Tafuta

Papa Francisko:Njia ya utakatifu haijafungwa,ni ya ulimwengu wote

Furaha ya watakatifu 10 wapya wa Kanisa,ambapo tarehe 15 Mei 2022 Papa amewatangaza akiwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro uliojaa waamini na mahujaji kutoka pande zote za dunia, kwa rangi ambazo zilifurahisha uwanja huo.Kati ya waamini hapakukosekana viongozi wa serikali mbali mbali, kuanzia na Rais wa Jamhuri ya Italia Bwana Sergio Mattarella.Hakuna utakatifu wa nakala, utakatifu ni asili.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameongoza adhimisho la Ekaristi Takatifu katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Dominika tarehe 15 Mei 2022, asubuhi yenye jua kali sana na ambapo amewatangaza watakatifu kumi. Hawa ni: Titus Brandsma, Lazzaro anayejulikana kwa jina la Devasahayam, César de Bus, Luigi Maria Palazzolo, Giustino Maria Russolillo, Charles de Foucauld, Marie Rivier, Maria Francesca di Gesù Rubatto, Maria di Gesù Santocanale na Maria Domenica Mantovani. Waamini zaidi 50,000 kutoka mataifa na mabara mengi wamefika Roma kusheherekea siku kuu ya wanaume na wanawake wengi waliowekwa wakfu, ambao pia wamepigiwa makofu ya nguvu, wakiwemo viongozi mbali mbali wa dini na serikali na hata Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella, alikuwa miongoni mwao.

Kutangazwa watakatifu kumi Mei 15 katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Kutangazwa watakatifu kumi Mei 15 katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Papa Francisko akianza mahubiri yake kwa waamini na mahujaji waliojazaamejikita juu ya Injili iliyosomwa ambayo Yesu anawakabidhi wanafunzi wake kabla ya kwenda kwa Baba yake maneno ambayo yanabainisha nini maana ya kuwa wakristo “Kama nilivyo wapenda ninyi, naye wapendeni wengine (Yh 13,34). Hii ndiyo mirathi ambayo Kristo aliacha, mantiki msingi kwa ajili ya kung’amua ikiwa kweli ni wanafunzi wake au hapana. Amri kuu ya upendo. Papa Francisko amependa kufafanua juu ya mambo mawili yaliyomo kwenye amri hiyo ya upendo  wa Yesu kwa ajili yetu: “kama nilivyo wapenda ninyi na upendo ambayo yeye anatutaka kushi “pendaneni kama nilivyo wapenda". Awali ya yote, Yesu alitupenda namna gani? Hadi kifo, hadi kujitoa zawadi yake binafsi.

Kutangazwa watakatifu kumi Mei 15 katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Kutangazwa watakatifu kumi Mei 15 katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Inashangaza kuona ambavyo yanatamkwa maneno hayo katika usiku wa giza, wakati hali halisi katika karamu kuu ilikuwa imejaa hisia kali na wasiwasi. Hisia kali kwa sababu Mwalimu anatoa buriani kwa wanafunzi wake; wasiwasi kwa sababu anatangaza kwamba mmoja wa wenzao atamsaliti.  Inawezekana kweli kufikiria uchungu wa Yesu aliyokuwa nao rohono mwake, giza nene katika moyo wa mitume na uchungu kwa kuona Yuda ambaye baada ya kuchovya kutoka kwa Mwalimu, alitoka nje katika usiku wa kumsaliti. Na saa ile ile  ya usaliti, Yesu anathibitisha  upendo kwa ajili ya wanafunzi wake. Kwa sababu katika giza, na dhoruba ya maisha, ni kujua udhihirisho kuwa  Mungu anatupenda. Mwanzo wa kuwa wakristo hakuna mafundisho na matendo lakini kuna mshangao wa kujigundua kupenda,kabla ya jibu. Wakati ulimwengu mara nyingi unapenda kutuaminisha kuwa tunathamani tu ikiwa tunasalisha matokea mazuri, Injili inatukumbusha kuwa ukweli wa ukweli sisi tunapendwa.

Kutangazwa watakatifu kumi Mei 15 katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Kutangazwa watakatifu kumi Mei 15 katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Walimu wa kiroho wa wakati wetu waliandika kuwa: "kabla ya chochote kile kutuona kama  mwanadamu, sisi tulitazamwa kwa upendo wa macho ya Mungu. Kabla ya mtu yeyote asikie kulia au kucheka kwetu, tulisikilizwa na Mungu wetu ambaye ni masikio kwa ajili yetu. Kabla ya mtu yoyote katika ulimwengu huu azungumze nasi, sauti ya upendo mielele ilikuwa imekwisha zungumza nasi (H. Nouwen, sentirsi amati 1997,50). Alitupenda sisi kwanza, alitungoja. Anatupenda. Anaendelea kutupenda, na huu ndio utambulisho wetu: kupendwa na Mungu. Hii ndiyo nguvu yetu: kupendwa na Mungu. Wakati mwingine kwa kusisitiza jitihada zaidi za kutimiza matendo mema,  tumzalisha wazo la utakatifu, linalojikita juu yetu, kuhusu ushujaa, binafsi, juu ya uwezo wa kujikatalia, kujisadaka kwa ajili ya kupata zawadi. Hivyo tukaufanya utakatifu kuwa lengo lisiloweza kushindikana, tukautenganisha na maisha ya kila siku badala ya kuutafuta na kuukumbatia katika maisha ya kila siku, katika vumbi la barabarani, katika taabu za maisha halisi na, kama Teresa wa Avila alivyowaambia watawa wenzake, kati ya sufuria za jikoni".

