Tafuta

Papa Francisko:Uhuru wa imani ni katika kuhudumia wema wa wengine

Katika katekesi ya Papa,Jumatano 20 Oktoba 2021 kwa waamini na mahujaji waliofika kwenye ukumbi wa Paulo VI,ameeleza juu ya mantiki ya uhuru wa na upendo kwa mujibu wa imani ya Kikristo.Uhuru unaongozwa na upendo na ndiyo njia pekee inayofanya kuwa na uhuru kwa wengine na binafsi.Kwa hakika ikiwa uhuru siyo huduma ni zoezi.Inahitaji kuchagua kila siku kwa dhati, njia hiyo.Na kuamini kuwa wengine siyo kizingiti cha uhuru wangu, nifursa ya kujikamilisha

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumatano tarehe 20 Oktoba ameendelea na katekesi yake katika Ukumbi wa Paulo VI, Vatican kwa kuongozwa na Barua ya Mtakatiofu Paulo kwa Wagalatia. Akianza katekesi hiyo ametoa mfano wa mtoto aliyekuwa anacheza cheza mbele yake. Lakini akiendelea na tafakari ya Katekesi amesema Mtume Paulo kwa barua yake kwa Wagalatia, taratibu taratibu anaanza kutuonesha mapya ya imani. Na ni kweli mapya makuu kwa sababu hayapyaishi baadhi ya mantiki ya maisha tu, lakini yanatupeleka ndani ya maisha yale mapya ambayo tulipokea kwa njia ya Ubatizo. Hapo alijionesha zawadi kubwa zaidi ya kuwa wana wa Mungu. Kwa kuzaliwa katika Kristo sisi sote tumepita kutoka katika dini za kisheria na kufika imani iliyo hai ambayo kiini chake ni katika umoja na Mungu na ndugu yaani katika upendo. Tumepitia kutoka utumwa wa hofu na dhambi hadi kufikia uhuru wa kuwa wana wa Mungu. Na kwa mara nyingine linakuja neno uhuru… Papa amebainisha.

Papa akiingia ukumbi wa Paulo VI
Papa akiingia ukumbi wa Paulo VI

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea amesema leo hii tujaribu kujua vema ni  maana ya  uhuru kwa mujibu wa  Mtume. Paulo anathibitisha kuwa ni kitu kingine kwani anasema mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, (Gal 5,13). Papa ameongeza kusema, uhuru siyo kuishi kwa majivuno, au kwa silika, utashi binafsi na msukumo wa ubinafsi; hapana, kinyume chake uhuru wa Yesu unatufikia ka njia ya upendo kwa wengine.  Je huo ni utumwa? Uhuru wa Kristo kwa namna nyingine anasema unaweza kuwa utumwa ambao unamambo makuu yanayootupeleka katika huduma ya kuishi kwa ajili ya wengine. Uhuru wa kweli, kwa maneno mengine unajieleza kilamilifu kwa njia ya  upendo. Kwa mara nyingine tunajikuta na  ulinganifu wa Injili kwamba tuko huru ikiwa tuna hudumia na siyo kufanya kile ambacho tunataka. Tuko huru katika huduma na hapo kuna uhuru kamili; Tunajikamilisha kwa kipimo ambacho tunajitoa na tuna ujasiri wa kujitoa; tuna maisha ikiwa tunayapoteza (Mk 8,35). Hiyo ndiyo Injiri safi! Papa amefafanua. Lakini je ni jinsi gani ya kuelezea juu ya ulinganifu huo na kwa nini ulinganifu? Jibu la Mtume ni rahisi sana japokuwa maana inahitaji jitihada, maana yeye anasema kwamba: “tumikianeni kwa upendo”. Papa amesema “Hakuna uhuru bila upendo. Uhuru wa ubinafsi wa kufanya kile ambacho ninataka siyo uhuru, kwa sababu unarudia binafsi, wala hauzai matunda”. Kwa njia ya upendo ndio upendo wa Kristo ambao unatupatia uhuru, ni uhuru ambao unatondoa katika utumwa ulio mbaya sana ule wa umimi;

