Tafuta

2021.12.02  Papa akizungumza na waandishi wa habari akitoka katika ziara ya kitume Ugiriki na Cyprus. 2021.12.02 Papa akizungumza na waandishi wa habari akitoka katika ziara ya kitume Ugiriki na Cyprus. 

Papa Francisko:Mwasiliano mazuri ni kusikiliza na sio upelelezi!

Katika Ujumbe wa Papa wa Siku ya 56 ya Upashanaji Habari Ulimwenguni 2022,anaonesha kukosekana kwa imani nyingi katika taarifa rasmi kumesababisha habari za kugushi na ni vigumu kufanya ulimwengu wa habari kuaminika na uwazi.Anaomba kusikiliza zaidi kuliko kupeleleza,ndiyo mawasiliano mazuri.Wito wake ni kwa ajili ya wahamiaji ili kushinda hukumu dhidi yao na kusikiliza historia zao kwani wao sio idadi na wavamizi hatari mbele yetu ni watu wenye sura ya Mungu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika siku ambayo Mama Kanisa anafanya kumbukumbu ya Mtakatifu Francis wa Sales, Msimamizi wa Vyombo vya habari Katoliki na waandishi wa habari, tarehe 24 Januari 2022, Baba Mtakatifu Francisko ametoa ujumbe wake kwa Siku ya 56 ya Upashanaji Habari Ulimwenguni itakayoadhimishwa na Mama Kanisa, Dominika  tarehe 29 Mei 2022,  sambamba na Sherehe Kupaa kwa Bwana Mbinguni.  Ujumbe   huo kwa mwaka huu unaongozwa na kauli mbiu isemayo “Kusikiliza kwa masikio ya moyo”. Katika Ujumbe huo Papa Francisko anafafanua kwamba katika ujumbe wake, wa mwaka jana tulitafakari juu ya hitaji la “Njoo na uone” ili kuweza kugundua ukweli na kuweza kusimulia kuanzia na uzoefu wa matukio na wa kukutana na watu. Kwa kufuata mwendelezo huo, shauku ya Papa ni kuweka umakini wa neno jingine la 'kusikiliza', ambo ni uamuzi sahihi katika safu ya mawasiliano na hali ya dhati ya mazungumzo.

Tunapoteza uwezo wa kusikiliza

Kwa hakika, Papa amesema amesema tupo tunapoteza uwezo wa kusikiliza aliye mbele yetu, iwe katika hali ya kawaida ya uhusiano wa kila siku, na hata katika mijadala kuhusu mambo muhimu ya kuishi kiraia. Wakati huo huo kusikiliza ndiyo unachukua maendeleo mapya yaliyo muhimu katika kuishi kimawasiliano na habari zinzaotelwa kwa njia nyingi kama vile podcast, chat za audio katika kuthibitisha kwamba kusikiliza bado kubaki kuwa muhimu katika mawasiliano ya binadamu. Kwa upande wa mtaalaam, daktari aliyezoea kutibu majeraha ya roho, aliombwa kujua ni mahitaji gani makubwa zaidi ya lazima ya kuwa binadamu.  Yeye alijibu: “Shauku isiyo na kikomo ya kusikilizwa”. Papa ameongeza kwamba ambayo mara nyingi hubakia mafichoni, lakini ambayo inampatia   mtu yeyote changamoto anayeitwa kuwa mwalimu au mtunzi, au ambaye kwa hali yoyote ana jukumu la kuwasiliana kama vile wazazi na walimu, wachungaji na wahudumu wa kichungaji, wafanyakazi wa mawasiliano  na wale wote wanaotoa huduma ya kijamii au kisiasa.

Kusikiliza kwa masikio ya moyo

Baba Mtakatifu Francisko anasema, kutoka katika sura za kibiblia, tunajifunza kwamba kusikiliza haina maana tu ya mtazamo wa kusikia, lakini ni muhimu kufungamanisha   na uhusiano wa mazungumzo kati ya Mungu na ubinadamu. “Shema’ Israel, yaani Sikiliza Israeli” (Kumb 6,4), ambayo ipo katika amri ya kwanza kwenye Torah iliendelea kupendekezwa katika Biblia, hadi kufikia Mtakatifu Paulo kuthibitisha kwamba: “imani inatokana na kusikiliza” (Rm 10,17). Anayeanza kiukweli ni Mungu ambaye anazungumza nasi na sisi, tunajibu kwa kumsikiliza; na hata hivyo kusikiliza Papa anabainisha kimsingi ni kutokana na neema, kama inavyojitokeza kwa kitoto kichanga ambacho hujibu mtazamo na sauti ya mama ana baba. Kati ya milango mitano ya fahamu, yenye muafaka na Mungu utafikiri ni ile ya kupitia masikio, labda kwa sababu haina uvamizi, ina busara zaidi kuliko kuona na kwa hivyo inamwacha mwanadamu huru. Kusikiliza kunaelekeza mtindo wa kinyenyekevu wa Mungu. Ni tendo ambalo linamruhusu Mungu kujionesha kama Yule ambaye kwa kuzungumza, anaumba mtu kwa mfano wake, na kwa kusikiliza anamtambua mpinzani wake. Mungu anapenda mtu na kwa maana hiyo anamwelekeza Neno, na wakati huo huo anamtegea sikio ili kumsikiliza.

