Zawadi ya Papa kwa watoto yatima wa Foyer Nazareth
Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.
Baadhi ya majina yanaosomeka kama vile Andréa, Ada, Lady, Odilia, Immaculéee, Joyce, Vanecia, Mélina, Saint Eude, Antony Mercia, Jessica, Franck, Daniel Beni, Gloire, Anaèlle… na wengine au mchoro, nukta lakini ni saini ya watoto 22 wa kituo cha watoto yatima wa Foyer Nazareth, kando ya mji mkuu wa Jamhuri ya Congo katika barua waliyomtumia Baba Mtakatifu Francisko.
Katika barua iliyoandikwa tarehe 3 Oktoba, kwa mkono na karamu ya blu kwenye kurasa tatu kutoka kwenye daftari wanazotumia shuleni watoto, wameandika kwa kusema: “Merci, Merci, Merci beaucoup” (“Asante, asante, asante sana), Papa kwa zawadi yake aliyoituma, ambamo ni madawa kwa ajili ya ugonwa wa seli mundu ambayo inakuwa shida upatikanaji wa madawa hayo katika sehemu yao. Hata hivyo pamoja na shida walizo za upatikanaji wa maji na lishe ni wazi kabisa kupata madwa kwa ajili ya uogonwa huo na wakati bei zake ni za juu.
Yeye mwenyewe aliandika barua hiyo kwa “Saint Père Pape François” : Baba takatifu , wazo lako kwa ajili yetu la kutuma vifaa vya kiafya kwa masisita wawili wanaotunza watoto yatima Odilia na Elise limetufanya kuona ndani mwake maneno ya Maandiko Matakatifu ya Maisha. Ndiyo, tumebaki bila maneno, lakini moyo wetu hauwezi kunyamaza na kusifu Bwana… Baba Mtakatifu madawa haya kwetu sisi tunaamini na kuthibitisha kuwa Bwana ametutembelea kupitia kwako Mfuasi wa Bwana wetu na mwokozi Yesu Kristo. Na sisi kwa mara nyingine tena tunasifu na kumwomba Neema zake na nguvu zake kwa ajili yako”.
Katikati ya ugumu wa kuishi na vizingiti vya rasiliamali, lakini bila kukata taaa, watoto wadogo wa Foyer Nazareth walichukua karatati na kuomba msaada kwa Papa. Yeye hakusubiri sana na akajibu kwa njia ya Msimamizi wa Sadaka ya Kitume Kardinali Konrad Krajewski na kupitia ubalozi wa kitume nchini humo ambao wameweza kuwafikishia vifaa hivyo ambavyo ndani mwake kulikuwa na madawa. Nje ya mabox hayo yameandikiwa zawadi ya Baba Mtakatifu” na kuwafikisha kwa wakuu wa Kituo cha watoto Yatima, Sr Elise Vouakouanitou, mwenye umri wa miaka 63 anni wa Congo Pointe-Noire. Sr. Elise na watoto wa Brazzaville tunatoa shukrani kwa Mungu kwa ajili ya Papa na Ubalozi kwa ajili ya umakini usio na kifani kwa haya. Kwa njia ya ishara hiyo tunatambua kuwa jina la waraka wa mwisho wa Fratelli tutti siyo wa bure .., lakini ni mpango wa kazi na utume ambao wewe mwenyewe ulikubali kwa niaba ya Kristo na Kanisa na ndiyo tunathibitisha kuwa sisi sote ni ndugu.
Jumuiya hii imefafanuliwa hivyo katika kufanya uzoefu kila siku kwenye kuta za Foyer Nazareth, mahali mbapo watoto wanlala lakini haya kuwa na elimu fungamani ambayo inajikita kwenye misingi ya kikristo. Hasa upendo na udugu wa kibindamu kwa mujibu wa Sr. Vouakouanitou akihojiwa na Vatican News, mara baada ya kupokea vifaa hivyo. Yeye hakukosa kueleza matatizo makubwa ya kuwalisha na kuwatunza kila siku watoto ha 22, wenye umri tofauti na ambao wanatoka katika hali tofauti za maisha. Ni watoto yatima walioachwa au peke yao au wenye wazazi wenye matatizo ya kiakili. Baadhi yao kama alivyo sema wana magonjwa kama ya ukosefu wa damu, kwa namna ya kusema anemia sugu, kutokana na ukosefu wa dawa inayo fa ana kwa maana ya kupokea dawa kama hizo wanaweza kweli kupata tiba na wengine wanao magonjwa mengine sugu. Tiba kwa ajili ya watoto hao inakuwa ngumu sana katika nchi, kwani madawa kwa kawaida yanauzwa bei ya juu zaidi ambapo ni vigumu kwao kupata kwa fedha za kukidhi haja hiyo.