Kwa mujibu wa Papa Francisko amebainisha kwamba uhuru unakua kwa njia ya upendo. Lakini lazima kuwa makini, kwani si upendo wa liwaya na wala wa kimapenzi ambao unatafuta kwa urahisi kile ambacho unataka na kupendelea; hapana, ni upendo ambao tunauona katika Kristo wa upendo. Ndiyo upendo wa kweli na unao okomboa. Ni upendo ambao unaangaza katika huruma ya bure, unaojikita kuona Yesu ambaye alikuwa anaosha mitume wake miguu yao na kusema: “nimewapa mfano ili nanyi mfanye kama nilivyo fanya mimi (Yh 13,15). Kwa maana ya kuhudumia wengine. Kwa mujibu wa Paulo, upendo siyo kufanya kile unachotaka, hapana. Hiyo ni aina ya uhuru bila sababu na bila mwelekeo na ambao ni uhuru mtupu, uhuru wa tamasha ambao siyo mzuri, papa ameeleza. Uhuru wa namna hiyo kwa hakika unaacha utupu wa ndani. Ni mara ngapi baada ya kuhisi silika, unagutuka kuwa na utupu wa ndani, wa kuwa umetumia tunu vibaya ya uhuru tulio nao, ya uzuri wa kuweza kuchagua wema kwa ajili yetu na kwa ajili ya wengine. Papa ameongeza kusema, uhuru wa kweli daima unatukomboa lakini tunapofanya yale ambayo tunataka na tusiyotaka lazima yatuache na utupu wa ndani. Ni uhuru kamili tu, wa kweli ambao unajikita ndani ya maisha ya kweli kila siku unao komboa.

Video fupi inayoonesha baadhi ya matukio ya katekesi

Katika barua nyingine ya kwanza kwa Wakorinto, Mtume Paulo anajibu yule ambaye ana mawazo potofu kuhusu uhuru. “Vitu vyote ni halali”; vyote ni halilia unaweza kufanya. Hapana Papa amesema, hilo  “ni wazo potofu, ndiyo lakini si vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; lakini si vitu vyote vijengavyo”. Paulo anajibu na kuongeza kwamba mtu asitafute faida yake binafsi,  bali ya mwenzake. (1 Kor 10,23-24). Hiyo ndiyo kanuni  ili kufunua kila uhuru wa kibinafsi. Hata kwa yule anayeshawishika kupunguza uhuru kwa ajili ya ladha zake tu, Paulo anapendekeza dharura ya upendo. Uhuru unaongozwa na upendo na ndiyo pekee ambao unafanya kuwa na uhuru kwa wengine na sisi binafsi; kwa wanaojua kusikiliza bila kulazimisha, ambao wanajua kupenda bila kuzalimishwa, wanaojua kujenga bila kuharibu, ambao hawanyonyi wengine kwa ajili ya mafao yao, kwa kuwatendea wema bila kuwatumia kwa mtumizi binafsi. Kwa hakika ikiwa uhuru siyo huduma, hilo ni zoezi. Ikiwa uhuru siyo huduma ya wema hauwezi kuzaa matunda. Kinyume chake, uhuru ambao unaongozwa na upendo unapelekwa kwa maskini, kwa kuwatambua katika nyuso zao, uso wa Yesu. Kwa maana hiyo huduma kwa wengine kwa upande wa Paulo akiwaandikia Wagalatia alisemea“tuwakumbuke maskini; nami neno na hilo nilikuwa na bidii kulifanya”. (Gal 2,10). Papa ameongeza kusema: “inashangaza sana hiyo baada ya mapambano ya kiitikadi kati ya Paulo na mitume wengine, walikubaliana, je waseme nini kwa mitume: Songa mbele na msisahau maskini, yaani kwamba kuhubiri  kwao kuwe ni kwa  uhuru katika huduma ya wengine na si kwa ajili yao binafsi na kufanya kile ambacho wanapenda”.

Papa akisalimia makundi mbali mbali yaliyofika kwenye katekesi yake
Papa akisalimia makundi mbali mbali yaliyofika kwenye katekesi yake

Papa Franciskoamesema jinsi ambavyo inatambuliwa kuhusu mantiki za kisasa zilizoenea kuhusu uhuru kwamba: “uhuru wangu unaishia mahali unapoanza wa kwako”, kwa mtazamo wake amesema hiyo ni kukosa uhusiano. Ni maoni ya kibinafsi. Kinyume chake aliyepokea zawadi ya ukombozi kutoka kwa Yesu hawezi kufikiria uhuru unaohusu kukaa mbali na watu wengine, kwa kuhisi ni usumbufu, ambaye hawezi kuona ubinadamu unaokaa peke yake bali ni uòe ambao unajumuishwa ndani ya jumuiya. Ukuu wa kijamii ni msingi kwa wakristo na ambao unaruhusu kutazama wema wa pamoja na siyo mafao ya binafsi.  Hasa katika kipindi hiki cha kihistoria, Papa amesisitiza kuwa kuna hataji la kugundua mantiki ya kijumuiya na siyo ya kibinafsi, ya uhuru. “Janga la sasa hasa limetufundisha kuwa tunahitaji mmoja na mwingine lakini haitoshi kujua hili, inahitaji kuchagua kila siku kwa dhati, njia ile ile. Tusema na kuamini kuwa wengine siyo kizingiti cha uhuru wangu, bali ni uwezekano wa kujikamilisha. Kwa maana uhuru wangu unazaliwa na upendo wa Mungu na unakuwa katika upendo”. Papa amehitimisha

20 October 2021, 16:29