Bwana anamwita mtu moja kwa moja katika mshikamano wa upendo

Kinyume chake Mtu anatafuta kukimbia uhusiano, kumgeuzia kisogo na “kufunga masikio” ili hasiweze kumsikiliza. Kukataa kusikiliza, mara nyingi kunaishia kuwa uchokozi kwa mwingine, kama ilivyojitokeza kwa wasikilizaji wa shemasi Mtakatifu Stefano ambao kwa kuziba masikio, walipiga mawe hadi kufa. ( Mdo 7,57). Kwa upande mwingine, yupo Mungu ambaye daima anajionesha  kuwasilisha habari bure, na kwa upande mwingine mtu ambaye anaombwa kuwa na maelewano na kujiweka katika usikivu. Bwana anamwita mtu  moja kwa moja katika mshikamano wa upendo ili aweze kugeuka kabisa kile ambacho yeye ni sura na mfano wa Mungu katika uwezo wake wa kusikiliza, kupokea na kutoa nafasi ya mwingine. Kusikiliza, zaidi ya yote, ni mwelekeo wa upendo. Kwa maana hiyo Yesu anawaita mitume wake na kuhakikishia juu ya ubora wao wa usikivu. Anawambia “Jiangalieni basi jinsi msikiavyo” (Lk 8,18). Kwa kufanya hivyo tu, kuwa na umakini kwa wale tunaowasikiliza, ni kitu gani tunasikiliza na jinsi gani tunawasikiliza, tunaweza kuunda sanaa ya kuwasiliana, ambayo kimsingi kitovu sio tu kinadharia au kiufundi, lakini ni uwezo wa moyo ambao unakuwa na uwezo wa ukaribu ( EG 171).

Msiwe na moyo katika masikio bali masikio ya moyo

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake anabainisha kwamba sisi sote tuna masikio, lakini mara nyingi hata mwenye kusikia vizuri kabisa hawezi kusikiliza mwingine. Kuna uziwi kwa hakika wa ndani, na mbaya zaidi wa kimwili. Usikivu kwa hakika hautazami mlango wa fahamu ya kusikia tu, lakini hata kwa ubinadamu wote. Makao ya kweli ya kusikiliza ni moyo. Mfalme Solomoni lichaya kuwa kijana mdogo alijionesha kuwa na  hekima kwa sababu aliomba Bwana amwezeshe kuwa na “moyo adili ambao unasikiliza (1Wafalme 3,9). Na Mtakatifu Agostino alikuwa anawaalika kusikiliza kwa moyo (corde audire), kupokea maneno si kwa kijuu juu katika masikio yao, bali kiroho katika moyo kwamba “Msiwe na moyo katika masikio bali masikio ya moyo”. Na Mtakatifu Francis wa Assisi alikuwa akiwashauri Ndugu Wadogo “kusikiliza kwa masikio ya moyo”. Kwa maana hiyo usikivu wa kwanza wa kugundua unapokuwa unatafuta mawasiliano ya kweli ni ule kujisikiliza, mahitaji binafsi ya kweli zaidi, yale yaliyoandikwa ndani ya kila mtu.  Haiwezekani kutoanzia katika kusikiliza kile ambacho kinatufanya wa kipekee katika kazi ya uumbaji na ambacho ni shauku ya kuwa na uhusiano na mmoja na mwingine. Hatukuumbwa kuishi kama atomi, lakini pamoja, Papa anasisitza.

