Tafuta

2021.08.27 Mkutano wa Papa na Mtandao katoliki wa wabunge kimataifa. 2021.08.27 Mkutano wa Papa na Mtandao katoliki wa wabunge kimataifa. 

Papa Francisko:Wanasiasa walinde hadhi ya binadamu na tishio la kiteknolojia

Papa amekutana na washiriki wa Mtandao wa Wabunge wa Kikatoliki Kimataifa na kusema zana za siasa na kanuni ziruhusu wabunge kulinda hadhi ya kibinadamu wakati inatishiwa kwa mfano,janga la picha za utupu kwa watoto,unyonyaji wa data kibinafsi, mashambulio ya miundombinu muhimu kama hospitalini,na uwongo ulioenea kupitia mitandao ya kijamii.Uviko ni janga kusiloelezeka kwa kuharibu uchumi kijamii.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Ijuma tarehe 27 Agosti 2021, amekutana na washiriki wa Mtandao wa Wabunge  Kikatoliki Kimataifa, kutoka Nchi mbali mbali  ambapo amesema anakutana nao katika kipindi kigumu cha kihistoria. Amemshukuru Kardinali Schönmborn na Bwana Alting von Geusau kwa ajili ya maneno yao na salamu katika utangulizi wake. Amefurahi Papa kwa uwepo wa uwakilishi wa Ignatius Aphrem II, Patriaki wa Kanisa la Siro ya Kiorthodox. Papa amesema kuwa tangu kuanza kwa Mtandao wa Wabunge wakatoliki Kimataifa mnamo 2010, wamesindikiza, wameunga mkono na kuhamasisha shughuli za Vatican kama mashuhuda wa Injili katika kutumikia nchi zao na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla. Papa Francisko anawashukuru kwa upendo wao kwa Kanisa na kwa ushirikiano wao na utume wao. Mkutano wao umeangukia katika wakati mgumu sana, ambapo ni katika janga la Uviko-19 unaoendelea. Papa amesema kweli kumerekodiwa maendeleo yenye maana katika uundaji na katika ugawaji wa chanjo muafaka, lakini bado inabaki kazi kubwa ya kupeleka hadi mwisho. Kuna mataifa ambayo yana milioni mbili za kesi za maambukizi, na vifo vya milioni nne katika balaa hili la kutisha, ambalo limesababisha uharibifu mkubwa wa uchumi na kijamii, amesisitiza.

Papa akikaribishwa kwenye ukumbi
Papa akikaribishwa kwenye ukumbi

“Jukumu lao la ubunge kwa maana hiyo ni muhimu sana.  Kwa kupendekeza kuhudumia kwa wema kwa ajili ya wote, wao wanaalikwa kushirikishana kwa njia ya matendo yao ya kisiasa na kupyaisha kwa dhati jumuiya zao na jamii zao zote. Na si tu katika kupambana na virusi na wala hata kwa ajili ya kurudi katika hali kabla ya janga, maana ameongeza kusema Papa kuwa haiwezekani ukawa  ndiyo ushindi, badala yake ni katika kukabiliana na sababu za kina ambazo zimeoneshwa na mgogoro huo na  kuongezea zaidi, kama vile umaskini, ukosefu wa usawa kijamii, kuongezeka kwa ukosefu wa ajira, na hukosefu wa kupate elimu. Papa amesema kuwa katika mgogoro haiwezeni kuondoka sawa, kwa maana hiyo au tutatoka tukiwa bora au vibaya.  Na hauwezi kutoka kwenye mgogoro ukiwa peke yako, kwani tutatoka tukiwa pamoja au hatutaweza kutoka nje ya mgogoro huo! amesisitiza Papa. Katika enzi ya machafuko ya kisiasa na ubaguzi wabunge na wanasiasa kwa ujumla hawana sifa kubwa. Na suala hili hakuna lililo jipya, amesema. Licha ya hayo kuna wito ambao ni mkuu uliopo na ambao ni wa kuhudumia wema wa wote na kutoa kipaumbele cha ustawi wa wote, kabla ya faida ya kibinafsi? Lengo hili linapaswa kuwapo daima na  kwa sababu endo la kuwa mwanasiasa mwema, ndiyo wajibu mkuu kwa ajili ya udugu wa ulimwengu na amani kijamii ( Waraka Fratelli tutti 176).

