Tafuta

Papa awakaribisha watoto na vijana wa msafara wa ukarimu katika Uwanja wa Mtakatifu Damasi,Vatican. Papa awakaribisha watoto na vijana wa msafara wa ukarimu katika Uwanja wa Mtakatifu Damasi,Vatican. 

Francisko awakumbatia watoto wa msafara wa ukarimu

Katika Uwanja wa Mtakatifu Damasi Vatican ulikuwa na washiriki wapatao mia moja katika mpango unaohusishwa na Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi ijayo. Papa amewaalika kucheza na kuwabariki.Hapo awali walikuwa wamesimama katika Uwanja wa Mtakatifu Petro ambapo kulikuwa na samau ya Amal,ishara ya wakimbizi wanaotafuta nchi mpya.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko akiwa katika harakati za kujiandalia na safari ya kwenda Budpest na Sloavakia, Ijumaa asubuhi tarehe 10 Septemba 2021, amewahutubia na kutoa salamu fupi ya upendo kwa watoto zaidi ya miaka moja na vijana wa parokia nyingine za jimbo la Roma, skauti na na Caritas ya Roma, walioshiriki katika maandamano ya 'Kukaribisha' yaliyoongozwa na mada ya "Fungua", yaliyoandaliwa kwa ajili ya tukio la Siku ya wahamiaji na mkimbizi mwishoni mwa mwezi huu nkatika uwanja wa Mtakatifu Damasi ndani ya Jiji la Vatican. Pamoja nao pia ulikuwapo uwakilishi wa shirika la Wascalabrini ambao wanajikita kwa kiasi kikubwa na shughuli za ukimbizi, pamoja na Kardinali Michael Czerny, katibu mkuu msaidizi kitengo cha Wahamiaji na Wakimbizi cha Baraza la Kipapa la Maendeleo fungamani ya Binadamu, na Askofu Benoni Ambarus, askofu msaidizi mwenye jukumu la  kichungaji kwa ajili ya Wahamiaji, warom na Wasinti katika jimbo la Roma.

SANAMU YA AMAL MBELE YA SANAMU KUBWA YA UHAMIAJI KATIKA UWANJA WA MTAKATIFU PETRO
SANAMU YA AMAL MBELE YA SANAMU KUBWA YA UHAMIAJI KATIKA UWANJA WA MTAKATIFU PETRO

Michezo katika Uwanja wa Mtakatifu Damasi, Vatican

Mara baada ya kufika katika uwanja wa Mtakatifu Petro na kutazama tamasha la "The Walk" yaani kutemba, ambali lilianzia mpakani mwa Uturuki na Siria kuelekea huko Manchester, na mabacho ni kichwan cha sanamu ya Amal, kikiwakilisha mtoto mkimbizi. Walismama katika uwanja wa Mtakatifu Petro na baadaye wakaenda kwenye Uwanja wa Mtakatifu Damasi, mahali ambapo wameimba, wamecheza na kushiriki sala ya Malaika wa Bwana, saa sita kamili. Kwenye saa sita na roba, Papa Francisko alifika na kwa haraka akazungukwa na watoto na vijana ambapo Papa alibaki nao akawaalika wakae katika Uwanja huo ili walicheze na wakati huo huo akawabariki na kuwaomba nao wasiahau kusali kwa ajili yake.

WATOTO WAKIMZUNGUKA BABA MTAKATIFU
WATOTO WAKIMZUNGUKA BABA MTAKATIFU

Kichwa cha sanamu ya Amal ni ishara ya watotot wakimbizi ulimwenguni

Kichwa cha sanamu ya Amal kinawakilisha mtoto wa miaka 9 na ni ishara ya janga la mamilioni ya watoto ulimwenguni katika ukimbizi wa vita na ambao wanatafuta kukaribishwa. Tangu tarehe 7 Septemba,  sanamu hiyo imafanya vituo mbali mbali vya miji ya Italia, baada ya kutoka Uingereza. Katika mji wa Roma imesimama hata Vatican, kwa kukaribishwa na Askofu msaidizi, Benoni Ambarus na kardinali Czerny. Ijumaa tarehe 10 Septemba kisananu hicho cha urefu wa mita tatu na nusu kiliwekwa karibu na mnara  wa Angels Unawares, ambao ni mchongo wa sanamu ya mtumbwi uliojaa wahamiaji, iliyozinduliwa miaka miwili iliyopita ikiwakilisha hali halisi ya uhamiaji ulimwenguni. Kichwa cha Amal kinawakilisha mtoto mmoja wa kike mkimbizi aliyeanza safari tarehe 27 Julai mwaka huu huko Gaziantep, karibu na mpaka wa Uturuki na Siria, anazunguka Ulaya kama wazo la kuwakilisha mtoto anayetafuta mama na ulazima wa kutafuta mtu au familia iliyo karimu, ili hasiweze kuzima ndoto yake ubunifu na utashi wa amani ambao kwa kawaida ndiyo asili ya watoto wadogo.

