Tafuta

Papa Francisko amempongeza Padre Massimo Fusarelli kwa kuchaguliwa kwake kuwaongoza Ndugu Wafrancisko Wakapuchini, na anakuwa ni mkuu wa Shirika wa 121 toka kwa Mt. Francisko wa Assisi. Papa Francisko amempongeza Padre Massimo Fusarelli kwa kuchaguliwa kwake kuwaongoza Ndugu Wafrancisko Wakapuchini, na anakuwa ni mkuu wa Shirika wa 121 toka kwa Mt. Francisko wa Assisi. 

Padre Giovanni Fusarelli Mkuu Mpya Wa Shirika La Wafranciskani!

Papa amemtumia Padre Giovanni Fusarelli salam na matashi mema baada ya kuchaguliwa kuliongoza Shirika. Amemhakikishia sala na baraka zake za Kitume, ili Mwenyezi Mungu aweze kumsaidia na kumlinda katika utekelezaji wa utume wake kwa ajili ya Shirika na Kanisa katika ujumla wake. Mt. Francisko wa Assisi amtie shime katika kuwaongoza ndugu zake Wafranciskani.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.  – Vatican.

Kardinali João Braz de Aviz, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume, Jumanne, tarehe 13 Julai 2021baada ya Uchaguzi Mkuu wa Shirika la Ndugu Wafrancisko Wakapuchini amemtangaza Mheshimiwa Padre Giovanni Fusarelli kuwa ndiye Mkuu mpya wa Shirika la Ndugu Wafrancisko Wakapuchini katika kipindi cha miaka sita yaani kuanzia mwaka 2021 hadi mwa 2027. Anakuwa ni mkuu wa Shirika wa 121 kutoka kwa Mtakatifu Francisko wa Assisi. Hadi kuchaguliwa kwake, Padre Giovanni Fusarelli, alikuwa ni Padre mkuu wa Kanda ya Mtakatifu Bonaventura kwa watawa wa Shirika walioko Lazio na Abruzzo. Alikuwa pia Paroko wa Parokia wa Kanisa la “San Francesco a Ripa”, Jimbo kuu la Roma. Alikuwa pia mratibu wa mradi wa huduma kwa ajili ya maskini.

Baba Mtakatifu Francisko amemtumia Padre Giovanni Fusarelli salam na matashi mema baada ya kuchaguliwa kuliongoza Shirika. Baba Mtakatifu anapenda kumhakikishia Padre Giovanni Fusarelli sala na baraka zake za Kitume, ili Mwenyezi Mungu aweze kumsaidia na kumlinda katika utekelezaji wa utume wake kwa ajili ya Shirika na Kanisa katika ujumla wake. Mtakatifu Francisko wa Assisi amtie shime katika kuwaongoza ndugu zake Wafranciskani. Itakumbukwa kwamba, Padre Giovanni Fusarelli alizaliwa tarehe 30 Machi 1963. Baada ya masomo na majiundo yake ya kitawa, tarehe 8 Januari 1989 akaweka nadhiri zake za daima na hatimaye, tarehe 30 Septemba 1989 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Wanashirika wanamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kazi na utume uliotekelezwa na Padre Michael Perry ambaye ameliongoza Shirika kwa kipindi cha Miaka sita. Ameonesha moyo mkuu na utu, na udugu wa kibinadamu. Mkutano mkuu wa uchaguzi wa Shirika la Ndugu Wafrancisko Wakapuchini umewashirika wanashirika 118 kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Kauli mbiu ambayo imeongoza maadhimisho haya ni “Tupyaishe dira yetu, tuyapokee yajayo”. Ni kauli ambayo inachota amana na utajiri wake kutoka katika Maandiko Matakatifu “Amka… na Kristo atakuangaza.” Ef 5:14. Mkutano utafungwa rasmi tarehe 18 Julai 2021.

Maadhimisho ya Mkutano Mkuu wa Shirika ni kipindi maalum cha sala, tafakari na mang’amuzi ya kina mintarafu amana na utajiri wa Shirika na wanashirika wenyewe; maisha na utume wa Shirika kwa kuangalia changamoto, matatizo na fursa zilizopo kama sehemu ya mchakato wa uinjilishaji mpya unaofumbatwa katika ushuhuda wenye mvuto na mashiko. Huu ni wakati muafaka wa kusoma alama za nyakati na kuangalia wapi ambapo Roho Mtakatifu anawataka kwenda katika kipindi cha miaka sita kuanzia sasa!

Wafranciskani
14 July 2021, 15:13