Kusikiliza ni hali ya kuwa na mawasiliano mema

Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba kuna matumizi ya kusikia ambayo sio ya ukweli wa usikivu, bali  kinyume chake ni kupeleleza. Kwa hakika, ni kishawishi ambacho daima kipo na ambacho leo hii katika kipindi cha mitandao ya kijamii, utafikiri ndiyo kinashamiri. Ni kusikiliza na kupeleleza, kuwanyonya wengine kwa maslahi binafasi. Kinyume chake kile ambacho kinafafanua mawasiliano mema na ya kibanadamu kabisa ni usikivu kwa yule ambaye yupo mbele, uso kwa uso, usikivu wa mwingine ambaye anatukaribia kwa ufunguzi wa kweli, imani na uaminifu. Ukosefu wa usikivu ambao unafanywauzoefu mara nyingi katika maisha ya kila siku inajionesha kwa bahati mbaya hata katika maisha ya umma, mahali ambapo, badala ya kusikilizana, mara nyingi wanazungumzia nyuma. Hii ni dalili ya ukweli kwamba maafikiano yanatafutwa zaidi ya ukweli na wema; zaidi ya kusikiliza, tunakuwa makini kwa hadhira. Mawasiliano mazuri, kwa upande mwingine, hayajaribu kuvutia umma na utani, kwa lengo la kumdhihaki mwingine, badala yake ni umakini na sababu za mwingine na yanajaribu kufahamu utata wa ukweli. Inasikitisha wakati, hata katika Kanisa, miunganisho ya kiitikadi inapoundwa, usikivu hupotea na kutoa nafasi kwa tofauti zisizo zaa na tasa.

Mazungumzo yanahitaji mimi na wewe

Baba Mtakatifu Fracisko amesema katika hali halisi kwenye mazungumzo mengi, sisi hatuwasiliani kiukweli. Tunakuwa tunasubiri mwingine amalize kuzungumza ili kumwelezea mtazamo wetu. Katika hali hiyo kama asemavyo mfalsafa Abrahamu Kaplan,  mazungumzo ni mazungumzo ya mtu anayezungumza peke yake akiwa na sauti mbili (monologue- duologue,)sehemu mbili. Katika mazungumzo ya kweli yanahitaji  mimi na wewe tuko pamoja katika kuelekeza mmoja na mwingine. Kusikiliza kwa maana hiyo ndiyo hitaji la kwanza katika mazungumzo na kuwasiliana vema.  Huwezi kuwasiliana ikiwa hakuna kusikiliza kwanza na hauwezi kuwa mwanzo wa habari bila kuwa na uwezo wa kusikiliza. Ili kuweza kutoa habari thabiti, zilizo na msimamo na kamili ni lazima kusikiliza kwa muda mrefu. Ili kuweza kusimulia tukio au kuelezea hali halisi katika kutoa habari, lazima kwanza kutambua kusikiliza, na kuwa tayari kubadilisha wazo, kubadilisha hata mawazo ya kwanza. Ikiwa mtu ataacha (monologue) kuzungumza peke yake, kiukweli, anaweza kufikia upatanisho wa sauti ambazo ni dhamana ya mawasiliano ya kweli. Kusikiliza vyanzo vingi, na usiishie kwenye habari za kwanza tu kama wataalam wa shughuli hiyo wanavyofundisha, kwamba huhakikishe na kuwa na  umakini katika habari tunayosambaza. Kusikiliza sauti zaidi, kusikiliza kila mmoja, hata katika Kanisa, kati ya kaka na dada, huturuhusu kutumia sanaa ya utambuzi, ambayo kila wakati inaonekana kama uwezo wa kujielekeza katika umoja wa sauti.

Mshangao unaturuhusu kufahamu

Baba Mtakatifu Francisko, anauliza swali:  Je ni kwa nini kukabiliana na ugumu wa kusikiliza? Mwanadipolmasia mmoja wa Vatican, Kardinali Agostino Kasaroli, alikuwa anazungumza kuhusu: “ushihidi wa uvumilivu kuwa ni wa lazima ili kusikiliza na kufanya usikilizwe katika kufanya mazungumzo na waingiliaji wagumu zaidi, na hatimaye huweze kupata haki nzuri uwezekanavyo kwa kiasi kikubwa katika vikwazo wa uhuru. Lakini hata katika hali zilizo ngumu kidogo, kusikiliza kunahitaji daima fadhila ya uvumilivu, pamoja na uwezo wa kuacha ushangazwe na ukweli, labda wa chembe tu moja ya ukweli  kutoka kwa mtu ambaye tuko tunamsikiliza. Ni mshangao tu ambao unaturuhusu kufahamu. Papa Francisko amefikiria utukutu wa mtoto ambaye anatazama dunia kwa kuikodolea  macho sana. Kusikiliza kwa namna hiyo ya roho, ya mshangao wa mtoto katika utambuzi wa mtu mzima, ni utajiri mkubwa daima, kwa sababu kutakuwa daima na kitu, hata kile kidogo ambacho ninachukuliwa mwingine na kuleta mafao  ya maisha yangu.  

