Tafuta

2021.11.25: Papa Francisko amekutana na Familia kubwa ya Mtakatifu Paulo katika fursa ya kumbu kumbu ya miaka 50 tangu kifo cha Mwanzilishi Mwenyeheri Padre Giacomo Alberione. 2021.11.25: Papa Francisko amekutana na Familia kubwa ya Mtakatifu Paulo katika fursa ya kumbu kumbu ya miaka 50 tangu kifo cha Mwanzilishi Mwenyeheri Padre Giacomo Alberione. 

Papa Francisko ahutubia familia kubwa ya Mt.Paulo gwiji wa mawasiliano katika uinjilishaji

Padre Alberion mara nyingi alirudia kusema mwanzilishi wao wa kweli ni Mtume Paulo.Siku zote alijionesha kwao katika msukumo na baba,kama mfano wa kuiga katika mchango kamili kwa Bwana Yesu Kristo na Injili yake,akijiruhusu mwenyewe kuongozwa na upendo wake katika njia ya utakaso.Ni maneno ya Papa alipokutana na familia kubwa ya Shirika la Mtakatifu Paulo wakiwa wanaadhimisha miaka 50 tangu kifo cha Mwanzilishi wa Shirika Padre Alberione.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko alhamisi tarehe 25 Novemba 2021 amekutana na Familia ya Mtakatifu  Paulo wakiwa katika fursa ya kuadhimisha miaka 50 tangu kifo cha Mwenye heri Giacomo Alberione, mwanzilishi wa shirika lao lenye matawi mengi ya kike na kiume walio wekwa wakfu na washirika walei ambao kwa pamoja wanaunda familia kubwa ya Paulo ulimwenguni kote. Papa Francisko ametoa shukrani kwa Mkuu wa Shirika hilo la Mtakatifu Paulo kwa kila watendalo kwa niaba ya wote. Kumbukumbu hiyo ni kwa ajili ya Kanisa na kwa namna ya pekee kwao na ambayo ni fursa kufanya kumbu kumbu ya mambo mengi yaliyotendwa na Roho Mtakatifu kwa njia ya Mwenyeheri Giacomo Alberione na kwa njia yake kuendeleza uthiibtisho wa karama katika mukutadha wa sasa wa matarajio ya Uinjilishaji mpya.

Mkutano wa Wajumbe wa Familia ya Mtakatifu Paulo katika fursa ya miaka 50 tangu kifo cha Mwenyeheri Padre Alberione Mwanzilishi wa Shirika hilo.
Mkutano wa Wajumbe wa Familia ya Mtakatifu Paulo katika fursa ya miaka 50 tangu kifo cha Mwenyeheri Padre Alberione Mwanzilishi wa Shirika hilo.

Mwanzilishi wao  Papa amesema alitambua  kutazama bele na kupokea katika karne ya XX hitaji ambalo Neno la Bwana linaendelea na kutukuzwa vile vile kama wao walivyo fanya (2Ts 3,1) na kueleza kwa utambuzi na kuthamanisha zana na lugha ya dhati iliyotolewa katika maendeleo ya kiteknolojia. Sura ya shuhuda wa Neno inaonesha kama alivyo fafanua  Mtakatifu Paulo VI mnamo 1969 kwamba alikuwa ni  mnyenyekevu, mkimya, hasiyechoka, anakesha na daima katika kupokea mawazo wakati akiwa kwenye sala na katika huduma; alikuwa makini na kujua ishara za nyakati, kwa maana hiyo alikuwa gwiji wa mtindo wa kufikia roho za watu”, amesisitiza Papa Francisko.  Kwa kuongeza kunukk maneno ya Mtakatfu Paulo VI Papa amesema: “ Padre Alberione alitoa kwa Kanisa zana mpya za kujeleza, mpya kwa ajili ya kutoa uhai na utume mkubwa, wenye uwezo mpya na dhamiri mpya na yenye uwezo wa utume wake katika dunia ya sasa na vyombo vya kisasa ( Hotuba kwa familia ya Paulo 28,Juni 1969).

Mkutano wa Wajumbe wa Familia ya Mtakatifu Paulo katika fursa ya miaka 50 tangu kifo cha Mwenyeheri Padre Alberione Mwanzilishi wa Shirika hilo.
Mkutano wa Wajumbe wa Familia ya Mtakatifu Paulo katika fursa ya miaka 50 tangu kifo cha Mwenyeheri Padre Alberione Mwanzilishi wa Shirika hilo.

Padre Alberio alipendelea kurudia mara nyingi kusema kwamba mwanzilishi wao wa kweli wa shirika ni Mtakatifu Paulo mtume. Papa amesema Yeye daima aliwaonesha alivyokuwa akimwiga na kuwa baba kama mfano wa wa kujitoa kabisa kwa Bwana wetu Yesu Kristo na Injili.  Kumwiga kwa nguvu ndiyo njia ya utakatifu ambayo pia kwao ni mwaliko wa utendaji wa hutuma waliyo kabidhiwa na katika shughuli za kitume ambazo wanatenda kwa mwanga wa furaha ya Injili. Shauku hiyo kwa ajili ya Injili iweze kufikisha  malengo hayo yao kama anavyoandika Mtakatifu Paulo: “Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nalijifanya mtumwa wa wote, ili nipate watu wengi zaidi. Nalikuwa kama Myahudi kwa Wayahudi, ili niwapate Wayahudi; kwa wale walio chini ya sheria, nalikuwa kama chini ya sheria, (ingawa mimi mwenyewe si chini ya sheria), ili niwapate walio chini ya sheria. Kwa wale wasio na sheria nalikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo), ili niwapate hao wasio na sheria. Kwa wanyonge nalikuwa mnyonge, ili niwapate wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu. Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya Injili ili kuishiriki pamoja na wengine”.(1Kor 9,19-23).