Hotuba ya wakuu wa Mtandao wa kimataifa
Hotuba ya wakuu wa Mtandao wa kimataifa

Katika nyakati zetu ambazo zimegubikwa na changamoto kubwa katika mtazamo huo unahitaji usimamizi wa teknolojia kwa faida ya wote. Maajabu ya sayansi na teknolojia ya kisasa yameongeza ubora wa maisha yetu. Kwa maana hiyo ni vema kufurahia kwa sababu ya maendeleo  haya na shauku kubwa mbele ya uwezekano mkubwa ambao unafunguliwa katika mapya haya yanayoendelea; kwa sababu sayansi na teknolojia  ni pia tunda la kushangaza la ubunifu wa kibinadamu ambao ni zawadi ya Mungu (rej Waraka wa Laudato s’,102). Walakini  hayo  yote yakiachwa peke yake na nguvu zake za masoko, bila ya kutoa fursa ya miongozo iliyochukuliwa na mikutano ya sheria na mamlaka nyingine za umma zinazoongozwa na hisia ya uwajibikaji wa kijamii, ubunifu huo unaweza kutishia hadhi ya mwanadamu. Sio suala la la kurudisha nyuma maendeleo ya kiteknolojia , Papa amesema. Walakini, zana za siasa na kanuni huruhusu wabunge kulinda hadhi ya kibinadamu wakati inatishiwa. Papa amefikiria, kwa mfano, juu ya janga la picha za utupu kwa watoto, unyonyaji wa data binafsi, mashambulio ya miundombinu muhimu kama hospitalini, na uwongo ulioenea kupitia mitandao ya kijamii. Sheria makini inaweza na lazima iongoze mabadiliko na matumizi ya teknolojia kwa faida ya wote.  Baba Mtakatifu Francisko anawatia moyo kwa jitihada za kuchukua wajibu wa kazi kwa umakini na kwa tafakari ya kina kimaadili juu ya hatari na fursa ambazo zimo katika maendeleo ya kisayansi na kiteknoloja ili sheria na viwango vya kimataifa vinavyozisimamia vizingatie kukuza maendeleo fungamani ya binadamu na amani, badala ya maendeleo kama mwisho wenyewe.

Akisalimiana na washiriki wa mtando huo wa kimataifa
Akisalimiana na washiriki wa mtando huo wa kimataifa

Wabunge kawaida huonesha nguvu na udhaifu kwa wale wanaowawakilisha, kila mmoja akiwa na umaalum wa kuwekwa katika huduma ya wote, amesema Papa. Kujitolea kwa raia, katika maeneo ambali mbali, ushiriki wa kijamii, kiraia na kisiasa, ni muhimu. Ameongeza Papa:“Sisi sote tumeitwa kukuza roho ya mshikamano, kuanzia na mahitaji ya watu dhaifu na wanyonge. Walakini, kuponya ulimwengu, kujaribiwa vikali na janga hili, na kujenga mustakabali unaojumuisha zaidi na endelevu ambapo teknolojia hutumikia mahitaji ya wanadamu na haitutenganishi na mmoja na mwingine kwa maana hatuhitaji tu raia wenye dhamana, lakini pia viongozi waliojiandaa na walio hai kwa kanuni ya faida ya wote". "Wapendwa, Bwana na awajalie kuwa chachu ya kuzaliwa upya kwa akili, moyo na roho, mashuhuda wa upendo wa kisiasa kwa walio dhaifu zaidi, ili, kwa kuwahudumia, muweze kumtumikia kwa kila mnachofanya. Ninawabariki, ninabariki familia zanu na ninabariki kazi yenu. Nanyi pia ninawaomba tafadhali, mniombee. Asante." Amehitimisha Baba Mtakatifu.

HOTUBA YA PAPA 27 AGOSTI 2021
27 August 2021, 16:14