SANAMU YA AMAL IKIZUNGUSHWA ROMA
SANAMU YA AMAL IKIZUNGUSHWA ROMA

Katika hotuba ya Kardinali Czerny kwa wanamsafara hao alisema kawamba  kama inavyosomeka katika sura ya kumi na nane ya Kitabu cha Mwanzo( Mw: 18)  jinsi walivyo mtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana akawakaribisha watu watatu kwa ukarimu na baadaye wakajionesha kuwa wametumwa na Mungu. Kwa maana hiyo amesema tujifunze kuwa kutoa ukarimu kwa watu wasio tarajiwa na wasio julikana, pia ukarimu inafunga uwezekanao wa kukutana na Mungu.  Wageni watatu kwa upande wao, wanakwenda kwa Ibarahimu na Sara kuwapa tangazao la mtoto. Wao ni watangazaji wa habari njema zisizotarajiwa, ambazo hutoa mtazamo mpya juu ya siku zijazo, ahadi ya kitu ambacho Ibrahimu na Sara walitamani na sasa bado wanaamini haiwezekani.

Kama kifungu hiki maarufu cha kibiblia kinatufundisha, ule ukarimu, kwa maana hiyo kinatengeneza maisha. Utamaduni wa kukutana, kama vile Baba Mtakatifu Francisko anavyosema, ni ishara ya changamoto na sio rahisi kila wakati!  Lakini ambayo inaruhusu jamuiya kukua kwa uangalifu kama familia ya wanadamu, katika nyumba yetu ya pamoja. Mpendwa Amal, unaweza kupumzika katika hema, hakika, lakini hivi karibuni utaendelea na safari yako. Kila mmoja wetu, kaka na dada wote wako njiani, Kanisa liko njiani na upyaisho wake unapitia mabadiliko ya kila mmoja, kuoneesha kwamba yuko hai.

SANAMU YA AMAL IKIZUNGUSHWA ROMA
SANAMU YA AMAL IKIZUNGUSHWA ROMA

Ukarimu hubadilika, kama inavyoshuhudiwa na jumuiya na familia nyingi ambazo zimewatunza wageni, hasa wale wanaowatunza watoto walioondolewa kutoka katika familia zao, kutoka jumuiya zao, kutoka katik matarajio yao, ambao wanapaswa kutegemea watu wasio wajua wenye mapenzi  ili kuwalinda na ambao Mungu alitaka wawe na kuchukua nafasi yao stahiki katika jumuiya zinazowakaribisha. Ujumuishaji ni mchakato wa pande mbili, na utambuzi wa pamoja na haki na wajibu, pia ni njia ngumu, wakati mwingine yenye ugumu, lakini ambao lengo lao lazima liwe la kufanikiwa kwa maendeleo ya kibinadamu ya wageni na vile vile wale wanaokaribisha, hasa walio hatarini zaidi kati yao.

KARDINALI CZERNY
KARDINALI CZERNY

Ikumbukwe kuwa 'Siku ya 107 ya Wahamiaji na Wakimbizi Duniani' itaadhimishwa ulimwenguni kote Jumapili tarehe 26 Septemba. Baba Mtakatifu alitoa ujumbe wake kwa ajili yao kwa kuongozwa na mada hii: Kuelekeza upamoja ulio mpana zaidi” yaani shirikishi utasaidia kufanya upya familia ya wanadamu, kujenga mustakabali wa haki na amani na kuhakikisha kuwa hakuna anayeachwa nyuma. Kwa maana hiyo ni kutaka kuonesha upeo wazi kwa safari yetu ya pamoja katika ulimwengu huu. Kiukweli Papa anasisitiza, kuwa sisi sote tuko katika mashua moja na tumeitwa kujitoa ili kusiwe na kuta tena zinazotutenganisha, hakuna wengine tena, lakini ni wamoja tu ambayo ndiyo iliyo kubwa kama wanadamu wote.

11 September 2021, 12:15