Kutangazwa watakatifu kumi Mei 15 katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Kutangazwa watakatifu kumi Mei 15 katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Na baadaye kutoa uzima, ambayo si tu kutoa kitu, kama vile baadhi ya mali ya mtu mwenyewe kwa wengine, lakini kujitoa mwenyewe. Papa amesema anavyo wauliza kama hao wanapotoa sadaka wanamuwangalia mtu machoni, au wanatazama kwingine?" jibu ni hapana hawafanyi hivyo  kwa njia hiyo ushauri ni kwamba waguse  na waangalie kwa maana ya kugusa na kutazama mwili wa Kristo anayeteseka ndani ya kaka na dada zetu. Hii ni muhimu sana. Na hii kutoa maisha ina maana hiyo. Utakatifu haujumuishwi na ishara chache za kishujaa, bali upendo mwingi wa kila siku. Je, wewe ni mtawa wa kike na kiume  aliyewekwa wakfu, na walikuwa wengi sana katika uwanja, Papa Francisko amewalenga ha na kuwalezea kuwa wawe  watakatifu kwa kuishi mchango wao kwa furaha.

Je, umeoa au umeolewa? Uwe mtakatifu na mtakatifu kwa kumpenda na kumjali mume au mke wako, kama Kristo alivyolitendea Kanisa. Je, wewe ni mfanyakazi, mwanamke, mwanaume mfanyakazi? Muwe watakatifu kwa kufanya kazi zenu katika huduma ya ndugu zenu  kwa uaminifu na umahiri na kupigania haki ya wenzako ili wasibaki bila ajira ili wawe na mshahara unaostahili siku zote... Je wewe ni mzazi au bibi au babu? Muwe watakatifu kwa kuwafundisha watoto kwa subira kumfuata Yesu. Papa ameendelea mbele zaidi kwa kusema “Unayo mamlaka? Na hapa kuna watu wengi ambao wana mamlaka! Nami nakuuliza: Je! unayo mamlaka? Iweni watakatifu kwa kupigania manufaa ya wote na kuachana na mambo yenu binafsi” (Apostolic Exhortation Gaudete et exsultate, 14). Hii ndiyo njia ya utakatifu, rahisi sana! Lakini, daima mwangalie Yesu katika wengine."

Kutangazwa watakatifu kumi Mei 15 katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Kutangazwa watakatifu kumi Mei 15 katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Kuhudumia Injili na ndugu, kutoa maisha kwa ajili ya mtu bila faida, hiyo ndiyo siri:, Papa ameseisitiza na kwamba "kutoa bila kusubiri faida, bila kutafuta utukufu wowote wa kidunia: sisi pia tunaitwa kwa hilo. Wenzetu katika safari, waliotangazwa kuwa watakatifu, waliishi utakatifu kwa njia hii: wakikumbatia wito wao kwa shauku kama padre, wengine, kama watawa, wengine, kama walei,  walijitolea kwa ajili ya Injili, waligundua furaha isiyo na kifani na wamekuwa tafakari tukufu za Bwana katika historia. Huyu ni mtakatifu wa kike na kiume ambao ni onesho zuri la Bwana katika historia.

Kutangazwa watakatifu kumi Mei 15 katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Kutangazwa watakatifu kumi Mei 15 katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Papa Francisko ameomba kujaribu hata wote pia kwa sababu njia ya utakatifu haijafungwa, ni ya ulimwengu wote, ni wito kwa sisi sote, inaanza na Ubatizo, haijafungwa. Hebu tujaribu pia, kwa sababu kila mmoja wetu ameitwa kwenye utakatifu, kwa utakatifu wa kipekee na usioweza kurudiwa. Utakatifu siku zote ni wa asili, kama Mwenyeheri Carlo Acutis alivyosema: hakuna utakatifu wa nakala, utakatifu ni asili, ni wangu na wako, wa kila mmoja wetu. Ni wa kipekee na hauwezi kurudiwa. Ndiyo, Bwana ana mpango wa upendo kwa kila mmoja, ana ndoto kwa maisha yako, kwa maisha yangu, kwa maisha ya kila mmoja wetu. Unataka nikuambie nini? Endelea kwa furaha. Amehitimisha Papa. 

TAFAKARI YA PAPA DOMINIKA 15 MEI WAKATI WA KUWATANGAZA WATAKATIFU
15 May 2022, 11:41