Tafuta

2021.09.06 Papa akutana na wakimbizi na watu wasio na makazi mara baada ya kutazama filamu"Francesco" 2021.09.06 Papa akutana na wakimbizi na watu wasio na makazi mara baada ya kutazama filamu"Francesco" 

Maneno ya Papa Francisko kwa wakimbizi na wasio na makazi maalum

Ilikuwa ni furaha isiyo na kifani jioni ya Jumatatu tarehe 6 Septemba katika uwanja wa Paulo VI Vatican,mahalia ambapo Papa Francisko amefika na kusalimiana na watu karibu 100,wasio kuwa na makazi maalum na wakimbizi waliolikwa kutazama filamu ya dokumentari iitwayo ‘Francesco’.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Zaidi ya watu 100 hivi wasio kuwa na makazi maalum na wakimbizi wameweza kutazama filamu moja ya dokumentari  iitawayo ‘Francesco’, Jumatatu tarehe 6 Septemba 2021 katika ukumbi mpya wa Sinodi wa Paulo VI mjini Vatican, ambamo miongoni mwake walikuwapo familia mbili za wakimbizi kutoka Afghanistan ambao wamefika hivi karibuni kutoka Kabul.  Tukio hili liliandaliwa na Mfuko wa Laudato sì mtayarishaji wa filamu Evgeny Afineevsky, ambaye ameweza kuwasalimia binafsi watu wote akiwakumbusha historia ya uhamishoni  kwa familia yake mwenyewe, ambaye asili yake ni kutoka Urusi na baadaye waliahamia nchini Israeli na hatimaye wakahamia tena nchini Marekani.

Uoneshaji wa filamu hiyo umefanyika katika hali ya hisia ya nguvu kwa watu waliokuwapo ambao kwa hakika wanaishi uzoefu huo wa janga, kwa ziadi ya watu 30 waathiriwa wa vita, dharura za mazingira na mateso. Hisia ya nguvu katika filamu hiyo hata hivyo iliyeyuka baada ya kusikia  maneno ya Papa Francisko ambaye amependa kuzungumza na wakimbizi hao katika uwanja mbele ya ukumbi wa  Paulo VI.

Papa Francisko
Papa Francisko

Katika hali ya kawaida na ya upendo wa kila mmoja, kila kundi la familia, ameweza kupokea maneno ya kutiwa nguvu na Papa mwenyewe moja kwa moja, kati ya mshangao hasa kwa wale watoto wadogo ambao wamejikuta wakiwa ,mbele na yule aliyekuwa mstari mbele katika filamu kwa dakika chache kabla ya kuwa katika uwanja huo. Wakati muhimu na wakina ulikuwa ni wa kukutana na wakimbizi 20 kutoka Afghanistan waliokimbia hivi karibuni na mgogoro mkubwa wa Uwanja wa Ndege wa Kabul.

Kwa mujibu wa msemaji wa vyombo vya habari Vatican kwa waandishi Dk. Matteo Bruni amesema: “leo jioni baada ya filamu ya ‘Francesco’, iliyotayarishwa na mkurugenzi wa filamu  kwa kushirikiana na  Mfuko wa Laudato Si, Baba Mtakatifu Francisko amefika kwenye uwanja wa Paulo VI na kukaa kidogo na watu karibia 100 wasio kuwa na nyumba na wakimbizi ambao walialikwa kutazama filamu hiyo. Miongoni mwao walikuwapo watu ishirini waliofika kutika Afghanistan katika wiki za mwisho, ambapo Papa amewaelekea kwa maneno ya upendo na kuwatia moyo. Kwa maana hiyo baadaye Papa amerudi nyumbani kwake Mtakatifu Marta na waandaaji wakawagawia watu hao vyakula vya kupeleka nyumbani”, alisema Dk Bruni.

Papa Francisko akisalimiana na watu waliotazama filamu 'Francesco'
Papa Francisko akisalimiana na watu waliotazama filamu 'Francesco'

Hata hivyo kuhusiana na wakimbizi kutoka Afghanistan, miongoni mwao kulikuwa na  kaka na dada wenye umri kati ya 20 na 14 waliofika Italia, shukrani kwa msaada wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio. Pamoja na kukabidhiwa vijana hao kwa mjomba wao ambaye alifika Italia miaka kadhaa,  wameacha wazazi wao waliobaki wamefungwa katika makambi ya wakimbizi nchini Iran. Bismillah, ndiye mkubwa kati yao ambaye ametoa ushuhuda kwa Vatican News juu ya umuhimu wa kuhisi kukaribishwa, kusikilizwa na kueleweka kwa Papa Francisko na jinsi ambavyo uwepo wake kwa siku hiyo jioni, umekuwa muhimu sana kwa kuashiria matumaini mapya ya kuweza kukabiliana na wakati ujao. Baada ya mkutano na wakimbizi hali ilikuwa ya siku kuu na furaha kubwa ambayo wao walifika hadi wanakutana na Papa Francisko aliyekuwa akiwasubiri nje ya ukumbi wa Paulo VI na baadaye kurudi nyumbani Mtakatifu Marta.

07 September 2021, 12:08