Tafuta

Maaskofu wa Ufaransa katika Mkutano wao Mkuu huko Lourdes Maaskofu wa Ufaransa katika Mkutano wao Mkuu huko Lourdes 

Papa Francisko:Ni kupeleka imani hata mbele ya kishindwa na aibu

Papa Francisko Alhamisi tarehe 4 Novamba 2021,amemtumia ujumbe Askofu Mkuu Éric de Moulins-Beaufort wa jimbo kuu katoliki la Reims,Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Ufaransa katika fursa ya Mkutano wao mkuu wa Maaskofu nchini Ufaransa kwa mwezi Novemba unaofanyikia huko Lourdes.

Na Sr. Angella Rwezaula- Vatican

Katika Gazeti la Osservatore Romano, kuna barua ya Papa Francisko aliyowaandikia maaskofu wa Ufaransa wanaofanya mkutano wao mkuu huko Lourdes ulioanza tangu Jumatatu hi ina mbao kwa siku nane. Mkutano unaofanyika mwezi mmoja baada ya kuchapishwa kwa ripoti ya unyanyasaji iliyoandaliwa na tume huru maalum inayoongozwa na Jean-Marc Sauvé, ambaye takwimu zake yake zimeibua mshtuko wa kweli, kuanzia idadi ya watu walioshambuliwa na makuhani kati ya 1950 na 2020, au zaidi ya 216,000. Papa anaandika “Wakati mnapitia dhoruba iliyosababishwa na aibu na janga la unyanyasaji wa watoto uliofanywa katika Kanisa, ninawatia moyo kubeba mzigo huo kwa imani na matumaini, na ninaubeba pamoja nanyi”

Kwa  ujumbe wake, kwa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Ufaransa (CEF), Askofu Mkuu Éric de Moulins-Beaufort, Papa “anaamini  kwamba kwa pamoja, na chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, mtapata zana za kufanya malipizi na kutoa heshima kwa wahanga na kuwafariji”, anawashauri waamini wote kufanya toba na uongofu wa mioyo, ili kuchukua hatua zote muhimu na ili Kanisa liwe ni makazi salama kwa wote, kuwatunza watu watakatifu wa Mungu, waliojeruhiwa na kufadhaika sana na hatimaye kuanza tena utume  kwa furaha, iliyoelekezwa kwa uthabiti kuelekea siku zijazo.

Katika barua hiyo Papa anaandika kuwa "Katika majaribu na kinzani ambazo unalazimishwa kuishi Papa anaandikia na , ambaye hivi karibuni alipokea baadhi ya maaskofu wa Ufaransa katika ziara ya yao ya kitume, kuwa na uhakika wa msaada na ushirika wa Makao makuu ya  Kitume. “Msiwe na shaka kwamba Wafaransa wanangojea Habari Njema ya Kristo, wanaihitaji zaidi kuliko hapo awali. Kwa maana hiyo ninawakabidhi kwa upole wa pekee wasiwasi wenu wa kina wa ubaba kwa walio wengi sana wa makuhani wenu wanaofanya huduma yao kwa ukarimu na kujitolea, na ambao wito wao mzuri kwa bahati mbaya umepakwa matope. Wanahitaji kuimarishwa na kuungwa mkono katika wakati huu mgumu”.

Katika siku ya kwanza ya mkutano mkuu, ili kudhihirisha umuhimu mkubwa wanaokusudia kuutoa katika kusikiliza maneno ya wahanga, maaskofu waliwaalika watano kati yao kushika nafasi ambazo kwa kawaida zimetengwa kwa ajili ya urais wa uaskofu katika ukumbi mkubwa wa mahali patakatifu, ili kushuhudia tukio lao la kutisha. Mbele ya uaskofuni, waathiriwa walionesha hasira, huzuni, tamaa, lakini pia matarajio na matumaini yao. Maneno yenye nguvu, magumu lakini ya lazima, alikiri Askofu Luc Crépy, wa Versailles na Rais wa Kikundi cha kudumu cha mapambano dhidi ya unyanyasaji kingono katika Baraza la Maaskofu Ufaransa (CEF). “Mabadiliko lazima yatekelezwe na hii ni kazi ya kila mtu, alisisitiza Askofu huyo kwa wanahabari. Akirejerea matarajio ya waathiriwa, Askofu François Touvet, wa Jimbo katoliki la Châlons, aliona kuwa ni jambo la dharura kuhama kutoka katika maneno hadi vitendo sasa, sio tena kuridhika na kutoa hotuba na maandishi, lakini kutenda kwa nguvu. “Lazima tuishi kulingana na matarajio haya na hatuna haki au uwezekano wa kupoteza wito huu” alikazia kiongozi huyo.

Katika ukumbii, ambapo kulikuwa na wahanga walioshiriki katika kuandaa ripoti ya unyanyasaji, maaskofu wengi walisoma baadhi ya vifungu kutoka kwenye waraka huo. Wakati wa mkutano huo, suala la fidia kwa waathiriwa pia lilijadiliwa, katikati ya matarajio mengi: “Kanisa lazima liwatambue watu hawa hata wakati ukweli umepita”, anasisitiza Crépy. Alasiri ya leo na alasiri ya kesho itatolewa kwa usawa kwa suala la unyanyasaji, wakati wakati sala ya toba ambayo imepangwa kufanyika Jumamosi katika uwanja wa kanisa kuu la Mama Maria.

Ulinzi wa kazi ya uumbaji ndio mada nyingine kuu ya mkutano huo wa vuli, ambao unafanyika wakati viongozi wa ulimwengu wamekusanyika huko Glasgow kushiriki katika mkutano wa tabianchi wa Umoja wa Mataifa. Chaguo ambalo Papa Francisko alilipongeza katika barua yake. Siku tatu na nusu zimetengwa kwa ajili ya kusoma waraka wa Laudato si 'na utekelezaji wake katika majimbo yote ya Ufaransa. Kauli mbiu iliyochaguliwa na Baraza la Maaskofu, “Makelele ya Dunia, Makelele ya Maskini”, iliyochukuliwa kutoka katika hati ya Kipapa, ilichaguliwa na Maaskofu ili kutoa nafasi kwa watu wanaoishi katika mazingira hatarishi. Mpango unaokumbuka ule ulioandaliwa miaka miwili iliyopita na Baraza la Maasskofu Ufaransa (CEF) wakati wa mkutano wa mawasilisho katika msimu wa vuli, ambapo zaidi ya watu mia mbili walei walialikwa kuwasilisha tafakari yao juu ya waraka wa Papa Francisko.

 

04 November 2021, 17:48