Tafuta

Papa ameombea Afghanistan:Nchi zipokee wanaotafuta maisha mapya

Mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana,Dominika Septemba 5,Papa Francisko amewaombea watu wa Afghanistan ambao wamebaki ndani na wale ambao wanaondoka na ambao tayari wamekwisha fika katika chi za makaribisho.Kwa wote waweze kupapa msaada na ulinzi wanaohitaji.

Na Sr. Angela rwezaula – Vatican.

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana Dominika tarehe 5 Septemba 2021, Papa Francisko ameinua moyo wake kwa Mungu kumbabidhi watu wa Afghanistan, ambao ulimwengu unaonekana kuwa na wasiwasi mkubwa: “Katika nyakati hizi zenye msukosuko, ambazo zinawaona Waafghanistan wakitafuta kimbilio, ninawaombea wanyonge zaidi kati yao; Ninaomba kwamba nchi nyingi ziwakaribishe na kuwalinda wale wanaotafuta maisha mapya ”. Aidha Papa amesema kuwa: “Ninawaombea pia wakimbizi wa ndani, ili wapate msaada na ulinzi wanaohitaji. Vijana wa Afghanistan wapate elimu, mali muhimu kwa ajili ya  maendeleo fungamani ya binadamu, na Waafghani wote waweze, wale walio  nyumbani, walio katika usafiri  au katika nchi za wenyeji zinazowakaribisha, waishi kwa hadhi, kwa amani katika udugu na majirani zao”.

Hata hivyo taarifa inabainisha jinsi ambavyo hofu inazidi kukua huko Panshir, eneo pekee la Afghanistan ambalo halijawa chini ya udhibiti wa Wataliban hata ikiwa wanaendelea na mapigano ya wao kwa wao. Makamu wa Rais wa zamani wa Afghanistan Saleh alithibitisha kuwa: “mzozo mkubwa wa kibinadamu unaendelea, kwa sababu ya kuzuiwa kwa uchumi na kukatika kwa umeme na mawasiliano ya simu uliotekelezwa na Wataliban”. Katika taarifa hiyo, Saleh ametoa wito kwa ajili ya watu elfu 250 waliohamishwa na ambao wanaishi katika makazi ya muda, misikiti, nje au katika vituo vya afya ambavyo sasa vimezidi uwezo wao. Anasema kuwa “Tunahitaji chakula, malazi, vifaa vya maji na usafi".

Maombi kwa ajili ya Marekani iliyokumbwa na kimbunga

Papa Francisko pia amegeuza mtazamo wake na sala zake kwa watu wa Marekani waliokumbwa na kimbunga kikali katika siku za hivi karibuni. Papa amesema:“Bwana apokee roho za marehemu na kuwasaidia wale wanaoomboleza kwa  ajili ya msiba huo”. Kwa mujibu wa na jarida la hivi karibuni, linataja kuwa idadi ya waathiriwa wa kupitiwa Kimbunga Ida, ambacho kiligonga Louisiana, New Jersey na New York hasa, imeongezeka na kufika idadi yawaathiriwa  60.

TAFAKARI YA PAPA DOMINIKA

 

05 September 2021, 13:44