Tafuta

Hija ya Kitume ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Iraq ilipania kujenga na kudumisha umoja na udugu wa kibinadamu. Hija ya Kitume ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Iraq ilipania kujenga na kudumisha umoja na udugu wa kibinadamu. 

Hija ya Kihistoria ya Baba Mtakatifu Francisko Nchini Iraq: Ushuhuda

Baba Mtakatifu amekuwa ni hujaji wa toba, ili kumwomba Mwenyezi Mungu msamaha, tayari kuanza mchakato wa upatanisho wa Kitaifa. Papa alikwenda nchini Iraq kama hujaji wa amani ili kukoleza majadiliano ya kidini na kiekumene muhimu kwa ujenzi wa udugu wa kibinadamu. Alipata nafasi ya kukutana na Kanisa la mashuhuda wa imani, ili kunogesha hija ya matumaini.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko kuanzia tarehe 5 hadi 8 Machi 2021 alifanya hija ya kitume nchini Iraq kwa kunogeshwa na kauli mbiu “Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu” Mt. 23:8. Baba Mtakatifu amekuwa ni hujaji wa toba, ili kumwomba Mwenyezi Mungu msamaha, tayari kuanza mchakato wa umoja na upatanisho wa Kitaifa. Baba Mtakatifu anasema, alikwenda nchini Iraq kama hujaji wa amani ili kukoleza majadiliano ya kidini, kiekumene na kitamaduni kama sehemu ya mchakato wa ujenzi wa mshikamano na udugu wa kibinadamu. Alipata nafasi ya kukutana mubashara na Kanisa la mashuhuda wa imani, ili kunogesha hija ya matumaini. Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 28 Februari 2022 amekutana na kuzungumza na wawakilishi wa Makanisa mbalimbali kutoka nchini Iraq kama sehemu ya kumbukizi la mwaka mmoja wa hija yake ya kitume nchini Iraq. Hii ni nchi ambayo inasimikwa katika ut una uhuru wa watu wake, na kamwe haiwezi kugeuzwa kuwa ni “uwanja wa vita.” Baba Mtakatifu katika hotuba yake amegusia umuhimu wa Iraq mintarafu Maandiko Matakatifu, changamoto ya wakimbizi na wahamiaji; umuhimu wa kujikita katika mchakato wa majadiliano ya kidini na kiekumene, ili kujenga na kudumisha umoja wa Kitaifa hata katika tofauti zao msingi na watambue kwamba, daima anawakumbuka na kuwaombea katika sala na sadaka yake.

Baba Mtakatifu Francisko anasema, hija yake ya kitume ya 33 kimataifa nchini Iraq ni kati ya hija ambazo zilikuwa hatari sana katika maisha na utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Alitumia muda mrefu kusali na kutafakari. Akapima madhara na faida yake kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu ndani na nje ya Iraq. Akajiaminisha mbele ya Mwenyezi Mungu na kuomba ulinzi na usalama kutoka kwa Bikira Maria, Afya ya Warumi, akapiga moyo konde na kuamua kwamba, kuanzia tarehe 5 hadi 8 Machi 2021 angefanya hija ya kitume nchini Iraq kwa kunogeshwa na kauli mbiu “Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu” Mt. 23:8. Baba Mtakatifu amekuwa ni hujaji wa toba, ili kumwomba Mwenyezi Mungu msamaha, tayari kuanza mchakato wa upatanisho wa Kitaifa. Baba Mtakatifu anasema alikwenda nchini Iraq kama hujaji wa amani ili kukoleza majadiliano ya kidini na kiekumene kama sehemu ya mchakato wa ujenzi wa udugu wa kibinadamu. Alipata nafasi ya kukutana mubashara na Kanisa la mashuhuda wa imani, ili kunogesha hija ya matumaini.

