Tafuta

Papa Francisko na wajumbe wa Mahakama ya Kitume wakati w uzinduzi Mwaka wa Mahakama ya Rufaa ya Kitume 2022. Papa Francisko na wajumbe wa Mahakama ya Kitume wakati w uzinduzi Mwaka wa Mahakama ya Rufaa ya Kitume 2022. 

Hotuba ya Papa kwa uzinduzi wa mwaka wa Mahakama ya Kitume 2022

Papa Francisko katika hotuba yake kwenye uzinduzi Mwaka wa wa Mahakama ya Rufaa ya Kitume amesitizia juu ya mchakato wa Sinodi ulioanza hivi karibuni wa Kanisa ma kuwa mchakato huo pia una mantiki ya mahakama na utume wa huduma ya familia hasa wale waliojeruhiwa na wenye kuhitaji manukato ya huruma.Katika mwaka uliowekwa kwa ajili ya familia ni fursa ya kijikita kutafakari sinodi katika michakato ya kubatilisha ndoa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko alhamisi tarehe 27 Januari 2022 amekutana wahamasishaji wa Haki, wachunguzi, maafisa, wanasheria na wahudumu wa Mahakama, na katika kuzindua Mwaka wa 92 wa Mahakama ya Rufaa ya Kitume. Papa Francisko amesema mchakato wa kisinodi ambao umeanza, ni pamoja na mkutano huo kwa sababu nahusu hata mantiki ya kimahakama na utume wao katika huduma ya familia, hasa ya majeraha na mahitaji ya mafuta ya huruma. Kazi ya kisinodi kwa hakika hata kama fulani  sio  kama mchakato huo lakini inajiweka katika mzungumzo na shughuli za kimahakama, hatimaye kuweza kutoa mufaka wa kufikiri kwa upya umuhimu wa uzoefu wa mchakato wa Kanoni ya sheria kwa ajili ya maisha ya waamini ambao wamepata uzoefu wa kushindwa katika ndoa zao na wakati huo huo kwa ajili ya kuleta umoja na uhusiano ndani ya jumuiya ya Kikanisa.

Papa akitazama mchakato huo amesema wajiulize nini maana ya kutoa huduma katika haki inayohitajika katika roho ya kisinodi. Awali ya yote, Sinodi ina maana ya kutembea pamoja. Kushinda maoni potofu ya sababu za ndoa, kana kwamba masilahi ya kibinafsi yamethibitishwa ndani yao na kugundua kuwa washiriki wote katika mchakato huo wanaitwa kupitia katika lengo moja, lile la kutafuta ukweli kuhusu muungano wa dhati kati ya mwanaume na mwanamke, ili kufikia mwisho wa kuishi au ndoa ya kweli kati yao. Kutembea pamoja kuelekea mwisho wa pamoja huko sio mpya katika uelewa wa Kanisa katika  michakato.

Ufunguzi wa mwaka wa Mahakama ya kitume 2022
Ufunguzi wa mwaka wa Mahakama ya kitume 2022

Papa amenukuu hotuba ya Mtumishi wa Mungu Papa  Pio XII, kulingana kwamba  “lengo la umoja, ambalo linapaswa litoe muundo wa kazi na kwa kushirikiana na wote ambao wanashiriki katika mchakato ya kesi za ndoa kwenye mahakama ya kikanisa kwa kila ngazi hasa lazima ziongozwe na kuwafikia katika umoja sawa wa makubaliano na wa matendo (Rota Romana, 2 Oktoba 1944). Katika mtazamo huo kazi ya kila mshiriki wa mchakato wa sheria ni katika kutafiti wa ukweli, pamoja na kuhifadhi kila mmoja umainifu wa nafasi yake. Huo ndiyo ukweli ikiwa unapendwa unageuka kuwa ukombozi. Tayari katika hatua ya mahakama, waamini wanapojikuta na matatizo na wanatafuta msaada wa kichungaji, na haiwezekani kukosa nguvu kwa ajili ya kugundua ukweli binafsi wa muungano, ambao muhimu kuweza kufikia uponyaji wa majaraha. Katika hatua hiyo inaelewesha jinsi gani ilivyo muhimu juhudi ya kusaidia msamaha na upatanisho kati ya wenzi wa ndoa.

Ufunguzi wa mwaka wa Mahakama ya kitume 2022
Ufunguzi wa mwaka wa Mahakama ya kitume 2022

