Papa Francisko:Jumuiya ya kitawa itambue kusaidiana mmoja na mwingine
Na Sr Angela Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko amekutana na kuzungumza na washiriki wa Mkutano Mkuu wa 164 wa Shirika la Mapadre wa Theatine na kuwaeleza jinsi walivyopitia mchakato wa safari ndefu kufikia miaka hiyo waliyopitia kwa upendo wa Mungu. Kwa sababu hiyo ni kutoa shukrani kubwa mno. Papa Francisko amemshukuru Mkuu wa shirika kwa maneno yake na kumtakia maendeleo mema ya huduma kwa kile ambacho amethibitisha katika hotuba yake. Mada waliyochagua kuongoza mkutano wao kwa siku hizi, inaibua kwa mara nyingine tena kauli ya utume wao isemayo: “Watheatine kwa ajili ya Utume”, kwa maana hiyo amewapongeza kwa uchaguzi huo wakiwa na mwelekeo msingi wa Kanisa ambapo Kristo mfufuka aliendelea kutoka nje kwa ajili ya uinjilishaji ambao unawagusa kila mkristo na kila jumuiya (GE 20). Kwa upande wao, karama hiyo inaunganishwa na ile ya Mtakatifu Gaetano Thiene na waanzilishi wenzake wa shirika ambao amesema ni “Ndugu Mitume wa Kikuhani” ambao wamesimika mizizi yao kwa kina katika maisha ya tasaufi na upendo wa dhati na wenye kuhitajika.
Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake amesema katika maisha ya Mtakatifu Gaetano, kama yale ya watakatifu wengi wa kike na kiume, yanashangaza kuona katika kipindi kingine kunakuwapo na ubora zaidi ambao kwa neno la Kibiblia. unaitwa “wito katika wito au uongofu wa pili. Huu ni mchakato wa maisha ambayo tayari ni mema na yanayosifiwa na maisha matakatifu yaliyo mkamili zaidi na ambayo yanatokana na Roho Mtakatifu. Ubora huo ni ule naofanya kukua si, tu katika maisha mwanaume au mwanamke, lakini hata maisha ya Kanisa. Ni yale ambayo kwa maana nyingine mabadiliko ya kutakaswa na kufanya huingie uzuri wa kiinjili. Ushuhuda huo na Injili hai unawezekana na lazima kufanya uendelee mbele katika mchakato binafsi na kijumuiya kwa kutambua vema kwamba haiwezekani Mkristo kufikia utume wake katika dunia hii bila kuutambua kuwa ni safari ya utakatifu (Esort. ap. Gaudete et exsultate,19). Hata Mtakatifu Gaetano Thiene alionesha kuwa kila mtakatifu ni utume. Kila mtakatifu kwa maana ya mwanaume na mwanauke ni mpango wa Baba kwa ajili ya kuangaza na kufanyika mwili katika nyakati zilizotabiriwa za historia na mantiki ya Injili.
Papa Francisko amesema kuwa “kile kinachoombwa kwetu sio kwa kuiga, kwa maana halisi, ambaye sisi sote tunapaswa kumwiga na ambaye ni Yesu Kristo tu, lakini kwa kufikiria kutoka kwa mtakatifu huyo wa kike na kiume mbinu ya nguvu za kiroho ambazo aliweza kuishi Injili, kwa kujaribu kuzitafsiri katika mazingira yetu ya sasa”. Na hilo pia ndilo lililopendekezwa kwa lengo kuu la Mkutano wao. Papa amenukuu: “Ili kufanikisha karama ya Theatine, kujibu changamoto za sasa kuanzia na utambulisho wetu”. Na utambulisho unahusu lengo maalum, Papa ameongeza. Kutokana na mantiki hiyo amesema hawezi kuwafundisha chochote kwani wao wanajua vizuri. Ila amependa kusisitiza juu ya mantiki muhimu ya ushuhuda wa Mtakatifu Gaetano na kwamba mabadiliko lazima yaanzie na Yeye alye mwanzilishi. Alipokuwa Roma kufanya kazi katika ofisi aliweza kutambua ufungufu wa kiroho na kimaadili ambao kwa bahati mbaya ulikuwa umeenea wakati ule. Na alifanya nini? Wakati akiendelea na kazi yake ofisini alikuwa anakwenda kwenye kituo kimoja cha “Divno Amore” , kuhamasisha sala na mafunzo ya kiroho na baadaye akaenda hospitali kuhudumia wagonjwa”. Papa amesema “Hiyo ndiyo njia ya kuanzia binafsi na kuishi kwa kina na ukweli wa Injili”. Watakatifu wote wanaeleza hivyo. Ni wao tu walimu wa kweli wa Kanisa. Anayeongoza ni roho Mtakatifu , anayeunda na kuunda kwa upya Kanisa na anafanya hivyo kwa njia ya Neno la Mungu na kwa njia ya watakatifu, ambao wanajikita kwenye matendo ya Neno katika maisha yao.