Papa Francisko alikuwa ni hujaji wa toba na imani
Papa Francisko alikuwa ni hujaji wa toba na imani

Hati ya Udugu wa Kibinadamu kwa Ajili ya Amani na Utulivu ilitiwa saini kati ya Baba Mtakatifu Francisko na Dr. Ahmad Al-Tayyib, Imam Mkuu wa Msikiti wa Al- Azhar, ulioko mjini Kairo, nchini Misri, tarehe 4 Februari 2019 huko Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu. Huu ni mwaliko na changamoto kwa waamini wa dini mbalimbali duniani, kuungana na kushikamana, ili kufanya kazi katika umoja na udugu wa kibinadamu, ili kujenga na kudumisha misingi ya haki, amani na maridhiano kati ya watu. Hati hii ni nguzo msingi ya haki, amani na upatanisho. Hati inakazia pamoja na mambo mengine kwamba: binadamu wote wameumbwa kwa sura na mfano wa Mwenyezi Mungu; wanatakiwa kusimama kidete kulinda, kutunza na kudumisha: uhai wa binadamu, mazingira nyumba ya wote, sanjari na kushikamana na maskini pamoja na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa vipaumbele vya jamii.

Baba Mtakatifu Francisko anasema Hati ya Udugu wa Kibinadamu kwa Ajili ya Amani na Utulivu ni sehemu ya mchakato wa majadiliano ya kidini na matunda yake ni Waraka wa Kitume wa "Fratelli tutti": Yaani “Wote ni Ndugu”: Kuhusu Udugu na Urafiki wa Kijamii”. Malengo ya Waraka wa Kitume:"Fratelli tutti" ni kuhamasisha ujenzi wa mshikamano wa kidugu unaoratibiwa na kanuni auni, kwa kutoa kipaumbele cha kwanza kwa utu, heshima na haki msingi za binadamu. Hii ni dhana inayokumbatia maisha ya kifamilia, kijamii, kitaifa na kimataifa. Ili kufikia lengo hili, kuna haja ya kujenga na kudumisha tasaufi ya udugu wa kibinadamu kama chombo cha kufanyia kazi katika medani za kimataifa, ili kusaidia kupata suluhu ya matatizo yanayoikumba Jumuiya ya Kimataifa. Huu ni msaada mkubwa katika kupambana na changamoto mamboleo kama vile: Vita na kinzani mbalimbali; baa la ujinga, njaa na umaskini duniani pamoja na athari za uharibifu wa mazingira nyumba ya wote.

Kipaumbele cha kwanza ni ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Mshikamano wa kidugu usaidie ujenzi wa mahusiano na mafungamano ya Jumuiya ya Kimataifa kama ilivyo pia miongoni mwa wananchi wenyewe. Ujasiri na ukarimu ni mambo yanayohitajika ili kufikia malengo ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Ayatollah Ali Sistani alisema, udugu wa kibinadamu unapata chimbuko lake katika kazi ya uumbaji inayowafanya kuwa ndugu na katika imani inayowaunganisha na kuwafanya kuwa ni ndugu wamoja. Usawa kama watoto wa Mungu ndilo jambo muhimu si tu katika masuala ya kidini bali hata katika utamaduni. Kwa Wakristo udugu huu umefunuliwa kwa njia ya Kristo Yesu, lakini imewachukua watu wa Mungu miaka mingi sana kuutambua na kuumwilisha udugu huu katika vipaumbele vyao vya maisha. Hati ya Udugu wa Kibinadamu kwa Ajili ya Amani na Utulivu kama nguzo ya majadiliano ya kidini, inalenga kudumisha amani duniani.

Papa Alisikitishwa kuona Makanisa mengi yakiwayameharibiwa kwa vita.
Papa Alisikitishwa kuona Makanisa mengi yakiwayameharibiwa kwa vita.