Baba Mtakatifu Francisko amesema katika kusubiri kubatilishwa kwa ndoa ni lazima kufanya watafakari waamini juu ya sababu ambazo zinafanya kuwa na uthibitisho wa kubatilisha, ndoa hiyo , kwa kusaidia kuwa na tabia ya kupokea hukumu ya mwisho, hata kama haiendani na makubaliano. Ni kwa njia hiyo tu mchakato wa kubatilisha ndoa unakuwa kielelezao cha kweli cha kusindikiza kichungaji waamini katika mgogoro wao wa ndoa na kwa maana ya kijiweka katika usikivu wa Roho Mtakatifu ambaye anazungumza katika historia ya dhati kwa watu. Baba Mtakatifu akianza kufafanua bila kusoma amesema: Hapa nasimama na kuomba radhi kwa kusema kuwa ni  hatari kubwa sana iliyopo. “Wakati inaposhindikana hata kwa wanasheria wanaweza kufanya uharibifu mbaya sana. Mwezi mmoja uliopita askofu mmoja alikuja kulalamika kuhusu tatizo moja la Padre mmoja. Tatizo kubwa. Tatizo halikuwa la ndoa; lilikuwa suala zito la nidhamu ambalo lilistahili kwenda mahakamani. Jaji wa mahakama ya kitaifa, alimwita askofu na kumwambia: “Nimepokea hili. Nitafanya kile unachoniambia. Ukiniambia nimhukumu, ninamhukumu; ukiniambia nimuondolee, ninamwachia”.  Papa ameongeza kusema “ii inaweza kutokea, ikiwa hakuna umoja huu katika michakato hata kwa michakato  unayopingana, lakini kwenda pamoja, kwa sababu kuna mema ya Kanisa, na mema ya watu! Sio mazungumzo ambayo hufanywa. Samahani, lakini historia hii imenielimisha sana”.

Ufunguzi wa mwaka wa Mahakama ya kitume 2022
Ufunguzi wa mwaka wa Mahakama ya kitume 2022

Baba Mtakatifu amesema Utafiti shirikishi wa ukweli lazima uwe na tabia ya kila hatua ya mchakato wa mahakama. Ni kweli kwamba katika mchakato kati ya nadharia zinazokinzana wakati mwingine hufanyika katika mchakato; hata hivyo, mabishano baina ya wahusika yanatakiwa yafanyike kila mara kwa kuzingatia kwa dhati yale yanayoonekana kuwa ya kweli kwa kila mmoja, bila ya kujifungia katika maono yake mwenyewe, lakini pia kuwa wazi kwa mchango wa washiriki wengine katika mchakato huo. Baba Mtakatifu amesema, hili la kwenda pamoja katika hukumu ni halali kwa wahusika na walinzi wao, kwa mashahidi walioitwa kudhibitisha kulingana na ukweli, kwa wataalam ambao wanapaswa kuweka sayansi yao katika utumishi wa kesi hiyo, na pia kwa njia ya umoja wa waamuzi. Kwa njia hiyo, utoaji wa haki ndani ya Kanisa ni dhihirisho la utunzaji wa roho, unaohitaji mahangaiko ya kichungaji ili kuwa watumishi wa ukweli na huruma inayookoa. Uaminifu huu wa huduma ya ukweli huwa na umuhimu wa pekee kwa Maaskofu, wanapohukumu kwa nafsi ya kwanza, hasa katika mashauri mafupi zaidi, na vilevile wanapotekeleza wajibu wao kuelekea mahakama zao wenyewe, hivyo pia kuonesha kujali kwao kwa ubaba kwa waamini.

Ufunguzi wa mwaka wa Mahakama ya kitume 2022
Ufunguzi wa mwaka wa Mahakama ya kitume 2022

Huduma ya ukweli hii unachukua umuhimu sana kwa maaskofu, wanahukumu wao binafasi, hasa katika michakato mifupi sana, na hata wanapojikita katika uwajibikaji wao mbele ya mahakama zao, kwa kuonesha hata namna yao ya ushauri kibaba mbele ya waamini wao. Papa Francisko amesema sinodi katika michakato inajikita na zoezi la kila wakati la kusikiliza. Hata katika muktadha huo lazima kujifunza kusikiliza, na siyo kiurahisi kusikia. Lazima kwa maana hiyo kuelewa maono na sababu za mwingine, na karibu kuzifananisha na mwingine.  Kama ilivyo katika mantiki nyingine ya kichungaji, hata shughuli za kimhakama lazima ziweza kusaidia utamaduni wa kusikiliza, kwa kuanzia na utamaduni wa kukutana.  Kwa hivyo majibu ya kawaida kwa shida madhubuti za watu binafsi ni mbaya. Kila mmoja wao, pamoja na uzoefu wake ambao mara nyingi huoneshwa na maumivu, hufanya kwa hakimu wa kikanisa pembe halisi ambayo kila hatua ya kichungaji ya mahakama lazima ipitie. Je, hii inachukua muda? Ndiyo, inachukua muda. Je, inahitaji uvumilivu? Ndiyo, inahitaji subira. Je, inahitaji ubaba wa kichungaji? Ndiyo, inahitaji ubaba wa kichungaji”. Papa amesisitiza.

Kwa namna ya pekee ina uchunguzi wa awali, unaolenga kubaini ukweli, unaohitaji wanaoiongoza kujua jinsi ya kuchanganya taaluma sahihi na ukaribu na kusikilizana. Mahakimu lazima wawe wasikilizaji makini sana wa kila kitu ambacho kinawekwa kwenye mchakato ili kusaidia na kudhibiti uthibitisho wa kubatilisha. Waamuzi lazima wawe wasikilizaji kwa ubora wa kila jambo lililojitokeza katika kesi kwa na kupinga tangazo la ubatili. Wamefungwa kwa hili kwa nguvu ya wajibu wa haki, wenye kuhuishwa na kuungwa mkono na upendo wa kichungaji. Hakika, “huruma ni utimilifu wa haki na udhihirisho angavu wa ukweli wa Mungu”.

PAPA KWA UZINDUZI WA MWAKA WA MAHAKAMA 2022
27 January 2022, 16:57