Ukosefu wa imani ya mawasiliano umesababisha hata habari za ugushi

Uwezo wa kisikiliza jamii ni wenye thamani katika kipindi kilichojeruhiwa kwa muda mrefu na janga. Ukosefu wa imani nyingi, uliokusanywa kabla kuelekea mawasiliano na taarifa rasmi kumesababisha habari za kugushi ambazo ni vigumu kufanya ulimwengu wa habari kuaminika na uwazi, Papa anabainisha. Lazima kutega sikio na kisikiliza kwa kina hasa matatizo ya kijamii yaliongezeka kwa kudorora au kukoma kwa shughuli nyingi za kiuchumi. Hata hali halisi ya uhamiaji wa kulazimisha, Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza ni matatizo magumu na hakuna aliye na orodha iliyo tayari ya kuweza kusuluhisha. Papa amerudia kutoa wito wake  kwamba ili kuweza kushinda hukumu na chuki dhidi ya uhamiaji na kulazimisha ugumu wa mioyo, lazima kujaribu kusikiliza historia zao. Kuwapa jina na historia kwa kila mmoja wao. Anawapongeza waandishi wa habari wanaofanya hivyo tayari. Na wengine wengi wanataka kufanya ikiwa inawezekana. Papa ameomba kuwatia moyo. Kusikiliza historia hizo. Kila mmoja atakuwa huru wa kusasisha  sera za uhamiaji ambao utakuwa unafaa katika nchi yake. Lakini mbele ya macho yetu, waamiaji sio idadi na wala sio wavamizi hatari bali ni sura na historia za watu kweli, wenye mitazamo, matarajio, na mateso ya wanaume na wanawake wa kusikilizwa!

Kusikiliza katika Kanisa:kutoa muda kidogo kusikiliza ni ishara ya upendo

Baba Mtakatifu Francisko anasisitiza kwamba hata katika Kanisa kuna hatari sana ya kusikiliza na kusikilizana. Ni zawadi kubwa sana na ya kuleta mafao na ambayo tunaweza kuwapatia mmoja na mwingine. Kama wakristo Papa, anashauri wasisahau kuwa, huduma ya kusikiliza ilikabidhiwa na Yule ambaye ni msikilizaji wa kwanza kabisa ambaye anatenda na sisi tunapaswa kushiriki.  “Ikiwa tunataka kuzungumza neno lake, sisi tunapaswa kusikiliza kwa njia ya masikio ya Mungu”.  Mtaalimungu wa Kiprotestanti, Dietrich Bonhoefferalikuwa anatukumbusha kuwa huduma ya kwanza ambayo lazima ifanyike kwa wengine katika kuungana, inahitaji kutoa umakini katika kusikiliza. Hasiye jua kusikiliza ndugu, mapema au baadaye hawezi kabisa kuwa na uwezo wa kusikiliza hata kidogo Mungu. Katika matendo ya kichungaji, kazi muhimu zaidi ni utume wa sikio. Kusikiliza kwanza kabla ya kuzungumza, kama anavyoshauri Yakobo; “Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema” (Yk 1,19”. Papa anashauri kutoa muda wa bure kidogo ili kusikiliza mtu ndiyo ishara ya kwanza ya upendo.

Kila sauti ya kwaya huimba huku ikisikiliza sauti nyingine

Baba Mtakatifu amekumbusha jinsi ambavyo Mchakato wa Sinodi ndio umeanza. “Tuombe kwamba iwe fursa nzuri ya kusikilizana. Ushiriki, kiukweli, sio matokeo ya mikakati na mipango, lakini umejengwa juu ya kusikilizana kati ya kaka na dada. Kama ilivyo kwa kwaya, umoja hauhitaji usawa, japokuwa umoja, lakini unahitaji wingi na aina za sauti, (polyphony). Wakati huo huo, kila sauti ya kwaya huimba huku ikisikiliza sauti nyingine na kuhusiana na upatanisho wa jumla”. Papa ameongeza kwa kuhitimisha ujumbe huo: Maelewano haya yanatungwa na mtunzi, lakini utambuzi wake unategemea maelewano ya sauti (symphony) ya wote na sauti moja. Kwa utambuzi wa ushiriki katika umoja ambao unawaongoza na kufungamanisha, tunaweza kweli kugundua Kanisa moja la maendeleo, ambalo kila mmoja ana uwezo wa kuimba sauti yake mwenyewe, kwa kuwakaribisha wale wengine kama zawadi, kudhihirisha maelewano kwa njia ya Roho Mtakatifu anayewaungnisha”.

UJUMBE WA PAPA WA SIKU YA MAWASILIANO
24 January 2022, 16:25