Tafuta

Mkumbatio mpya kati ya Papa na Edith Bruck katika kumbu kumbu ya maangamizi dhidi ya Wayahudi ifanyikayo kila tarehe 27 Januari ya kila mwaka. Mkumbatio mpya kati ya Papa na Edith Bruck katika kumbu kumbu ya maangamizi dhidi ya Wayahudi ifanyikayo kila tarehe 27 Januari ya kila mwaka. 

Mkumbatio mpya kati ya Papa na Edith Bruck:kurithisha kumbu kumbu kwa vijana

Katika siku ya kumbukumbu za mauaji ya kimbari dhidi ya Wayahudi ifinyakayo kila tarehe 27 Januari kila mwaka,Papa Francisko kwa upya amekutana katika Nyumba ya Mtakatifu Marta,Vatican na mwandishi wa vitabu wa Hungaria aliyenusurika katika kambi la Auschwitz.Saa moja ya mazungumzo kati ya kumbukizi na kubadilishana zawadi kwa uwepo wa msaidizi Olga na Mkurugenzi wa Gazeti la Osservatore Romano,Andrea Monda.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Upendo ambao sasa unawafungamanisha pamoja, tangu wakati ule wa ziara yake ya kwanza mnamo tarehe 20 Februari 2021, umeonekana katika zawadi ambayo Papa alimpatia na kwa maneno ambayo yalisindikiza zawadi. Skafu ya sufu, aliyomwekea juu ya mabega yake akisema: “Hii ni kwa ajili ya joto, kwa sababu sasa ni baridi”. Edith Bruck, mwenye umri wa miaka 90, Ni mama Mwitaliano lakini mwenye asili wa Hungaria, alinusurika katika mateso ya moja ya kambi sita za mateso, na sasa ni shuhuda  wa thamani ya wakati wetu na mwandishi maarufu wa kimataifa, aliyejaribu tangu mwanzo kuzuia machozi yake na badala yake aliyatoa mbele ya zawadi ya Papa kwa ukarimu wake aliomwonesha. Aliguswa sana na huruma ya mwanaume ambaye hakumficha kamwe kwamba alivutiwa naye na ambaye, kama asemavyo mara nyingi, alianzisha urafiki ulioanzia katika barua na simu.

Mkutano wa Papa na Edith Bruck
Mkutano wa Papa na Edith Bruck

Upole huo ulionekana katika mkumbatio ambao Papa Francisko alimkaribisha mwanamke huyo kwenye Nyumba ya Mtakatifu Marta,  Vatican anapoisha katika siku isiyo sahulika ambapo waathirika wa Shoah wamefanya kumbu kumbu ya maangamizi makubwa yaliyotokea kwenye kambi ya mauaji ya kimbari ya Auschwitz- Birkenau. Jumatato tarehe 27 Januari, walipata kuwa na mkutano uliodumu kama saa moja mbele ya Olga, msaidizi wa mwandishi wa Kiukreine na Andrea Monda, mkurugenzi wa Gazeti la Osservatore Romano, ambaye ameripoti juu ya maelezo hayo yaliyotukia katika mkutano huo. Hotuba nyingi, hadithi, kumbukumbu zilikumbukwa, lakini juu ya yot ilikuwa mada ya kumbukumbu na umuhimu wa kuipitisha kwa kizazi hiki kipya cha vijana, kufungwa, historia na kuteswa na vituko vya  ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Wayahudi ambazo zinaonekana kuibuka kwa mara nyingine tena.

Wote wawili walisisitiza thamani isyo na mfano ya kupeleka kumbukumbu za wakati uliopita kwa wadogo zaidi hata katika vipengele vyake vyenye uchungu zaidi, ili suala hili lisirudie tena kwa mujibu wa taariza za  Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican. “Wanaume hawakujifunza kutokana na makosa yao. Hawakujifunza kutokaAuschwitz, kama walivyojifunza kutoka Vietnam", Alisema Bruck  katika mahojiano siku ya Alhamisi akihojiwa na Vatican News. Mwandishi huyo, mshindi wa mwisho wa Tuzo ya Strega, alimwambia Papa Francisko kila kitu anachofanya. Sio tu ushiriki katika tukio muhimu, mamia ya mahojiano yaliyotolewa katika siku za hivi karibuni kwa ajili ya siku hiyo, lakini zaidi ya yote kuwa 'mhujaji' katika shule za Roma ili kuzungumza na watoto na kuwaambia kile alichokiona, kile alichopoteza, na kwamba, aligundua mengi sana, kazi ambayo ni msingi kwa jamii lakini pia kwake yeye mwenyewe. Edith Bruck alimwambia  Papa "Ni nzuri kwangu" . Na Papa Francisko kwa hakika alijibu kwa huruma kwamba aliona kuwa kazi inamfanya kuwa kijana.

