Tafuta

Papa na Askofu Mkuu Bartolomeo Patriaki wa Costantinopoli Papa na Askofu Mkuu Bartolomeo Patriaki wa Costantinopoli 

Barua ya Papa kwa Patriaki Bartolomeo I kufikisha miaka 30 ya uaskofu Mkuu

Papa Francisko ametuma barua kwa Patriaki wa kiekumene Bartolomeo I katika fursa kutimiza miaka 30 tangu achaguliwe kama Askofu Mkuu wa Constantinopoli na Patriaki wa Kiekumeni. Katika barua hiyo amegusia urafiki wao muhimu ulioanza tangu achaguliwe kuwa papa na kukuzwa wakati wa mikutano mbali mbali Roma na nje ya Roma.Anamshukuru kwa jitihada za kutunza mazingira pia mchango mchakato kuelekea umoja wa makanisa.

Na Sr. Amgela Rwezaula - Vatican

Ijumaa tarehe 21 Oktoba 2021, Baba Mtakatifu Francisko amemtumia Askofu Mkuu wa Constantipoli, Bartolomeo I, Patriaki wa Kiekumene. Katika barua hiyo ameanza na neno la Mungu: “Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja” (Uf 1,4). Papa anaonesha furaha katika fursa ya kutimiza miaka 30 tangu kuchaguliwa kuwa Askofu Mkuu wa Costantinopoli na Patriaki wa kiekumene na kumtakia heri kwa shauku: Χρόνια πολλά! Ad multos annos! Papa anaungana naye katika kumshukuru Bwana kwa ajili ya baraka nyingi alizomshushia kwa ajili ya  maisha yake na juu ya huduma yake kwa miaka hii na anasali kwa Mungu ambaye zawadi zote zinatoka kwake ili amjalie afya, furaha kiroho na neema nyingi ya kumsaidia kwa kila mantiki ya huduma yake kuu.

Uhusiano ulio kuwa kwa njia mbali mbali za mikutano

Papa anasema ni shukrani kwa Mungu anapotafakari juu ya uhusiano wa kina binafsi, ambao ulinzishwa kwa kipindi sasa, hasa  tangu siku ya kuanza kwa upapa wake, wakati alipofurahia uwepo wake Roma. Na kwa kadiri ya siku zilikwenda mbele, uhusiano huo umekuwa urafiki kidugu na kuongezeka wakati wa mikutano mengi, ambayo si Roma tu lakini hata huko Phanar, Yerusalemu, Asisisi, Cairo, Lesvos, Bari na Budapest. Papa Francisko aidha ameandika kuwa  na kama ilivyojionesha wazi tena kwa mara nyingine tena kwa ushiriki kwake katika matukio yaliyofanyika hivi karibuni Roma, mahali ambapo uwepo wake ulikuwa kwa nama ya pekee kupongezwa, Papa anashirikisha naye uelewa wa wajibikaji wa pamoja kichungaji mbele ya changamoto za dharura ambazo familia nzima ya kibinadamu hadi leo inaendelea kikabiliana nayo.

Shukrano kwa jitihada za ulinzi wa mazingira na njia ya mazungumzo ili kufikia umoja kamili

Kwa namna ya pekee, Papa amemwakikishia kuunga mkono juhudi  zake za ulinzi wa kazi ya uumbaji na kwa tafakatari yake juu ya mada ambayo yeye mwenyewe amejifunza na anaendelea kijifunza zaidi. Kwa kuibuka janga na matokeo yake magumu ya kiafya, kijamii na kiuchumi, ushuhuda wake na mafundisho yake juu ya ulazima wa uongofu kiroho wa ubinadamu, umepata umuhimu wake wa kudumu.  Na zaidi Baba Mtakatifu Francisko anamshukuru kwa dhati kwa ajili ya kuelekeza bila kuchoka njia ya mazungumzo, ya upendo na katika ukweli, kama njia pekee zinazoweze kufanya kufika upatanisho kati ya waamini katika Kristo na ili kurudisha umoja wao kamili. Kwa msaada wa Mungu hiyo ndiyo njia na  ndefu ambayo itaendelezwa kupitia kwa uhakika wa kutembea pamoja, kwa sababu ukaribu na mshikamano kati ya Makanisa , ni mchango muhimu wa udugu wa kibinadamu na haki kijamii, ambamo ni dharura ya mahitaji ya ubinadamu. Kwa hisia za udugu wa kina, Papa Francisko amemtumia salamu na mkumbatia wa kidugu katika upendo wa Bwana Yesu Kristo.

BARUA YA PAPA KWA PATRIAKI BARTOLOMEO I
22 October 2021, 15:54