Tafuta

Papa Francisko amekutana na Klabu ya Tevere Remo mjini Vatican. Papa Francisko amekutana na Klabu ya Tevere Remo mjini Vatican. 

Papa akutana na Klabu ya Makasia ya Tevere Remo:kuzeni thamani ya michezo

Ni muhimu kwa kila hatua ya rika, hasa kwa vijana ambao hawatakiwi kusimama mbele ya vizingiti vya maisha,bali kushinda matatizo kwa ujasiri,imani kwa Mungu na binafsi na kwa msaada wa wengine.Kwa njia ya mchezo wao wanaitwa kuhamasisha thamani safi za mchezo,urafiki na mshikamano.Ndivyo Papa amesema kikutana na wajumbe wa Klabu ya Makasia Tevere Remo katika fursa ya kutumiza miaka 150.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 9 Machi 2022, amekutana na Circolo Canottieri Tevere Remo’ yaani  yaani Klabu ya Makasia ya Tevere na kumshukuru Rais kwa maneno yake. Mkutano huo ni katika fursa ya kuadhimisha miaka 150 tangu kuanzishwa Klabu hiyo. Papa amesema kuwa ni siku muhimu. Kupitia kwao, wazo la upendo la Papa pia limewaendea familia zao na wale wote ambao wamekuwa na ushirikiani huo wa kale. Maadhimisho ya mwaka huo yanatoa fursa kwa ajili ya kutafakari juu ya maana na mtindo wa uwezo wa chama chao, jijini Roma katika mkoa wa Lazio. Wao wanawakilisha hali halisi ya mchezo ambapo wanaklabu wanashinda zaidi kwa nidhamu, na hiyo inawaalika  harakati nzima kujikita katika safari.

Papa amekutana na Wanachama wa Klub ya Makasia Tevere Remo
Papa amekutana na Wanachama wa Klub ya Makasia Tevere Remo

Ni muhimu kwa kila hatua ya rika, hasa kwa ajili ya vijana ambao hawatakiwi kusimama mbele ya vizingiti vya maisha, bali kushinda matatizo kwa ujasiri, imani kwa Mungu na ndani mwao binafsi na kwa msaada wa wengine. Kwa njia ya mchezo wao wanaitwa kuhamasisha thamani safi za mchezo, ya urafiki na ya mshikamano. Hii ndiyo kueneza utamaduni wa mchezo ambao unatambua zoezi la mchezo si tu kama muktadha wa ustawi wa mwili, lakini kama wazo jasiri, na kama chombo cha ukuaji fungamani wa mtu. Katika mchakato wa miaka hiyo, wao wamejitahidi kupendekeza chama chao kama kiwanja cha mafunzo ya kibinadamu. Baba Mtakatifu amewatia moyo wa kuvumilia ili watoto, vijana na watu wazima waweze kukuza kwa njia ya michezo mbambali zile thamani muhimu, kama vile upendo kwa ukweli, na haki, kuheshimu kazi ya uumbaji, ladha ya uzuri na wema, utafutaji wa uhuru na wa amani.

Papa amekutana na Wanachama wa Klub ya Makasia Tevere Remo
Papa amekutana na Wanachama wa Klub ya Makasia Tevere Remo

Wakati mwingine ulimwengu wa michezo unaonekana kuteseka kutokana na hali ya mantiki ya faida na ushindani mkali, ambao unaweza pia kuharibika na kuwa matukio ya vurugu. Pia ni kazi ya ukweli kama wanashuhudia nguvu ya maadili ya shughuli za michezo ambayo, ikiwa itafanyiwa uzoefu kwa usahihi, husaidia kuanzisha urafiki mzuri na kupendelea ujenzi wa ulimwengu wa utulivu na wa kidugu, ambao mtu anaunga mkono na kusaidiana. Hasa kwao, wanariadha wapendwa, anawatakia mazoezi ya michezo kwa uaminifu na roho ya ushindani yenye afya. Kwa njia hii itawasaidia kukabiliana na mbio zinazodai maisha kwa ujasiri na uaminifu, kwa furaha na imani tulivu katika siku zijazo, wakiacha kungojea kwa subira wale ambao wanakimbia polepole na wana shida zaidi ya kutembea.

Papa amekutana na Wanachama wa Klub ya Makasia Tevere Remo
Papa amekutana na Wanachama wa Klub ya Makasia Tevere Remo

Rais wao ametoa vidokezo viwili ambavyo alitaka kuchukua tena. Cha kwanza ni Ukraine. “Katika siku hizi hatuwezi kuzungumza mambo mengine bila angalau kukumbuka, kukumbuka yaukatili unaoweza kufikiwa. Roho ya kimichezo, hii ya ustaarabu wenu, ni maandalizi ya kutoanguka katika mambo haya, kukuza urafiki wa kibinadamu hutuandaa kutoanguka katika janga hili na kufikiria wale watu ambao ni waathirika wa janga hili. Asante kwa kutaja Ukraine katika hotuba yako”. Papa amewakabidhi kwa Bwana na kwa maombezi ya Bikira Maria, Salus Populi Romani, 'yaani Maria Afya ya Waroma', familia nzima ya Kikundi cha Klabu ya Wanamakasia wa Tevere Remo (Circolo Canottieri Tevere Remo). Amewabariki na kuwatakia kila wema katika shughuli zao. Jambo la pili ambalo amesema ni kusali kwa ajili yake, kwa sababu naye anahitaji maana mchezo huo kwake sio rahisi.

HOTUBA YA PAPA KWA KLUB YA TEVERE REMO
09 April 2022, 16:13