Ni sehemu ya utekelezaji wa maamuzi ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, kama hata kuanzishwa kwa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini. Hii ni hati ambayo imeandaliwa kwa sala na tafakari ya kina, ili kuweza kudhibiti: vita, uharibifu unaosababishwa na vitendo vya kigaidi, chuki na uhasama kati ya watu! Lengo ni kudumisha misingi ya haki, amani na maridhiano, chachu muhimu sana ya ustawi na maendeleo fungamani ya binadamu! Hakuna maendeleo ya kweli pasi na amani duniani. Hii ni hati inayopata chimbuko katika misingi ya imani kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa huruma na mapendo! Iliandaliwa kwa usiri mkubwa. Lakini pamoja na faida zote hizi, Baba Mtakatifu Francisko mara kwa mara amekuwa akipokea shutuma kali dhidi yake na wakati mwingine inambidi kufanya maamuzi mazito! Haya ni maamuzi yanayotolewa baada ya sala, tafakari ya kina na ushauri.

walivyopokonywa hata ile hali ya kuishi kwa amani na hivyo kushindwa kuendelea kuwa ni mashuhuda na vyombo vya uhuru, amani na maridhiano kati ya watu. Kumbe, Baba Mtakatifu Francisko kusimama kitambo kidogo nchini Lebanon kama alivyokuwa ameombwa ingekuwa ni kutowatendea haki na heshima kutokana na matatizo, changamoto pamoja na fursa wanazokabiliana nazo. Lebanon imekuwa mstari wa mbele katika mchakato wa kuwapokea na kuwahudumia wakimbizi na wahamiaji. Baba Mtakatifu Francisko anasema amemtembelea na hatimaye kuzungumza na Ayatollah Ali Sistani, kiongozi mkuu wa kiroho na kisiasa nchini Iraq, ni kiongozi mwenye hekima na busara. Amemwelezea kuhusu nia ya hija yake ya kitume nchini Iraq kuwa ni hujaji wa toba, imani na matumaini; mambo ambayo yamemsukuma kutoka katika undani wake, kwenda kumsalimia. Kwa muda wa miaka kumi, Ayatollah Ali Sistani anapokea viongozi wa kidini tu!

Baba Mtakatifu anakiri kwamba, hija yake ya kitume nchini Iraq imemwezesha tena kukutana na watu mubashara na hivyo kupyaisha maisha na utume wake kama ilivyokuwa kwa Naamani jemedari wa Mfalme wa Shamu aliyeponywa ukoma wake na Nabii Elisha hata yeye amepyaishwa tena kutoka katika undani wa maisha yake. Viongozi wa Kanisa na waamini katika ujumla wao, wajifunze kujisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya Kristo na Kanisa lake bila kupenda sana kupokea “takrima”. Utamaduni wa kukutana na watu katika huduma ni chachu ya wokovu inayowasaidia viongozi wa Kanisa kuadhimisha Fumbo la Ekaristi Takatifu, kuwatangazia na kuwashuhidia watu Neno la Mungu pamoja na kuwaondolea dhambi zao. Baba Mtakatifu anasema aliguswa sana na shuhuda za watu wa Mungu nchini Iraq, watu ambao wamesiginwa na umaskini pamoja na vita, lakini, wako tayari kutubu na kumwongokea Mungu pamoja na kutoa msamaha kwa wale waliowatenda jeuri. Ni muda muafaka kwa waamini kujifunza kusamehe na kusahau, kiini cha Injili ya Kristo Yesu kwa wanafunzi wake.

Baba Mtakatifu anasikitika kusema kwamba, ameguswa sana alipoona Makanisa yaliyokuwa mazuri yamebomolewa na kubaki kuwa magofu, kiasi cha kupigwa bumbuwazi. Huu ni ukatili kupita kiasi unaochangiwa na biashara haramu ya silaha duniani. Silaha hizi ndizo zinazopandikiza mbegu ya chuki, uhasama na uadui kati ya watu. Wanawake wameteswa, wakanyanyaswa na kudhulumiwa utu, heshima na haki zao msingi nchini Iraq, lakini bado wameibuka kidedea. Kuna wanawake na wasichana wanaotumbukizwa kwenye biashara ya binadamu na utumwa mamboleo. Yote haya ni mambo yanayodhalilisha utu wa binadamu.

Papa Iraq

 

05 March 2022, 17:11