Tafuta

2021.10.11 Juma la 49 la kijamii katoliki Italia huko taranto 2021.10.11 Juma la 49 la kijamii katoliki Italia huko taranto  

Papa Francisko kwa Juma la 49 la kijamii katoliki Italia:Chachu ya upendo itazame maskini

Katika ujumbe wa Papa Francisko kwa washiriki wa Juma la 49 la Kijamii KATOLIKI Italia ambao wamejikita katika muktadha wa“Laudato sì’”,anawaonesha njia za tumaini ili kurudisha hali nzuri dhidi ya mgogoro ulioletwa na janga na kuhamasisha michakato ya mabadiliko ya kudumu kwa faida ya kizazi cha vijana.“Hatuwezi kujiachia na kubaki kuchungulia dirishani,hatuwezi kukaa na sintofahamu bali ni kuchukua hatua za kuwajibika".

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko ametuma ujumbe wake kwa washiriki wa Juma la 49 la Kijamii katoliki Italia, ambalo limezinduliwa tarehe 21 na litafungwa 24 Oktoba 2021 linalofanyika hukoTaranto Linaongozwa kwa hakika na kauli mbiu “sayari tunayotegemea. Mazingira, kazi, wakati ujao, vyote hivyo vinaunganika. Katika ujumbe wake, Papa amewasalimia kindugu, kuanzia kwa Kardinali Guaritiero Bassetti, Rais wa baraza la Maaskofu Italia, Askofu Mkuu Filippo Santoro wa Jimbo Kuu la Taranto na Maaskofu wote waliopo na wajumbe wa kamati ya kisayansa ikiwa ni pamoja na waandalizi, na vyama vyote, na wote  waalikwa na ambao  wanafuatilia tukio hili. Tukio hili lina ladha maalum amesema Papa ambayo ni kuhisi haja ya kukutana na kutazamana uso, kutabasamu na kuandaa mipango, kusali na kuota ndoto kwa pamoja. Hili ni jambo la lazima katika mukatadha wa mgogoro uliosababishwa na UVIKO, pamoja na kwa ujumla wa kiafya na kijamii. 

Ili kuondokana nacho inaombwa ujasiri zaidi hata kwa wakatoliki wa Italia. Papa amesema “Hatuwezi kujiachia tu na kubaki kuchungulia kutoka dirishani, hatuwezi kukaa na sintofahamu na bila kuchuka hatua ya kuwajibika kuhusiana na wengine na kuelekeza kijamii. Wote wanaitwa wawe chachu ambayo inafanya kuumuka kwa unga (Mt 13,33).  Janga limefunua  na kuonesha majivuno ya wakati wetu na kutufanya tukirie Mwenyezi, kwa kukanyaga ardhi ambayo tunaishi na mazingira ambayo tunaishi. Ili kuamka tena katika hili  lazima kumwongokea Mungu na kujifunza kuwa na matumizi mema ya zawadi zake, iliyo  kwanza zaidi ya yote ni kazi yake ya uumbaji. Kusikosekane uongofu wa kiikolojia, lakini pia hasa shauku ya uongofu wa kijumuiya.

Hata hivyo katika jambo hilo lililotokea lazima kusikiliza hata mateso ya maskini, walio wa mwisho, wenye kuhangaika, familia zilizochoka kuishi katika maeneo machafu, zilizonyonywa, maeneo yaliyochomwa moto, maneo yaliyo raruliwa na ufisadi na rushwa. Kutokana na hayo ndiyo Papa ametaka kuwasaidia watafakari ili kutembea kwa shauku kubwa katika njia ya matumaini na ambazo wanaweza kuziona katika mambo matatu. Papa amesema kuwa kuna haja ya matumaini na ambayo yanaongozwa katika kauli ya Juma la kijamii huko Taranto, mji ambao ni ishara ya matumani katika vipingamizi vya nyakati zetu, na Sayari tunayo tarajia. Mazingira, kazi, wakati ujao vyote vinaunganika pamoja. Hii ina maana ya kwamba kuna shauku ya maisha, kiu ya haki, ukamilifu unaobubujika kutika katika jumuiya iliyopata pigo la janga.

Ya kwanza ni umakini wa mapitio. Kuna watu wengi tunakutana nao katika maisha yetu wakati wanajikuta katika mahangaiko. Vijana wanaolazima kuacha Nchi zao za asili ili kuhamia mahali pengine, ukosefu wa ajira au unyonyaji usio na mwisho; wanawake ambao wamepoteza kazi katika kipindi cha janga  au wanalazima kuchagua kati ya ujauzito au taaluma; wafanyakazi walioachwa nyumbani bila fursa; maskini na wahamiaji ambao hawapokelewi na kufungamanishwa; wazee walioacha katika upweke wao; familia waathiriwa na madeni, mchezo wa kamali na ufisadi; wajasiliamali wenye matatizo na uongezekaji wa makundi ya kihalifu ya mafya; jumuiya zilizoharibiwa na uchomaji wa moto… Lakini pia kuna watu wengi wagonjwa, watu wazima na watoto, wafanyakazi waliolazimika kufanya kazi bila malipo au bila maadili na mara nyingi katika hali zisizo na usalama. Ni historia ambazo zinatufanya kujiulize, na ambapo hatuwezi kubaki na sintofahama, Papa amebanisha. Kwamba ni kwa ajili ya kaka na dada hao waliosulibiwa na ambao wanasubiri ufufuko. Ubinifu wa Roho utusaidie bila kuacha lolota la kishawishi ili uhalali wao wa matumaini uweze kutimizwa.

