Tafuta

2021.08.28 Mkutano wa Papa na Kikundi cha Chama cha  "Lazare" 2021.08.28 Mkutano wa Papa na Kikundi cha Chama cha "Lazare" 

Papa:nendeni pembezoni penye njaa ya upweke na majeraha

Papa akikutana na Chama cha 'Lazare',kikundi cha upendo kwa maskini na wasio na nyumba kutoka Ufaransa katika fursa ya kuadhimisha miaka kumi tangu kuanza kwake amewakabidhi hotuba aliyokuwa ameandaa na akazungumza yaliyotokana na ushuhuda wao akiwakumbusha kuwa katika mazingira yamejaa sintofahamu,ubinafsi na utofauti lakini wao wanonwsha thamani za maisha ni ya dhati zinazopatikana katika kukarimu,kukaribisha na kuheshimu hadhi ya binadamu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko Jumamosi tarehe 28 Agosti 2021 akikutana na Wajumbe wa Chama cha ‘Lazare’, ambao ni muhimili wa shirika la upendo kwa ajili ya maskini na wasio  na nyumba kutoka Ufansa wakiwa katika fursa ya kuadhimisha miaka kumi tangu kuanza kwa chama hiki, ambao walikuwa ni mchanganyiko kuanza vijana hadi kufikia watu wazima alipendele kuzungumguza moja kwa moja nao. Kwani alisema: “Nilikuwa nimeandaa hotuba ya kuwahutubia, lakini ninawapa maandishi kwani ninataka kuzungumzia juu ya yale ambayo yametoka  ndani humu. Ninataka kusisitizia juu ya picha ya mwisho kuhusu ‘mlango’. Uzoefu huu wa mlango uliofunguliwa, mlango uliofungwa, hofu ya kutoweza kufunguliwa mlango, hofu ya kuona  mlango unafungwa machoni pa mtu… Ni uzoefu huu ambao tumemaliza kuusikia kutoka kwa  mmojawapo kati yenu, ni uzoefu wa kila mmoja wetu anayetusikiliza humu ndani.

Mkuu wa Chama cha Lazare akisoma hotuba kwa niaba ya chama cha upendo kwa maskini
Mkuu wa Chama cha Lazare akisoma hotuba kwa niaba ya chama cha upendo kwa maskini

Na ninauliza je mimi ninahusiano gani na mlango? Wengine wanafikiria mlango ni milki yao na na huweka kufuli na kujifungia. Wengine wanaogopa kubisha hodi. Ni hofu hiyo tuliyonayo ya kujua ikiwa tutakaribishwa na kukubalika. Wengine wanataka kuingia lakini wanaogopa mlango na wanajaribu kuingia kupitia dirishani. Na kwa hivyo tunaweza kufikiria hali nyingi na kujiuliza, je! Nina uhusiano gani na mlango?

Mlango ni Mungu, kwa njia hiyo uhusiano wangu na mlango ni upi? Papa ameuliza swali la pili na kufafanua “Ninajipatia mlango mimi mwenyewe na simruhusu mtu yeyote aingie au ninaogopa kubisha hodi au natumaini bila kubisha kwamba mtu atanifungulia. Kila mmoja wetu ana mitazamo tofauti na Mungu, ambaye ni mlango. Wakati mwingine maishani unahitaji kuwa na unyenyekevu kubisha mlango. Wakati mwingine unahitaji kuwa na ujasiri wa kutokuwa na hofu ya yeyote atakayenifungulia mlango, ambaye ni Mungu.

Papa akibariki mama mjamzito wa kikundi cha chama cha Lazare
Papa akibariki mama mjamzito wa kikundi cha chama cha Lazare

Papa Francisko akiendelea ameendelea kufafanua kwamba “Na mara tu ninapoingia ni muhimu kuwa na ukuu wa kutofunga mlango nyuma yangu bila kufungulia  wengine kuingia na ndivyo Lazare wanavyofanya, kufungua milango. Na hiyo ndiyo ninapenda kuwashukuru kwa leo, ushuhuda huu, sio tu wa walinda mlango, wao sio walinda mlangi bali ni wanaume na wanawake ambao, kwa kuwa mara moja baada yakufunguliwa mlango kwa kila mmoja wao, wanahisi haja ya kuwafungulia wengine. Mlango ni Mungu, ambaye hutufungulia, mlango ni moyo wetu… uko wazi, unalindwa…. Yote ni kazi ya kufikiria lakini wawao wanajua jinsi ya kufanya.

Machozi kutokana na hisia za kufikiria machungu mbele ya Papa
Machozi kutokana na hisia za kufikiria machungu mbele ya Papa

Papa amewemshukuru kila mmoja wao kwa ushuhuda ambao wanatoa na kuendelea. ‘Lazare’ ni jambo dogo, watu wachache, maeneo machache, mbele ya hitaji kubwa sana. Lakini Yesu wakati mmoja alisema kitu: kwamba hata chachu ni kitu kidogo na kwamba inauwezo wa kufanya kukua na kuzidisha, vile vile  kwamba mbegu ni  kitu kidogo lakini chenye uwezo wa kukuza mti ukawa mkubwa. Jambo baya zaidi ambalo linaweza kutokea kwa Lazare ni kusahau kuwa wao ni wadogo, kwa sababu ikiwa watajifanya kuwa wakubwa moyoni, kwa njia ya nguvu, kiburi, kutoridhika, mti hautakua na wingi wa majani yake hautapanuka.

Ukaribu wa Papa wa kupokea kila mmoja
Ukaribu wa Papa wa kupokea kila mmoja

Utajiri wao hauko benki, utajiri wao ni mdogo na uendelee. Papa ameomba walioombee Kanisa, ili Mama Mtakatifu wa  Kanisa, sisi wanaume na wanawake wa Kanisa, tujifunze kufungua mlango kila wakati na kuwa na sikio kwa wale wanaobisha hodi, wakati mwingine wakiwa dhaifu, amehitimisha.

30 August 2021, 13:57