Tafuta

2021.06.06 Misa ya Papa katika Siku kuu ya Mwili na Damu ya Yesu 2021.06.06 Misa ya Papa katika Siku kuu ya Mwili na Damu ya Yesu 

Papa Francisko:Liturujia irudi katika kiini cha imani ya Wakristo

Papa Francisko ametuma salamu kwa washiriki wa Wiki ya Liturujia kitaifa kuanzia 23-26 Agosti na kwamba mwaka wa Uviko-19 unaweza kusaidia Kanisa kugundua umuhimu wa nin maana ya mkutano wa Ekaristi ya Dominika.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko ametuma ujumbe wake uliotiwa saini na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro parolin, Katibu wa Vatican kwa Mwenyekiti wa Kituo cha shughuli za Liturujia Monsinyo Claudio Maniago katika fursa ya Ju,a la Liturijia Kitaifa nchini Italia ambayo imeanza tarehe 23 Agosti na itamalizika tarehe 26 Agosti 202,  huko Cremona, Italia. Katika ujumbe huo, unaonesha matashi mema kwa wote katika Jimbo lilalokaribisha wiki hiyo na washiriki wote katika siku hizi za mafunzo. Papa anaungana kwa pamoja kumshukuru Bwana kwa sabababu Mwaka huu ambao imewezekana kufanyika tukio hili baada ya huzuni mkubwa wa kipindi chote cha mwaka jana kutokana na hali ngumu ya uviko -19 na ambapo waliahirisha mpango huo. Maamuzi yenye uzito yaliyotolewa lakini yaliwezesha kuthibitishwa na nuru mpya iliyochagulia katika mantiki na hali halisi iliyojitokeza na jaribu gumu la kuenea kwa Uviko 19  na  vizingiti vyake  vya kuzuia.  Papa amesema kauli mbiiu iliyo chaguliwa kuongoza kwa hakika ni kiashirio cha wafuasi wa Bwana katika kukutana  “fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu (Lk 22, 19):mahali walipo  wawili au watatu kwa jina langu(Mt 18,20). Jumuiya, liturujia na eneo.

Papa anasema kuwa “Wiki ya kukusanyika kwa pamoja katika jina la Bwana, tangu asili yake ilioneshwa wazi na wakristo kama hali halisi isioachwa na isiotengenishwa ule uhusiano  wa utambulisho wake, japokuwa ilishambuliwa wakati wa kipindi kigumu cha kujizuia na janga.  Lakini pendo kwa ajili ya Bwana na ubunfu wa kichungaji ulisukuma wachungaji na waamini walei kugundua njia nyingine kwa ajili ya kumwilisha muungano huo wa imani na wa upendo na Bwana na ndugu, katika matarajio ya kurudi kwa ukamilifu kuadhimisha ekaristi katika utulivu na usalama. Ni matarajio mengi na mateso yaliyangazwa na fumbo la Msalaba wa Bwana na kutoa matunda mengi ya shuguli za utunzaji, upendo kidugu na huduma kwa watu wa Mungu ambao waliteseka kutokana na matokeo ya dharura ya kiafya. Uzoefu wa huzuni wa kufungwa kwa liturujia kwa mwaka jana, imefanya kuonekana  ule wema katika safari kubwa iliyotimizwa kuanza na Mtakaguso wa Pili wa  Vatican, katika njia iliyoonesha kwenye Katiba ya Sacrosanctum Concilium.

Liturujia iliyositishwa wakati wa kipindi kigumu na matatizo ya kuanza kwa upya yameoneshwa watu jinsi ambavyo walikuwa na shida wakati wa Dominika katika Peninsula ya Italia  yote ambayo ilionesha wazi mabadiliko makubwa ya nyakati. Tunaona jinsi katika maisha halisi ya watu, maoni ya wakati wenyewe yamebadilika na, kwa maana hiyo, Dominia zenyewe, nafasi, na athari juu ya njia ya kuwa na hisia za jamii, watu, familia na uhusiano na eneo. Kuunganika katika siku ya Dominika kwa maana hiyo ilikuwa haina ushuriki   wa kizazi, kwa  maana ya utofauti wa kitamaduni, na kwa juhudi za kupata ule ujumuishaji mzuri katika maisha ya parokia, kuwa kweli kilele cha shughuli zake zote na chanzo cha nguvu ya kimisionari ambacho kinaleta pamoja Injili ya huruma katika sehemu mahalia za kijiografia na zilizopo.

Papa Francisko anayo matumaini kuwa kWiki ya Liturujia kitaifa, na majibu yake ya tafakari na wakati wa maadhimisho hayo licha ya kufanya kwa uwepo wa watu na kwa njia ya mtandao, inaweza kuwa ya aina yake na kutoa ushauri kwa baadhi ya miongozo ya kichungaji kiliturujia ili kuwapa  wanaparokia,  katika Dominika, katika mkutano wa ekaristi, huduma na ili ibada iweze  kuonekana upenda ambapo Ekaristi ina kuwa kiini katika imani na hali ya kiroho ya waamini wote. Uchapishaji wa hivi karibuni wa toleo la tatu la Misale ya Kirumi na utashi wa Maaskofu wa Italia uwasindikize ndugu na kuanza tena kwa malezi ya kiliturujia ya watu watakatifu wa Mungu na ambayo inaasharia vizuri mwelekeo huu. Papa anahitimisha ujumbe wake kwa kukaribisha Maadhimisho ya Wiki ya 71 ya Liturujia kitaifa inayofanyika katika eneo ambalo limeteseka sana kwa sababu ya janga na lakini ambalo limeona wema unachanua ili kufariji mteso ya kibinadamu. Anawakikishia sala zake na kuwabariki kwa baraka takatifu ya kitume,  Askofu wa Jimbo linalokaribisha Juma hili, Askofu Antonio Napolioni, maaskofu wengine, makuhani, mashemasi, watawa, watoa mada na washiriki wote. 

23 August 2021, 15:52