani, wafikirie wao na wakumbuke kuwa Injili haiwezi kutangazwa kwa maneno magumu lakini kwa kutumia lugha rahisi ya watu kama alivyotufundisha Yesu, Hekima inayojikita ndani. Kwa kusisitiza:  Injili ipitishwe kwa lugha mama rahisi kwa watu wa Mungu, kile ambacho watu wanaelewa, kwa urahisi. Wawe waangalifu na wasiwe makasisi wa serikali. “Kuweni wachungaji wa watu. Ukaribu na watu unaotoka nje. Paulo alimwambia Timotheo: "Mkumbuke mama yako na nyanya yako, mizizi yako, watu unaohusika. Na nabii aliacha hesabu kwamba ulichaguliwa kwa usahihi kutoka katika kundi: usisahau kundi ambalo ulichaguliwa kutoka kwao: ni mali yako ya kwanza. Mwandishi wa Waraka kwa Waebrania analipendekeza hivi: “Wakumbukeni baba zenu waliowahubiria Neno la Mungu”. Tafadhali usisahau watu unaotoka. Msiwe makuhani wa maabara ya kitaalingu: hapana, Makuhani kutoka kwa watu, kwa harufu ya watu, na harufu ya kundi. Nilisema kwamba Injili haitangazwi kwa maneno magumu bali kwa lugha mama”.

Baba Mtakatifu akiendelea amesema ardhi nzuri  ndiyo ile inayowafanya waguse mwili wa Kristo, uliopo kwa maskini, kwa wagonjwa, wanaoteseka, kwa wadogo na walio rahisi, kwa yule anayetekeseka na ndimo alimo Yesu. Kwa  kuongeza amefikiria kwa namna ya pekee wakimbizi wa sasa wa Ukraine hata Romania wanawapokea na kuwasaidia. Akiwageukia wanafunzi, wa lugha ya kiarabu ambao wanatoka katikaTaasisi ya zamani ya Mtakatifu Efrahim amesema, kwa miaka karibu kumi wanaunda Jumuiya moja. Ushiriki wako wa maisha haupaswi kuhisi kama upungufu wa sifa zao tofauti, lakini kama ahadi yenye matunda ya siku zijazo. Wanafunzu wa Kitaifa, magharibi na kilatino hawapaswi kujisikia wakuu ambamo watarudi baada ya ya mowa wa masomo kuishi kana kwamba wako nyumbani, lakini kama warsha za ushrikiano wa umoja wa kindugu, ambapo watapata uzoefu wa ukatoliki wa dhati wa  umoja wa Kanisa. Umoja huu ni hewa nzuri ya kupumua ili kutokuwa na mambo fulani yanayozuia uinjilishaji. Kwa kuhitimisha amekumbusha tena mambo matatu aliyowaeleza, kusimika mizizi, ardhi, na hewa nzuri. Na kuwatakia kwa pamoja kuhamaisha namna hiyo wito wao kwa miaka ya aadhimisho . Amewaomba wasisahau kusali kwa ajili yake.

19 May 2022, 17:28