Lengo la pili maalum ni umoja. Kwa upande huo Papa Francisko kwa kutazama Mtakatifu Gaetano wanapenda kusema ni Roho Mtakatifu ambaye hasukumi ili kufanya peke yake mchakato binafsi. Hapana. Yeye alimweka kuunda jumuiya ya Ndugu wa kawaida ili waishi Injili kwa mujibu wa mtindo wa maisha ya Mitume. Katika Wosia wa Gaudete et exsultate, ambayo Papa amewashauri sana kuisoma kwa mara nyingine na itawasaidia, kwani yeye anafanya hivyo kwa sababu anaweza kusahau kile ambacho aliandika kwa wengine, amebainisha alivyokumbusha baadhi ya Jumuiya takatifu ambazo waliishi kishujaa Injili (141), Katika watakatifu hao, Papa amebainishwa wanaweza kuongeza hata waanzilishi wao, lakini kwa kawaida familia na katika jumuiya za kidini na maisha ya kikristo zimeundwa kwa ishara nyingi za kila siku. Jumuiya ambayo inatunza walio wadogo kwa namna ya pekee kwa upendo, mahali ambapo wao wanatunza mmoja na mwingine na kuunda nafasi iliyo wazi ya uinjilishaji ni mahali pa uwezo wa Mfufuka ambaye anatakatifuza kwa mjibu wa mpango wa Baba.(145).
Papa Francisko akiendelea na hotuba yake amesema kuna sentesi moja ambayo ninapenda kuisisitiza. Wajumbe ambao wanatunza mmoja na mwengine. “Ndugu mdudu mkubwa sana aliyeko katika Mashirika la kitawa na jumuiya za kitawa ni pale ambapo ndugu wanaposhindwa kusaidia mmoja na mwingine na zaidi wanapoanza masengenyo. Tafadhari, fukuzeni mbali kila aina na masengenyo. Muwe watu waliowekwa wakfu”. Na hatimaye lengo la tatu ambalo Papa amependekeza kwao hasa ni lile la utume ambalo ni kujua kung’amua ishara za nyakati ili kutangaza na kuishi Ufalme wa Mungu katikati ya waamini. Kwa msingi wa karama iliyounda na shirika, utume wao sio ule wa watu wa mataifa, kwani Mtakatifu Gaetano aliinjilisha Roma ,Venezia na Na Napoli na alifanya hasa kwa njia ya ushuhuda wa maisha na kazi za huruma, kwa kujikita katika protokali kuu tuliyo achiwa na Yesu inayohusu Hukumu ya mwisho kutoka Injili ya Matayo( 25, 31-46). Yeye na wenzake walihudumia na kufanya kukua Kanisa la “ Ospitali kambini ambalo leo hii Papa amesisitiza kuna hakja kuwana ya kuwa nalo.
Papa Francisko amewatia moyo wa kuendelea mbele katika nyayo zao, kwa upole wa Roho, bila kuwa na ugumu, ambapo ameweka mkazo mkuu wa kuwa makini na ugumu kwa sababu ugumu ni upotovu unaokuja kwa usahihi kutokana na kujisikia ukuhani hivyo ni jambo jingine baya na chini ya ugumu wowote ule kuna uozo kila wakati bila mipango migumu, lakini thabiti katika mambo muhimu, ambayo ni sala, kuabudu, maisha ya kijumuiya, umaskini na huduma kwa maskini. Yote hayo yafanyike kwa moyo wa kitume na wasiwasi mwema wa kiinjili katika kutafuta awali ya yote Ufalme wa Mungu. Papa Francisko amesema kama wao wajuavyo kati ya mji ulionjilishwa na Mtakatifu Gaetano kuna hata Buenos Aires: Siku Kuu ya Myakatifu Cayetano, tarehe 7 Agosti ina ushiriki mkuu wa ibada ya watu. Watu wengi wanamheshimu na kusali kama Msimamizi wa kpata mkate na ajira. Kwa njia ya maombezi yake na ile ya Mama Maria amewakibidhi katika safari yao ya utume. Na kuhitimisha akiwaomba wasisahau kusali kwa ajili yake.