Tafuta

Papa ametoa wito kwa Ethiopia kwa ajili ya mshikamano

Papa ametoa wito kwa Ethiopia kwa ajili ya mshikamano kufuatia na vurugu, ameombea ndoto ya Wacuba,sambambana na kukumbuka siku kuu ya Bikira Maria,juu ya mwenyeheri Kardinali Wyszyński nchini Poland na kuwaomba vijana wajifunze kuboresha ulimwengu.Hayo ni mara baada ya katekesi katika ukumbi wa Paulo VI,Jumatano 8 Septemba.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ufafanuzi ni mfupi, ambao ni  hali mbaya ya kibinadamu, lakini ndani kuna ulimwengu wa ukatili na moyo wa huzuni wa Papa. Kwa baadhi ya wachambuzi wanasema kuwa, kinachotokea nchini Ethiopia ni kutengana kwa nchi, vita vya mauaji kati ya wanajeshi hadi wanamgambo wa Chama maarufu cha Ukombozi wa Tigray, ambacho kinalenga Addis Ababa. Vile vile katikati, kuna habari za mauaji, ubakaji, udhalilishaji, vurugu nyingi ambazo zinamfanya afikirie sana Papa Francisko hadi kufikia leo hii kusema kuwa: “Mwaka Mpya utaadhimishwa tarehe 11 Septemba nchini Ethiopia. Ninatoa salamu kwa upendo kwa watu wa Ethiopia, hasa kwa wale ambao wanakabiliwa na mzozo unaoendelea na hali mbaya ya kibinadamu ambayo imesababishwa. Na uwe wakati wa kufanya udugu na mshikamano ambao tunaweza kusikiliza hamu ya amani”.

Ninaombea  ndoto ya Wacuba

Wito umefunga salamu kwa vikundi mbali mbali  vya lugha,ambapo Papa Francisko kwa njia katika salamu hizo kwanza aemekumbuka sikukuu ya leo ambayo Mama Kanisa anaadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Maria. Na kwa ajili ya siku kuu ya Bikira, wa upendo huko Cobre, ambaye ni msimamizi wa Cuba, pia ni wazo ambalo Papa Francisko amehitimisha katika katekesi iliyofanyika kwa lugha ya  kihispania. Kumbukumbu ya shukrani ni ya miaka sita iliyopita, alipotembelea madhabahu ya Bikira Maria  kisiwa cha Caribbean mnamo Septemba 2015. Hija ambayo ambayo Wacuba wanakumbuka Mama yao imesukuma hata Papa Francisko awambie kwamba wawasilisha ndoto zao, matumaini na maumivu ya watu wa Cuba katika miguu yake mama Maria. Popote pale alipo mcuba leo hii Papa amesema kwamba aweze kufanya uzoefu wa upole wa Maria na awaongoze wote kwa Kristo, Mwokozi.

Wyszyński, shujaa wa matumaini

Papa Francisko pia ametoa salamu maalum kwa waamini wa Kipoland. Jumapili ijayo baada ya zaidi ya mwaka mmoja kwa sababu ya janga lililolazimisha kuahirishwa, hatimaye Kardinali Stefan Wyszyński atainulia katika altare kuwa mwenyeheri ambapo Papa amependa  kunukuu maneno ya kihistoria yaliyotamkwa siku moja na Mtakatifu Yohane Paulo II: “Juu ya kiti cha Petro pasingekuwapo na Papa huyo ya kipoland kama isingekuwa imani yako, ambayo haikupungua mbele ya kuwa gerezani na mateso, tumaini lako la kishujaa, imani yako kamili kwa Mama wa Kanisa. Nawe agano la kiroho la Milenia kwa maana hiyo ninaweka kila kitu kwa Maria na ujasiri wa mama Elizabeth Rosa Czacka", Papa amepngeza kusema kuwa " hii inaweza kuwa nguvu ya taifa lenu kila wakati".

Vijana, jifunzeni kuboresha ulimwengu

Papa Francisko  hakusahau ulimwengu wa wanafunzi ambao wako karibu kurudi shuleni. "Vijana wapendwa mwaka huu wa masomo uwe fursa kwenu nyote kukua kiutamaduni na kuimarisha uhusiano wa urafik. Hata hivyo alikuwa pia amesema: "Ninyi watoto na  vijana, wanafunzi na walimu ambao mnarudi shuleni siku hizi, Bwana awasaidie kuhifadhi imani na kukuza sayansi, kuwa wahusika wakuu wa siku bora zijazo, ambazo ubinadamu unaweza kufurahia amani, udugu na utulivu".

08 September 2021, 16:39