Tafuta

Papa Francisko:Tunahitaji mkate wa uzima ambao ni Yesu mwenyewe

Papa Jumapili Agosti,8 kabla ya sala ya Malaika wa Bwana ametoa tafakari ya Injili ya Siku ambapo Yesu anaeleza kuwa Yeye ni Mkate wa Uzima(Yh 6,8).Papa amesema ili kuweza kuishi kunahitajika mkate na mwenye njaa hataki chakula laini bali mkate na wala cha bei,lakini mkate.Hasiye kuwa na kazi,haombi mshahara mkubwa,bali mkate wa siku.Yesu hapendi kuondoa uhusiano wa karibu na Yeye au kumtafuta wakati tukiwa na shida.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Injili ya Liturujia ya siku, Yesu anaendelea kuhubiri kwa watu ambao waliona miujiza ya mikate. Na anawaalika watu hao kufikiria mbali zaidi, baada ya kuona manna ambayo Mungu aliwashibisha mababa katika hija yao  ya safari wakiwa jangwani, na sasa anatoa ishara nyingine ya kuwa Yeye mkate. Yeye anasema wazi: “Mimi ni mkate wa Uzima” (Yh 6,48). Lakini hii ina maana gani ya mkate wa uzima? Papa anauliza na kujibu kuwa ili kuweza kuishi kuna haja ya mkate. Mwenye njaa haombi chakula kilaini, na cha bei, lakini mkate. Hasiye kwa na kazi, haombi mshahara mkubwa, bali mkate wa siku. Yesu anaonesha wazi jinsi mkate, kwa maana ya kitu kilicho muhimu katika maisha ya kila siku. Bila Yeye hakuna jambo linafanya kazi. Ndivyo alivyo anza Papa Francisko tafakari yake kwa mwahujaji na waamini waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican, tarehe 8 Agosti 2021.

Papa akiwapungia mkono mahujaji katika kiwanja cha Mt. Petro
Papa akiwapungia mkono mahujaji katika kiwanja cha Mt. Petro

Siyo mkate kati ya mikate bali ni mkate wa uzima

Papa akiendelea na tafakari hii amesema kuwa "Siyo mkate kati ya mikate, bali mkate wa uzima. Kwa maneno mengine, sisi bila yeye badala ya kuishi tunazeeka. Hii ni kwa sababu, ni Yeye peke yake anaye mwilisha roho, ni Yeye peke yake anaye samehe mabaya ambayo kwetu sisi hatuwezi peke yetu kushinda kwani ni Yeye ambaye anatufanya kuhisi tunapenda hata kama sisi wengi wanatukatisha tamaa. Ni Yeye anatupatia nguvu za kupenda na ni Yeye anatupatia nguvu za kusamehe katika matatizo. Ni Yeye peke yake anatoa amani ya moyo ambayo tunatafuta; ni Yeye anatupatia uzima wa milele wakati maisha ya hapa dunia yanakwisha. Ni mkate muhimu wa uzima. “Mimi ni mkate wa uzima anasema”, Papa kuwa tubaki katika sura hii nzuri ya Yesu. Yeye angeweza kufikiria, maonesho, lakini tutambua kuwa Yesu anazungumza kwa mifano na ndiyo vielelezo vyake. “Mimi ni mkate wa uzima”.

Mkate wa uzima unajumuisha ukweli wake na utume wake

 “Mimi ni mkate wa uzima”, ambao unajumuisha ukweli wake na utume wake. Huo utaonekana kikamilifu mwishoni, wakati wa karamu Kuu. Yeye anajua kuwa Baba anamwomba si tu kwa kuwapatia watu chakula wale, lakini yeye, aweze kujimega mwenyewe, maisha yake, mwili wake na mwoyo wake ili sisi tupate uzima. Maneno haya ya Bwana yanatoa mwamko ndani mwetu ya kuwa  mshangao wa zawadi ya Ekaristi. Hakuna mtu yeyote katika ulimwengu, kwa kiasi anachompenda mtu mwingine anaweza kuwa chakula kwa ajili yake. Mungu alifanya hivyo na anafanya kwa ajili yetu. Baba Mtakatifu anaomba tupyaishe mshangao huo. Tufanye hivyo kwa kuabudu mkate wa uzima kwa sababu kuabudu kunajaza uzima na mshangao.

Mahujaji katika kiwanja cha Mt. Petro
Mahujaji katika kiwanja cha Mt. Petro

Yesu hapendi kutafutwa wakati tukiwa na shida

Katika Injili lakini badala ya kushangaa, watu walianza kunung’unika, wanachana nguo. Wanafikiri wakisema “Huyu siye Yesu, tunamjua na familia yake? Sasa asemaje huyu, Nimeshuka kutoka mbinguni? (Yh 6,41-42). Hata sisi labda tunanung’unika hivyo Papa amesema. Tunasema kuwa ingekuwa vizuri Mungu akae mbinguni bila kujichanganya katika maisha yetu, wakati sisi tunaendelea na mambo yetu hapa duniani. Badala yake, Mungu alijifanya mtu ili aingie kwa dhati ulimwenguni, aingie kwetu kwa dhati, Mungu aijifanya mtu kwa ajili yangu, yako na kwa ajili yetu sisi ili awe katika maisha yetu. Na kila kitu katika maisha yetu, vinamhusu”, amesisitiza Papa. “Sisi tunaweza kumsimulia juu ya matokeo ya kazi, ya siku na kila kitu, uchungu, huzuni na mambo mengine, tunaweza kumwambia yote kwa sababu Yesu anatamani kuwa na uhusiano huo wa kina kwetu sisi. Lakini je ni kitu gani ambacho hakipenda? Papa ameuliza swali na kulijibu: "Ni kule kuondoa uhusiano wa ukaribu naye, Yeye ambaye ni mkate, kujiachia na kujiweka pembeni, au kumtafuta wakati tukiwa na shida tu, amebainisha.

Umati ukisali na Papa sala ya Malaika wa Bwana
Umati ukisali na Papa sala ya Malaika wa Bwana

Angalau mara moja katika chakula cha usiku tumwalike Yesu mkate wa uzima

Mimi ndimi mkate wa uzima. Papa Francisko ameshauri kwamba “Angalau mara moja kwa siku tujikute tunakula chakula kwa pamoja na labda wakati wa usiku katika familia, baada ya siku ya kazi au masomo”. Ingekuwa vizuri sana kabla ya chakula, kumwalika Yesu, mkate wa uzima, kumwomba kwa urahisi, kubariki kile ambacho ametenda na kile ambacho tumeweza kufanya. Kumwalika nyumbani na kusali katika mtindo wa kinyumbani. Yesu atakuwa katika karamu na sisi, na tutushibishwa kwa upendo mkubwa", Papa amesisitiza. "Bikira Maria, ambaye Neno lilifanyika mwili, atusadie kukua siku hadi siku katika urafiki wa Yesu, mkate wa uzima". Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu Francisko amewasalimia mahujaji wote waliofika kutoka pande  za Italia na nje ya Italia. Na amehitimisha kwa kuwatakia kila baraka ya Domenika na mlo wa mchana mwema.

TAFAKARI YA PAPA
08 August 2021, 13:01