Tafuta

2021.10.23  Maria Montessori. 2021.10.23 Maria Montessori. 

Papa:Montessori aliacha ishara ya ujenzi wa dunia ya kidugu na amani

Papa Francisko ametuma ujumbe kwa washiriki wa Kongamano la Kimataifa la Kazi ya kitaifa ya Montessori aliyekuwa mtaalam wa kufundisha na juhudi kwa ajili ya ulimwengu wa amani,kukumbuka miaka 150 tangu kuzaliwa kwake ambapo Papa anawashauri watazame mfano wake kwa ajili ya kusaidia mafunzo ya watu mshikamano na uzalendo wa ulimwengu ulio wazi katika mazungumza na ukarimu.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Katika fursa  ya Kongamano la Kimatafaifa lililoandaliwa kwa siku ya 23-24 Oktoba 2021 katika  fursa ya kukumbuka Miaka 150 ya kuzaliwa kwa Maria Montossori mnamo  tarehe 31 Agosti 1870 huko Chiaravalle, wilaya ya Ancona, Italia, Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake uliotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican ambapo anawasalimia wote na kuelezea kufurahishwa kwa mpango huo unaojielekeza kufanya kumbu kumbu ya mtu huyo mkubwa wa mafundisho, sura kati ya sura kubwa za utamaduni wa miaka 1900 ambaye aliacha ishara ya kina katika muktadha wa elimu na katika jamii nzima.

Katika kukumbusha juhudi kwa ajili ya ujenzi wa dunia ya kidugu zaidi na amani ni matumaini  Baba Mtakatifu kuwa furaha hiyo ya maana iweze kuwa karimu kwa kijikita kwa shauku kwa ajili ya vizazi vipya ili  kuunda mtu wa mshikamano, mzalendo  wa ulimwengu ulio wazi katika mazungumzo na ukarimu. Baba Mtakatifu anawakikisha sala zake na kuwapa baraka ya Bwana kwa waandaaji, watoa mada na wale wote watakaoshiriki katika tukio hili la kumbu kumbu.

Hata hivyo kuhusiana na mpango huo ambao unafanyika kwa njia ya mtanfao ni kutokana na kuendelea kwa dharura ya kiafya ya UVIKO -19, ambapo  Baraza la  Kazi ya Kitaifa ya Montessori (ONM) iliyofanya kikao chake mnamo tarehe 2 Julai 2021 baada ya kutathimini mbadala, waliamua kufanya Kongamano la Kimataifa katika kuadhimishia miaka 150 tangu kuzaliwa kwa Maria Artemisia Montessori mnamo tarehe 31 Agosti 1870 huko Chiaravalle, wilaya ya  Ancona Italia kwa njia ya mtandao.  Kongamano hiyo limeandaliwa na Kazi ya Kitaifa ya Montessori kwa ushirikiano na Chama cha Kimataifa cha Montessori na Montessori-Pierson Publishing Company, na Kata ya Chiaravalle.

Katika Kongamano hilo la siku mbili 23 - 24 Oktoba2021 linawaona watoa mada kuhusu masuala ya kisayansi, kielimu, kifalsafa  na kijamii katika wazo na kazi ya Maria Maria Montessori.  Aidha wanawakilisha pia Mapango mkuu wa Kitaifa  (PRIN 2017) kwa kuongoza na mada “Maria Montessori: kati ya historia, na usasa. Mapokeo na kuenea kwa ufundishaji wake nchini Italia tangu miaka 150 ya kuzaliwa kwake.

23 October 2021, 16:14