Hatua ya pili ambayo Papa Francisko amependa kuileleza ni chachu dhidi ya kusimama. Ikiwa tunaona majimbo, maparokia, jumuiya, vyama, harakati, makundi ya kikanisa yamechoka na kukata tamaa, wakati mwingine kujiachia mbele ya hali ngumu, Tunaona unyafuzi. Kinyume chake, upendo wa Mungu kamwe hausimami na kukataa tamaa, maana unaamini yote na kutumaini yote (1 Kor 13,7).  Upendo daima unatusukumaa na kutuzuia kusimama. Unatuweka katika injini kama waamini na mitume wa Yesu ili kutembea katika njia za ulimwengu kwa mujibu wa Yule ambaye ni njia (Yh 14,6) na aliyeanza mchakato huo katika njia zetu. Papa ameomba wasikae katika sakrestia, wasisimame katika makundi ya wasomi ambayo mara nyingi hujibagua na kujifungia binafsi. Matumaini yako safarini daima na yanapitia hata kwa njia ya jumuiya ya kikristo, ya watoto wa ufufuko ambao wanatoka nje, kutangaza, kushirikisha kusindikiza na kupambana kwa ajili ya ujenzi wa Ufalme wa Mungu.

Kuhusu suala hili njia ya kati ni kucheleweshwa kidogo kwa maafa. Inahusu kufafanua upya maendeleo. Maendeleo ya kiteknolojia na uchumi ambayo hayaachi ulimwengu bora na maisha bora na fungamani hayawezi kuzingatiwa maendeleo (Ft 194). Wakati mwingine hofu na ukimya hutawala, ambavyo huishia kupendelea hatua ya mbwa mwitu wa ulimwengu wa watu wa chini na ya masilahi ya mtu binafsi. Hatuogopi kukemea na kupinga uharamu, lakini pia hatuogopi juu ya kupanda mbegu ya wema! Papa Francisko ametoa ushauri katika eneo hilo lilolokubwa na uchafuzi mwengi na uharibua kwa wakkristo wasisite kutangaza lakini kuchukuwa wajibu wa kuunda mitandao ya ya kuthibiti. Katika Waraka wa Laudati si imeandikwa kuwa haotoshi kupatanisha katika njia za kati, kutnza maumbe na na fesha, au kihifadhi mazingira na maendeleo.

Njia ya tatu na ya mwisho ambayo papa Francisko amependa kuwashauri njia ya moja kwa moja ambayo huwezi kurudi nyumba. Hii inatolewa na kilio cha maskini na ile ya dunia. Hii ni kwa sababu amasema matumaini yanatualika kwamba hatuwezi kubadilisha dira, na kwamba tunaweza daima kufanya lolote lile la kutoa suluhishi la matatizo. Amemnukuu Askofu Tonino Bello, kwamba ni nabii wa ardhi ya Puglia alikuwa anapenda kurudia maneno kuwa “hatuwezi kuacha kutumainia”. Hivyo Papa ameongeza kusema kwamba “Tunapaswa kuandaa matumaini. Tunasubiliwa uongofu ambao uguse awali ya yote ikolojia ya mazingira, ya kibinadamu na ikolojia ya moyo. Mabadiliko yatakuwapo tu ikiwa dhamiri itafundawa na si kutafuta suluhishi rahisi ya kulinda wale ambao wana hali nzuri katika, ni katika mchakato wa kudumu wa kubadilisha kwa ajili ya kizazi. Uongofu huo wa kubasilisha ikolojia kijamii, unaweza kukuzwa wakati huu ambao umefafanuliwa kama mpito wa kiikolojia, mahali ambapo chaguzi za kutimiza zisiwe tu matunda ya ugunduzi mpya wa kiteknolojia, lakini hata upyaisho wa mitindo ya kijamii.

Mabadiliko ya wakati ambayo yanapitiwa wakati huu yanahitaji miito ya lazima.  Amehimiza watazame a katika maana hiyo ishara nyingi za matumaini, kwa watu wengi ambao Papa amependa kuwashukuru kwa sababu mara nyingi katika kazi yao ya kijificha, wanajibika kuhamasisha mitindo tofauti ya kiuchumi na usawa zaidi na makini kwa watu. Kwa maana hiyo sayari inayosubiliwa, ile ambayo utamaduni wa mazungumzo na wa amani utaweze kuleta matunda siku moja na mahalia ambapo kazi yenye  hadhi kwa watu na ulinzi  wa  uumbaji utakuwao na  mahali ambapo dunia za tamaduni tofauti zitakutana  kwa kuongozwa na wasiwasi shirikishi kwa ajili ya wema wa pamoja. Papa anawasindikiza kwa sala kwa ajili ya kazi yao na kuwatia moyo amewabariki na kuwatakia waendelee kwa shauku na udhati wa mapendekezo yao katika siku hizi za mkutano.

UJUMBE WA PAPA KWA WIKI YA 49 YA KIJAMII ITALIA
21 October 2021, 16:42