Tafuta

2021.09.09:Papa Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Wamisionari wanawa moyo safi wa Maria (Claretian) 2021.09.09:Papa Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Wamisionari wanawa moyo safi wa Maria (Claretian) 

Papa:Shauku ya Injili &washa upendo wa Mungu kwa watu

Papa Francisko amekutana jijini Vatican na washiriki wa Mkutano mkuu wa Shirika la Wamisionati wa Wana wa Moyo safi wa Bikira maria,(Claretian).Katika hotuba ametoa onyo kwa watawa kutoendana na mantiki za kiulimwengu ili wasipoteza mwelekeo wa maisha yao na chaguo za kimisioanari.Hawezi kuishi na roho za kiulimwengu na kujidai kuhudumia Bwana.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko amekutana Alhamisi tarehe 9 Septemba mjini Vatican amekutana na na washiriki wa Mkutano mkuu wa Wamisionari wa Moyo safi wa Bikira Maria wajuliakanao (Waklaretiani. Papa Francisko akianza hotuba yake ameonesha furaha yake ya kukutana na washiriki hao wa kimisionari waliotoka katika ulimwengu mzima wakiwakilisha wanashirika elfu tatu wanaounda Tasisi yao ya kimisionari. Anawashukuru kufika kukutana na Papa na pia Kardinali Aquilino Bocos Merino kwa uwepo wake. Amempongeza Padre Mathew Vattamattam ambaye amechaguliwa tena katika mkutano huo, kuwa Mkuu wa shirika tena na ndugu wote waliochaguliwa kuunda Baraza kuu la Taasisi ya kitawa. Na Roho Bwana awe nao kila wakati katika kutangaza Habari njmea kwa maskini(rej. Lk 4, 19) na kwa wale ambao wanajaa ya Neno la Mungu linalookoa (Is 55, 10-11). 

Mada iliyochaguliwa kuongoza mkutano huo Papa amesema  ni kusimika mzizi ndani ya Yesu kwa shauku. Kwa maana hiyo amesema kwamba hii inawataka wawe  na maisha ya sala na kutafakari kwa kina ili kufikia kusema kama Ayubu “Nilikujua kwa kusikia, lakini sasa macho yangu yanakuona” (Ay 42, 5). Maisha ya sala na tafakari ya kina ambayo yanawawaruhusu kuzungumza, kama rafiki uso kwa uso na Bwana. (Kut 33, 11). Maisha ya sala na kutafakari ambayo yanawaruhuhsu kutafakari katika kioo kuwa ni Kristo ili hata nao pia kugeuka kuwa  kama kioo kwa wengine. Papa Francisko ameeongeza kusema kwamba wao ni wamisionari, na ikiwa wanataka utume wao uwe wa kweli wenye matunda hawawezi kutengenisha utume na tafakari ya kina na maisha ambayo ni ya undani na Bwana. Ikiwa wanataka kushuhudia hawawezi kuacha kuwa waabuduo. Shuhuda na kuadudu ni mambo mawili ambayo yanakutana katika moyo wa Injili. Aliwaita ili wawe pamoja na baadaye  kuwatuma kuhubiri ( Mk 3,4). Ni dhamana mbili ambazo zinafanana pamoja na ambazo haziwezi kuishi kipekee bila mwenzake, Papa amesisitiza.

“Mtoto wa Moyo safi wa Maria ni mtu ambaye anawaka upendo na mahali popote anapopita anawaka, kwa mujibu wa kanuni yao kuu ya Claret (n 9). Papa Francisko amewashauri waachie nao wachomwe na Bwana, upendo wake kwa namna ya kwamba wanaweza kuunguza kila mahali wanapopita, na moto wa upendo wa Mungu. Na huo ndiyo uwe uhakika pekee wa usalama wao. Huo utawaruhusu kuwa watu wa matumaini, matuma ambayo hayakatishi tamaa (Rm 5,5), wa matumaini ambayo hayajuhi hofu, kwa sababu inatambulika kuwa ni “katika udhaifu ndipo kuna nguvu ya Mungu” ( rej. 2 Kor 12,9). Kwa kunukuu tena katika kanuni ya ya shirika lao, Papa Francisko amewashauri kuw “msiache kuogopeshwa na lolote lile. Msiwe na hofu ya udhaifu wenu; msiogope, hasa kwa kuangukia katika anguko la kiroho na roho ya dunia, ambayo mnaweza kuwapatiwa na wapendwa wenu na ngamia zenu, nguvu zenu, na kujiamini kuwa walio bora, kwa kutafuta kwa udi na uvumba ustawi binafsi na madaraka”( Evangelii gaudium, n. 93).

