Tafuta

2021.11.24 Zawadi ya Papa ya  Mtambo wa uzalishaji wa Oksijeni katika Ospitali ya Mtakatifu Rafaeli jijini Bagdadi, Iraq ukiwa unabarikiwa. 2021.11.24 Zawadi ya Papa ya Mtambo wa uzalishaji wa Oksijeni katika Ospitali ya Mtakatifu Rafaeli jijini Bagdadi, Iraq ukiwa unabarikiwa. 

Iraq:Papa Francisko ametoa zawadi ya mtambo kwa ajili ya uzalishaji wa oksijeni

Papa ametoa zawadi ya mtambo wa kuzalisha Oksijeni ya madawa kwa ajili ya Hospitali ya Mtakatifu Rafaeli jijini Baghdad nchini Iraq.Tarehe 23 Novemba 2021 ilikuwa ni uzinduzi rasimi wa mtambo huo.Mhusika wa Hospitali hiyo Sr.Maryanne Pierre, O.P.,amemshukuru Papa kwa zawadi hiyo yenye thamani kubwa katika wakati huu ambao ni wa dharura ya janga la UVIKO-19.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Mnamo Jumanne tarehe 23 Novemba 2021, kwa ibada ya Baraka Takatifu wamezindua rasimi mtambo kwa ajili ya uzalishaji wa Oksijeni ya dawa katika Hospitali ya Mtakatifu Rafaeli, jijini Baghdad nchini Iraq ambayo ni zawadi kupitia mfuko uliowekwa wa Vatican, wa Baraza la Makanisa ya nchi za Mashariki na Mfuko wa Sadaka ya Kitume wa Papa na ambao umewezesha kufanikisha msaada huo mkubwa katika wakati huu ambao ni muhimu kihistoria kutokana na janga la uviko-19 ulimwenguni kote

Uzinduzi rasmi wa mtambo wa uzalishaji Oksijeni katika Hospitali ya Mt. Rafaeli jijini Bagdad
Uzinduzi rasmi wa mtambo wa uzalishaji Oksijeni katika Hospitali ya Mt. Rafaeli jijini Bagdad

Mhusika wa Hospitali hiyo Sr. Maryanne Pierre, O.P., wa Shirika la Watawa Wadominikani, ameonesha shukrani zake kubwa kwa Baba Mtakatifu kwa zawadi yenye thamani kubwa. Naye Bwana Ghaleb Mansoor Sawa, Mkurugenzi wa kituo hicho na Dk. Amjad Khacheek Majeed, Mkuu wa Kitengo cha maabara ya uchunguzi, wamethibitisha kuhusu mtamba huo unavyo fanya kazi vizuri na kwa miezi kadhaa wamebainisha kuwa umezalisha oksijeni ya kutosha na sio kwa ajili ya Hospitali ya Mtakatifu Rafaaeli tu lakini pia kwa kuzalisha kwa ajili ya Hospitali nyingine za nchi hata na miji mingine.

Uzinduzi rasmi wa mtambo wa uzalishaji Oksijeni katika Hospitali ya Mt. Rafaeli jijini Bagdad
Uzinduzi rasmi wa mtambo wa uzalishaji Oksijeni katika Hospitali ya Mt. Rafaeli jijini Bagdad

Uwezo wa mtambo huo hata hivyo kwa mujibu wao, wamesema umewezesha kukabiliana vizuri na dharura ya  COVID-19  na itakuwa muhimu bila shaka katika wimbi lijalo la janga hili katika hospitali hiyo.

Uzinduzi rasmi wa mtambo wa uzalishaji Oksijeni katika Hospitali ya Mt. Rafaeli jijini Bagdad
Uzinduzi rasmi wa mtambo wa uzalishaji Oksijeni katika Hospitali ya Mt. Rafaeli jijini Bagdad
24 November 2021, 16:56