Tafuta

2022.05.16 Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Wahudumu wa Wagonjwa la Mtakatifu Camillo de Lellis. 2022.05.16 Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Wahudumu wa Wagonjwa la Mtakatifu Camillo de Lellis. 

Papa Francisko,Wakamiliani:wawe wasamaria wema katika Kanisa

Papa Fransisko akikutana na washiriki Mkutano Mkuu wa 59 wa Shirika wa Wakamiliani ambao ni Wahudumu wa Wagonjwa,na ambao wamemchagua mkuu mpya,Padre Pedro Tramontin wa Marekani,ameomba wabebe majeraha na mahangaiko ya kaka na dada walio hatarini zaidi,kwa kuendeleza mfano wa mwanzilishi wa Shirika Mtakatifu Camillo De Lellis aliyebadilishwa na upendo wa Mungu

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu tarehe 16 Mei 2022 amekutana mjini Vatican na Shirika la Wahudumu wa Wagonjwa wa Mtakatifu Camillo wakiwa katika fursa ya Mkutano wao Mkuu. Amewasalimu wote na kuwatakia kila jema na zaidi huduma ya Mkuu wa Shirika. Kitovu cha tafakari yao kwa siku zao za mkutano walioongozwa na mada ya “Ni unabii upi wa wakamiliano leo hii? Papa amesema kwa kuongozwa na neema ya Mkutano mkuu wameishi vema katika kusikiliza roho, ndugu na historia. Wao wamejikita kutafuta njia mpya za uinjilishaji na ukaribu ili hatimaye kutimiza kwa uaminifu mwenendo wa karama yao na kujikita katika huduma yao kwa wagonjwa. Mtakatifu Camillo De Lellis kwa kubadilishwa kwa upendo wa Mungu alihisi wito wa kujitoa maisha kwa ajili ya Familia mpya ya kitawa ambayo kwa kuiga mfano wa mateso na huruma ya Yesu kuelekeza wenye mateso katika mwili na katika roho, aishi amri ya upendo kwa kueneza kwa furaha tangazo la Injili, na kwa kutunza zaidi walio wadhaifu.

Mkutano wa Papa na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Wakamiliani
Mkutano wa Papa na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Wakamiliani

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea amesema, wakati wetu umekabiliwa na ubinafasi na sintofahamu ambayo inazalishwa upweke na kusababisha ubaguzi wa maisha mengi.  Huu ndio utamaduni wetu leo hii. Papa ameongeza kusema: “Ubinafsi, kutojali ambako kunasababisha upwekwe na kuzalisha ubaguzi na hivyo unakuwa utamaduni wa kutupa”. Akiendelea amesema Jibu la kikristo katika kutazama, si kukata tamaa, kujiachia wakati uliopo au kulilia ya zamani, lakini ni katika upendo ambao unaongozwa na imani ya Mungu mpaji, na hivyo anajua kupenda wakati wake na kwa unyenyekevu na kutoa ushuhuda wa Injili. Kwa kile ambacho alitimiza Mwanzilishi wao na ambaye ni moja ya sura za watakatifu ambao walijikita katika vema kwenye mtindo wa Msamaria mwema, wa kujifanya karibu na ndugu aliyejeruhiwa katika njia. Katika uchaguzi wa maisha, kwa maana hiyo kuna kubadilisha dira kutoka katika ulimwengu ulio fungwa na kuzalisha ulimwengu ulio wazi (Fratelli tutti 1-3).

Mkutano wa Papa na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Wakamiliani
Mkutano wa Papa na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Wakamiliani

Baba Mtakatifu amesema, kazi wanayotakiwa ni kuiga kutoka kwake ili kutazama hali halisi ya mateso, ya ugonjwa na kifo kwa macho ya Mungu. Kwa kufanya hivyo watafanya unabii wa Wakamiliani,  unabii wa kina ambao unasukuma kubeba mizigo ya wengine, majeraha ya wengine, mahangaiko ya kaka na dada walio katika mazingira magumu. Kwa kufanya hivyo inahitaji ufunguzi wa upole kwa Roho Mtakatifu ambaye anahuisha kila mwenendo wa kitume: ma inahitaji aina fulani ya dozi ya shauku, ya kugundua, ya kupitia njia pamoja za kuvumbua kwa upya au kuendeza mifumo mipya ya nguvu ya karama na ya huduma ya wakamiliani. Mtindo wao wa maisha na utume, ambao unajikita hasa katika huduma kwa wagonjwa na watu walio wadhaifu na wazee, Papa amebainisha kwamba unakwenda sambamba na mambo mawili msingi ya maisha ya kikristo. Kwa upande mmoja inaanzia na shauku ya kushuhudia na udhati kuelekea kwa wengine, na kwa upande wa pili, ni mahitaji ya kuweza kujijua binafsi kwa mujibu wa sheria ya udugu kiinjili.

Mkutano wa Papa na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Wakamiliani
Mkutano wa Papa na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Wakamiliani

Papa Francisko amewaalika wote kuchaota daima kutoka katika kiini cha Heri ili waweze kupeleka kwa upole na urahisi, tangazo jema kwa maskini na watu wa mwisho leo hii. Amewatakia watiane moyo pamoja kwa imani kwamba wema wa pamoja wa kaka au dada anayeteseka ni zawadi iliyofanywa na Yesu mwenyewe na kwamba wanapohisi na kutoa kila siku furaha, hata kama haionekani kwa macho ya ulimwengu, haiwezi kamwe kupotea bali ni kama mbegu iliyoanguka katika ardhi inachupua na kuzaa matunda. Papa amewaomba wasidharau kutunza kumbu kumbu ya upendo wa kwanza ambao Yesu aliwapatia ndani ya moyo wao ili kupyaisha daima mizizi ya chaguzi zao za maisha ya kitawa. Kwa maana hiyo wanatakiwa daima kurudi katika mizizi ya upendo wa kwanza kwani ndipo hapo kuna utambuzi wa kitwa yaani kuwa na mazungumzo na Yesu, na kuitwa.

Mkutano wa Papa na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Wakamiliani
Mkutano wa Papa na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Wakamiliani

Katika nyayo za ubunifu wa Mkatifu Camillo, Papa Francisko amewatia moyo wa kushirikiana na Roho Mtakatifu katika kutafuta kila njia za kuweza kuishi karama ya huruma, kwa kuthaminisha hata mitindo inayostahili zaidi ya kushirikiana na walei, kwa namna ya pekee wahudumu wa kiafya. Kukuza kati yao na kwa wote tasaufi ya umoja ambao utawasaidia kufanya mang’amuzi vizuri kila ambacho Bwana anawataka kutoka kwao. Papa amewashukuru kwa kile ambacho wao ni, na kile ambacho wanafanya katika Kanisa. Na kwamba ikiwa wanataka kutoa huduma kwa watu , wanapaswa kuwa katika hosptiali kambini, mahali ambamo aliyejeuhiwa anaweza kukutana na kuhisi ukaribu na hutuma ya Kristo, ikiwa wanataka hili hawezi kufanya lolote zaidi ya Karama ya Mtakatifu Camillo de Lellis. Atafuta umoja katika utashi wa Bwana. Ni juu ya mikono, miguu, akili na moyo wa zwadi hiyo ya Mungu ili iweze kutoa shughuli ya Mungu katika kambi yao. Bwana awabariki kwa neema tele kazi yao ya Mkutano Mkuu na mama Maria awasindikize daima katika safari yao katika wakati ambao wanaisha wito wao. Amewaomba wasisahau kusali kwa ajili yake.

HOTUBA YA PAPA KWA WAKAMILIANI
16 May 2022, 16:43