Tafuta

Papa Francisko:tumieni uzalendo kutunza nyumba yetu ya pamoja

Katika Siku ya Maskini duniani mada ni Maskini mnao siku zote pamoja nanyi.Na ni kweli:ubinadamu unaendelea,unakua,lakini maskini wako nasi daima,ni wengi daima,Kristo yuko ndani yao,Kristo yuko katika maskini.Papa amewatia moyo washiriki wa COP26 wenye majukumu ya kisiasa na kiuchumi kuchukua hatua mara moja kwa ujasiri katika kukabili mabadiliko ya tabianchi.Amekumbuka siku ya kisuria diniani.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya Tafakari na Sala ya Malika wa Bwana, Baba Mtakatifu Francisko, Dominika tarehe 14 Novemba 2021 amesema:"leo tunaadhimisha Siku ya V ya Maskini Duniani, iliyozaliwa kama matunda ya Jubilei ya Huruma. Mada ya mwaka huu ni maneno ya Yesu: “Maskini mnao siku zote pamoja nanyi” (Mk14,7). Na ni kweli, ubinadamu unaendelea, unakua, lakini maskini wako nasi daima na kweli wako wengi daima na Kristo yuko ndani yao, Kristo yuko katika maskini". Papa Francisko akiendelea ameeleza jinis ambavyo tarehe  12 Novemba alikwenda huko Assisi, ambapo walipata wakati mzuri wa ushuhuda na maombi, ambayo yeye binafsi amewaalika waamini na mahujaji waliokuwa wamekusanyika wayapitie tena na kwamba yatawasaidia. Ameshukuru kwa ajili ya mipango mingi ya mshikamano ambayo imeandaliwa katika majimbo na parokia yote ulimwenguni.

COP26: Kuwa na ujasiri wa kuona mbele

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea amesema kuwa "Kilio cha watu maskini, pamoja na kilio cha Dunia, kilisikika katika siku za hivi karibuni katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi COP26, mjini Glasgow". Kwa maana hiyo Papa anawatia moyo wale walio na majukumu ya kisiasa na kiuchumi na kuchukua hatua mara moja kwa ujasiri na kuona mbele; wakati huo huo amewaalika watu wote wenye mapenzi mema kutumia uzalendo hai kwa ajili ya utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja. Vile vile kufuatia na tukio amesema " leo katika, Siku ya Dunia ya Maskini, umefunguliwa usajili kwenye jukwaa la Laudato si ', ambalo linahamasisha ikolojia fungamani".

Siku ya kisukari duniani sala kwa wanaoteseka na ugonjwa huo na wahudumu wa kiafya

Papa Francisko amekumbusha kilele cha Siku ya Kisukari Duniani, ambapo amesema kwamba ugonjwa huo sugu unaosumbua watu wengi wakiwemo vijana na watoto. Anawaombea wote na wale wanaoshiriki uzoefu wa ugumu huo kila siku, pamoja na wahudumu wa afya na watu wa kujitolea wanaowasaidia. Kwa kuhitimisha amesalimia watu warumi, mahujaji wote kutoka sehemu mbalimbali kama vile Hispania na Poland; Kikundi cha Maskout wa Palestrina na waamini wa Parokia ya Mtakatifu Timoteo, Roma na Parokia ya Bozzolo.  Kwa wote amewatakia Dominika njema na wasisahau kusali kwa ajili yake.

14 November 2021, 12:56