Hija ya Kitume ya Papa Francisko Budapest:mapokezi ya shangwe
Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.
Habari katika picha: Papa ameondokea katika Uwanja wa ndege wa Fiumicino baada ya kufkia kwa gari kutoka katika nyumba ya mtakatifu Marta.Hii ni ziara yake ya kitume ya 34 ya upapa wake.
Itakuwa ni siku tano kati ya nchi ya Hungaria na Slovakia itakayo kuwa na matukio awali ya yote kuabudu na sala katika moyo wa Ulaya na pia nia ya pili ya Papa ni kumkabidhi maombi kwa mashujaa wengi wa imani ambao nchini Hungaira na Sloavkaia wameshuhudia Injili ndani ya vizingiti na mateso. Habari katika video na picha zinaonesha mapokezi hayo mara baada ya kufika Budapest, maandamano na kuanza Ibada ya Misa Takatifu. Ndugu msomaji na msikilizaji wa Vatican News, endelea kufuatilia Ziara ya Kipapa nchini Hungaria na Slovakia 12-15 Septemba 2021.