Papa Francisko ametoa onyo kwa watawa hao la kutoendana na mantiki za kiulimwengu ambazo zitafanya Injili ya Yesu isiwe mwelekeo wa maisha yao na chaguo za kimisioanri. Wao hawezi kuishi na roho za kiulimwengu na kujidai kuhudumia Bwana. Walekeze maisha ya katika thamani ya Injili. Wasitumue Injili kuwa zana binafsi, kama itikadi, na badala yake iwe kama Vademecum yaani mwongozo, wa kuwaelekeza  kila wakati na chaguzi za Injili na shauku kubwa ya kumfuata Yesuna kumwiga katika sala na ugumu, kwa kutafuta daima utukufu wa Mungi tu na wokovu wa roho. (Padre Claret). Papa amewaomba waweke maisha yao katika Kristo kwa namna ya kuweza kusema na Paulo: “si mimi ninaishi bali Kristo anaishi ndani mwangu” ( Gal 2,20). Mwelekeo huu utawafanya wawe na ujasiri katika utume wao  kwani ujasiri ulikuwa utume wa Padre Claret na wamisionari wa kwanza waliojiunga naye. Maisha yaliyowekwa wakfu yanahitaji ujasiri na yanahitaji watu wazee ambao wanapinga kuzeeka kwa maisha na vijana ambao wanapinga kuzeeka kwa roho.

Kusadikika huku kutawezesha kutoka nje, ili kujikita katika safari na kwenda mahali ambapo hakuna mtu anataka kwenda, ambapo nuru ya Injili inahitajika, na kufanya kazi bega kwa bega na watu. Utume wao hauwezi kuwa wa mbali, bali wa ukaribu na kukaribiana. Katika utume hauwezi kufurahiwa na kukaa barazani na  kuchungulia kupitia dirishani, kwa kuchunguza tokea mbali. Inawezekana kwenda kwenye ubaraza wa hali halisi na jitihada ya kubadilisha. Ushiriki wo ni  kwa ajili ya kubadili hali halisi ya dhambi ambayo watakutana nayo katika safari, Papa amefafanua. Wasiwe na sintofahamu mbele ya majanga ambayo wengi wanaishi nyakati hizi, badala yake wafanye jitihada katika kupambania hadhi ya binadamu, na heshima kwa ajili ya haki msingi za binadamu. Papa ameomba waache waguswe na Neno la Mungu na ishara za nyakati, na kwa njia ya Mwanga wa Neno na ishara za nyakati zitawasaidia  kusoma tena historia yao, karama yao, kwa kukumbuka kuwa maisha ya kitawa ni kama maji, ikiwa hayatiririki yanachafuka. Kwa kufanya kumbu kumbu ya kutoka katika wakati uliopita, na kuwa  kiini cha karama. Hayo yote yatawafanya kuwa na maisha ya kinabii na ambayo yatawawezeka kuwa makini katika akukesha na kungazia ulimwengu. Papa Francisko amesema: “Neno na ishara za nyakati zitutikise kutoka katika vuguvu  nyingi na kutoka katika hofu nyingi ambazo ikiwa hatuko waangalifu, zinatuzuia kufikia nyakati na hali ambazo zinahitaji maisha ya wakfu yenye shauku na  ujasiri wa maisha ya kitwa yaliyo huru,  yalikuombolewa dhidi ya hatari zetu”.

Ni matarajio ya Papa Francisko kuwa mkutano wao mkuu ambao unaokaribia kumalizika uwasaidie kujikita kwa ndani yaliyo ya msingi kwani : Yesu awe ndiyo kiini cha  usalama wao, na katika Yeye peke yake na katika Yeye ndiye aliye wema wa yote, usalama wa ukweli. Hii inaweza kuwa moja ya matunda bora katika kipindi hiki cha janga ambacho kimeleta mjadala mkubwa kwa kuonesha uongo mwingi tulio nao kuhusu usalama”. Ni matarajio ya Papa kuwa Mkutano huu umewafanya kutazama mambo msingi ambayo yanafafanua maisha yao ya kila siki kwa walio na wakfu, ambao unathamanisha mahusiano na Mungu; maisha ya udugu katika jumuiya, kipaumbele cha uhusiano wa kweli na ndugu; na utume ambao uwapelekee kutoka nje kwenda kukutana na wengine kwa namna ya pekee maskini na  kuwapeleka kwa Yesu. Papa amekumbuka kabla ya kumalizia kuwashukuru kwa kazi ya kitume ambayo wanafanya na tafakari yote kuhusu maisha ya kitawa wanayoishi ambayo wameweza kuipeleka mbele kwa miaka hii. Amewaomba watende vema na Roho mtakatifu awaongoza katika kazi hiyo msingi. Kwa kuhitimisha amewabariki kwa Baraka ya kitume familia yote ya Waklaretiani, na wasisahau kusali kwa ajili yake.

HOTUBA YA PAPA KWA WAKLARETIAN
09 September 2021, 16:41