Hija ya Kitume ya Papa Francisko Cyprus na Ugiriki:kukaribishwa rasmi Larnaca
Na Sr. Angella Rwezaula - Vatican.
Katika ziara yake ya 35 kimataifa, Papa Francisko aliondoka kutoka Roma na Ndege A320 ambayo kwa mara ya kwanza ina bendera ya Italia ambamo ndani mwake kulikuwa na waandishi wa habari 77, miongoni mwake 7 wakiwa ni kutoka Cyprus na Ugiriki. Papa Francisko amewasalimu wote na kuwashukuru kumsindikiza. "Ni safari nzuri ambayo itagusa baadhi ya madonda. Ninatumaini tunaweza kweli kukaribisha ujumbe kutoka kwao", amesema Papa Francisko.
Baada ya kufika uwanja wa ndege wa kimataifa Larnaca saa 9 alasiri, amekaribishwa vizuri. Balozi wa kitume wa Cyprus, Askofu Mkuu Tito Yllana alipanda ngazi kwenda kumsalimia Papa Francoslp kabla ya kushuka. Katika video fupi inaonesha matukio yaliyofuata.