Mkutano wa Papa na Edith Bruck
Mkutano wa Papa na Edith Bruck

Aliyenusurika ametiwa moyo zaidi ya yote kwa kuona matokeo ya ajab ambayo maneno yake yanawagusa vijana. “Ningependa kuwaambia wazazi kwamba watoto wao ni bora kuliko wanavyofikiria,” Bruck alisema, kama ilivyoripotiwa na Monda,  Mkurugenzi wa Gazeti la Osservatore Romano. Kwa hivyo Papa alisisitiza, kama anavysema mara nyingi katika hotuba zake, kwamba ni muhimu mawasiliano ya kweli yaanzishwe tena kati ya wazazi, babu, bibi wajukuu, kati ya wazee na vizazi vipya. Maongezi yaliendelea kwa muda mrefu. Alisimama tu wakati wa kupena zawadi, akiwa na hisia kali za kumpatia  Papa mkate uliosukwa na ambao uliokwa nyumbani. Ni ile “mkate uliopotea”, kwa  jina la riwaya yake maarufu, ambayo mama yake alioka kabla tu ya kuchukuliwa na Wanazi, ambao leo uliwasilishwa kwa Papa kama ishara ya “mkate uliopatikana". Ishara, pengine, ya utulivu uliopatikana licha ya kumbukumbu ya wazi ya uovu. Kila mtu aliyekuwepo alionja kipande cha mkate huo.

Mkutano wa Papa na Edith Bruck
Mkutano wa Papa na Edith Bruck

Mbali na skafu, ambayo alimpatia rafiki yake, Francisko Papa pia alimzawadia medali iliyotengenezewa huko Yerusalemu, ambayo ilimvutia sana Bruck.  Na Yeye pia alimwachia vitabu viwili Papa chenye jina: “Barua kwa mama yangu, katika toleo jipya la Nave di Theseo, na kitabu cha mashairi cha Miklós Radnóti, mshairi wa Hungaria ambaye kazi yake nzuri kama alivyosema Papa Francisko mwenyewe  huko Budapest kuwa  alivunjwa na chuki iliyopofushwa ya wale ambao, kwa sababu tu alikuwa wa asili ya Kiyahudi, walimzuia kwanza kufundisha na kisha kumuiba kutoka katika familia yake. Mashairi yalitafsiriwa na kuhaririwa na Bruck mwenyewe.

Papa alimtembelea Bruck mwaka jana nyumbani kwake

Kumbatio lingine liliashiria mkutano huo, pamoja na machozi ya mwanamke huyo na pongezi za Papa kwa akili na ufahamu wake. Pia kulikuwa na mazungumzo mafupi ya maneno na msaidizi, kutoka Ukraine, ambaye alimwomba Papa maombi kwa ajili ya ardhi yake yenye mzozo kwa sasa. Naye Papa Fransisko alimwahakikishia kuwa atasali kwa ajili yake. Papa Francisko alikutana kwa mara ya kwanza na Edith Bruck mwaka jana. Alikuwa amemtembelea katika nyumba yake katikati ya jiji la Roma, mara baada ya kusoma mahojiano yenye kugusa moyo katika Gazeti la Osservatore Romano ambamo mwanamke huyo alisimulia kwa kina, lile giza ambalo yeye na familia yake walifanya uzoefu wakati wa mnyanyaso wa Wanazi.

Ukurasa mweusi wa historia ya mwanadamu

"Nimekuja hapa kukushukuru kwa ushuhuda wako na kutoa heshima kwa watu waliouawa shahidi kwa kutokana na uwazimu wa umati wa Wanazi na ninarudia kwa dhati maneno niliyozungumza kutoka moyoni mwangu kwa Yad Vashem na ambayo narudia mbele ya kila mtu kama wewe, aliyeteseka sana kwa sababu hiyo ; msamaha wa Bwana katika jina la ubinadamu" ”, Papa Francisko alisema maneno hayo katika tukio hilo. Maneno ambayo Papa hakuacha kamwe kurudia mbele ya umati uliokuwa katika Ukumbi wa Papa Paulo VI,  mara baada ya Katekesi yake Jumatano  26 Januari akifafanua tukio hili kama  ukurasa mweusi katika historia ya mwanadamu uliowekwa alama na ukatili usioelezeka!

28 January 2022, 11:55