Tafuta

2021.10.29 : Dibaji ya  Papa Francisko katika Ebook ya Laudato si' 2021.10.29 : Dibaji ya Papa Francisko katika Ebook ya Laudato si' 

Papa anatoa wito kutoka kilio cha ardhi na maskini ili kubadilisha mtindo wa maendeleo

Dibaji ya Papa katika e-book Laudato si Readre.An Alliance of Care for Our Common House",katika toleo la nyumba ya Vitabu Vatican(Lev)katika fursa ya COP26.Kitabu kitaweza kupakuliwa kuanzia 12 Novemba kwenye Tovuti ya Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu ambayo imehamasisha.Ni mkusanyikao wa tafakari ya Waraka wa Laudato si ulimwengu mzima.Kuna hata tafakari ya Katibu mkuu wa UN,António Guterres.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Miaka 6 iliyopita ulichapishwa ujumbe ulimwenguni wa Waraka wa Laudato si kuhusu utunzaji bora wa mazingira na kuufanya kwa njia ya mazungumzo ambayo yanawahusu wote na mazungumzo hayo yameweza kuwa chanya na kupata mwangwi wa kuufanyia kazi kati ya dini na jumuiya za kikanisa ulimwengu kote Kutokana na Waraka huo,  mipango mingi sana  imeweza kuanzishwa katika maeneo mengi, ya binadamu na shughuli za elimu kwa mujibu wa ikolojia na baionuai. Tafakari nyingi zimeendelezwa za watu na jumuiya ambazo kwa sasa zinaonekana hata katika kitabu cha Laudato si' "Reader.  An Alliance of Care for Our Common House", mshikamano wa kutunza nyumba yetu ya pamoja  ambacho kimechapishwa  nyumba ya duka la vitabu la Vatican (Lev) katika fursa ya kufanyika mkutano wa Cop26 unaohusu mabadiliko ya tabianchi huko Glasgow nchini Scotland.  Kitabu kipo katika mtindo wa e-book, ambacho kitaweza kupakuliwa bure kuanzia tarehe 12 Novemba 2021 kutoka katika Tovuti ya Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu ambalo limehamasisha uchapishwaji wake,; vile vile kutoka Tovuti ya Lev na kutoka katika Idhaa ya Kiingereza ya Vatican News. Kitabu hicho kinajumuishwa mchango wa wanaharakati wa mazingira, mabalozi, watu wakuu wa Kanisa na madhehebu tofauti ya kikristo. Wakati mfumo wa kitabu kamili cha karatasi kitapatikana kutoka kwenye Tovuti ya Duka la vitabu la Vatican: www.libreriaeditricevaticana.va

Katika dibaji ya kitabu hicho, Papa  ameandika kuwa “ ni hitimisho linalofaa la Mwaka Malum wa Laudato si’ ambao uliadhimishwa kuanzia tarehe 24 Mei 2020 hadi 24 Mei 2021. Katika maandishi yake Papa anatoa ufupi kwa kielelezo cha “kilio cha maskini na kilio cha ardhi” , matokeo magumu ya kushindwa kwetu katika kutunza nyumba yetu ya pamoja na ambayo imeongezwa na dharura ya UVIKO-19. Kwa upande wa Papa Francisko, Mgogoro ambao hadi sasa unakatisha ulimwenguni ni fursa kwa ajili ya kutambua na kujifunza makosa ya wakati uliopita. Mgogoro wa sasa unapaswa kutufanya kubadilisha mateso binafsi yaliyopo kwa sasa ulimwenguni na kwa namna ya kutambua ni mchango upi ambao kila mtu anaweza kuutoa (LS, n. 19).

Vile vile Papa anabaibisha kuwa ni kipindi kwetu sisi ambacho kinaweza kubadilisha mwenendo, kubadilisha tabia mbaya  na hatimaye kuwa na uwezo wa kuota  kuunda, kutenda kwa pamoja ili kutumiza wakati ujao wa haki na usawa. Ni wakati sasa wa kuendelea katoa mtindo mpya wa mshikamano wa ulimwengu ambao umejengwa juu ya udugu, ya upendo, uelewa wa pamoja; mshikamani ambao unathamanisha watu zaidi ya kupata faida, unaotafuta mitindo mipya inayoelewa kuendelea na maendeleo. Na kwa namna hii, tumaini langu, sala zangu ni kwamba tusitoke katika mgogogoro huu tukiwa tunafanana kama tulivyoingia! Ni wakati wa kutenda na kutenda kwa pamoja. Ni sasa! Anahitimisha Papa.

Guterres: ni lazima kuacha moto juu ya asili

Maandiko hayo ni sawa na jitihada za Umoja wa Mataifa kupitia kwa Katibu wa Umoja wa mataifa, Bwana António Guterres ameanzia hapo katika Utangulizi wa kitabu kwa kushuhudia na si tu muktadha binafsi na juu ya kazi za Mataifa wanachama katika yale yaliyomo kwenye Waraka wa Papa, wa matokeo mazuri tangu 2015 na kuendelea, lakini pia hata kuweza kuwasha watafakari juu ya majanga ya mazingira ambapo ulimwengu unapitia leo hii. Kutengeneza amani na maumbile ni lazima iwe ndiyo kipaumbele cha karne ya XXI. Kuanza kwa upya kwa janga umewea kuonesha jinsi ya  uwezekano wa kurudi nyuma katika giza. Katibu wa Umoja wa Matifa anazungumza kipimo cha kisiasa adili na hata majaribu ya maadili.  Kwa maana hiyo  Katibu mkuu anaonesha dharura nne na kuweka umakini juu ya ubinadamu: upunguzaji wa gasi ya kaboni hadi Zero kufikia 2050; msaada kwa wale ambao tayari wanakabiliana na matokeo mabaya ya mabadiliko ya tabianchi; mshikamano wa kifedha ulimwenguni katika jitihada za Mkataba wa Paris na Malengo ya Maendeleo Endelevu, na mwisho kusimamisha dharura kubwa ya kisayari. Huu ni wakati wa ukweli. Ikiwa tunabaki na mitindo ya kizamani ya ukosefu wa usawa, ukosefu wa haki, chuki, kutawala bila kutunza ardhi, tunakwenda kukutana na mabalaa”. Kwa kunukuu katika kifungu cha Waraka wa Fratelli Tutti, Katibu Mkuu ameandika kuwa “ dunia inahitaji kuongeza uhusiano wa mshikamano wa ulimwengu kwa ajili ya kujenga wakati ujao wa amani kwa ajili ya wote.

31 October 2021, 12:03