Mkutano wa Wajumbe wa Familia ya Mtakatifu Paulo katika fursa ya miaka 50 tangu kifo cha Mwenyeheri Padre Alberione Mwanzilishi wa Shirika hilo.
Mkutano wa Wajumbe wa Familia ya Mtakatifu Paulo katika fursa ya miaka 50 tangu kifo cha Mwenyeheri Padre Alberione Mwanzilishi wa Shirika hilo.

Papa Francisko amesema ni mtakatifu Paulo aliyemshauri Mwanzilishi wao njia ambazo angeweza kuendeleza katika utume wa familia ya kitawa licha ya tofauti zilizopo kwa kuwafikia katika umoja wao na kwa njia ya Kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na ufalme na mamlaka katika ulimwengu wa roho. Kwa maana hiyo Papa amefafanua shughuli za familia kubwa hiyo kwamba: Jumuiya ya Mtakatifu Paulo na Mabinti wa Mtakatifu Paulo wanajikita kwenye shughuli za vitabu, majarida, magazeti na uchapishaji wa digitali. Wafuasi wa Mungu Mwalimu wao ni kwa njia ya utume wa kiliturujia, kipadre na kiekaristi. Masista wa Yesu Mchungaji Mwema wao ni  katika huduma ya parokia. Masista wa Taasisi ya Malkia wa Mitume wakiwa na utume wa uhamasishaji wa miito. Na baadaye kuna mchango maalum wa taasisi za maisha ya wakfu kwa walei: Taasisi ya Malaika Mkuu Gabriel; Taasisi ya Maria Mtakatifu wa habari njema; Taasisi ya Kuhani Yesu na Taasisi ya Familia Takatifu. Wanachama wa Taasisi hizi, pamoja na Washirika wa Paulini, wote amesisitiza kuwa wanatumikia Injili zaidi ya yote katika mazungumzo na ulimwengu wa kisasa, ambao, kama walei na wa kidunia, wameingizwa kikamilifu. Ni kweli kwamba mageuzi ya kiteknolojia yamepelekea jumuiya nzima ya kikanisa kuchukua zana za kisasa za mawasiliano kuwa ni vipengele vya kichungaji na vya kawaida; Walakini, uwepo wao bado ni muhimu sana leo hi ambapo Papa amesema zaidi na zaidi kwamba ni kuhuishwa na uzuri wenyewe na kuimarishwa na uzoefu wa kufanya kazi katika nyanja hiyo.

Mkutano wa Wajumbe wa Familia ya Mtakatifu Paulo katika fursa ya miaka 50 tangu kifo cha Mwenyeheri Padre Alberione Mwanzilishi wa Shirika hilo.
Mkutano wa Wajumbe wa Familia ya Mtakatifu Paulo katika fursa ya miaka 50 tangu kifo cha Mwenyeheri Padre Alberione Mwanzilishi wa Shirika hilo.

Papa Francisko akiendelea na hotuba yake amejikita kuelezea muktadha wa mchakato wa sinodi ambao umeanza sasa, hivi karibuni na kuwaomba wasikose kutoa mchango wao wa dhati. Kwa maana hiyo amewatia moyo ili waendelee kufanya kazi pamoja  katika mtandao mkubwa na kutoa mchango wa kila mmoja kwa wajibu wake wa shauku ya Mwenyeheri Alberione. Maadhimisha ya mwanzilishi wao ya Miaka 50 tangu kuzaliwa kwake mbinguni, imewapa fursa ya kujua tena vema thamani ya kinabii ya ushuhuda wake. Kwa kufuata mfano wake na kwa maombezi yake, wao pia wanachagua njia ya mawasiliano kuwa  ndiyo muhimu, kama yeye mwenyewe alivyosema: “Yesu Kristo aweze kujulikana kwa wanadamu wa wakati wetu kwa kutumia wakati wetu”. Papa Francisko amewashukuru kwa jitihada zao za kazi hasa kusali ili Watu wa Mungu watakatifu wamwilishwe daima na Neno la Mungu. Kwa kutafuta katika kila kitu na moyo uliojaa maisha na katika utume wao, daima utukufu wa Mungu tu na amani kwa watu wote wenye mapenzi mema. Mama Maria Malkia wa Mitume awasindikiza kwenye njia za ulimwengu kama mitume wa Injili walio wazi daima kujifungua kwa watu wa kawaida kama alivyokuwa anapenda kusema Padre Alberione. Baba Mtakatifu naye anawasindikiza kwa sala zake na kuwabariki, lakini pia wasishau kusali kwa ajili yake.

Mkutano wa Wajumbe wa Familia ya Mtakatifu Paulo katika fursa ya miaka 50 tangu kifo cha Mwenyeheri Padre Alberione Mwanzilishi wa Shirika hilo.
Mkutano wa Wajumbe wa Familia ya Mtakatifu Paulo katika fursa ya miaka 50 tangu kifo cha Mwenyeheri Padre Alberione Mwanzilishi wa Shirika hilo.
25 November 2021, 17:56