Tafuta

Papa Francisko:Upendo unatakasa maisha na siyo kuhukumu wengine

Katika tafakari ya Papa Francisko kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana,amekumbisha kuwa uponywaji ambao unahesabiwa zaidi katika maisha ni ule wa upendo zaidi. Upendo hainunuliwa bali unapatikana kwa kuongia katika urafiki wa kweli na Yesu huku ukwasaida wengine waliojeruhiwa na walio na upweke.Ametoa onyo la kutohukumu wengine kwa maana upendo unatakasa maisha.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Jumapili tarehe 27 Juni 2021 tafakari ya Papa kabla ya sala ya Malaika wa Bwana imeongozwa na Injili ya Marko 5,21-45 akiwageukia waamini na mahujaji wote waliounganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican.  Papa amesema: “leo hii, katika Injili, Yesu anakumbana na hali zetu mbili za kutisha kifo na ugonjwa. Kutokana na hayo anawaokoa watu wawili, mmoja ni mtoto ambaye alifariki wakati baba yake amekwenda kumwomba Yesu msaada; na mwanamke ambaye kwa miaka mingi alikuwa anatokwa damu. Yesu anaacha aguswe na uchungu wetu na kifo chetu na anatenda ishara mbili za uponyaji kwa ajili ya kutueleza kuwa, uwe uchungu wala kifo havina neno la mwisho. Anatueleza kuwa kifo siyo mwisho. Yeye anashinda adui ambaye hatuwezi kujikomboa peke yetu.

Papa Francisko ameomba kujikita kutafakari wakati huu ambapo magonjwa bado ni kiini cha habari za kila siku, hasa katika ishara nyingine ya uponywaji wa mwanamke. Zaidi ya afya yake, ni mapenzi yake ambayo yalibadilishwa: alikuwa na upotezaji wa damu na kwa hivyo, kulingana na mawazo ya wakati huo, alichukuliwa kuwa mchafu. Ugonjwa mkubwa sana katika maisha ni ukosefu wa upendo, na kukosa kupenda. Na uponywaji ambao unahesabiwa zaidi ni ule wa upendo wa karibu, Je jinsi gani ya kuupata?  Je ulikuwa ni saratani, TB,  janga? Hata ukosefu wa upendo ni ugonjwa. Sisi tunaweza kufukiria wapendwa wetu, je ni wagonjwa au wana afya, Yesu ana uwezo wa kuwaponesha. Kwa maana hii alikuwa amebaguliwa hasingekuwa na uhusiano wenye msimamo, kuolewa, kuwa na familia, kuna na uhusiano wa kawaida wa kijamii. Alikuwa anaishi peke yake, na moyo uliojeruhiwa.

Papa kwa kutoa mifano hai amesema: “Sisi sote tuna historia na kila mmoja wetu, kwa siri yake, anajua mambo mabaya ya historia yake vizuri. Lakini Yesu anawatazama ili awaponye. Badala yake tunapenda kuangalia mambo mabaya ya wengine. Ni mara ngapi, tunapozungumza, tunaingia kwenye gumzo, ambayo ni kusengenya juu ya wengine, “kuwachuja ngozi” wengine. Lakini angalia: huu ni upeo gani wa maisha? Sio kama Yesu, ambaye kila wakati anaangalia njia ya kutuokoa, anaangalia leo, kwa mapenzi mema na sio historia mbaya ambayo tunayo. Yesu huenda zaidi ya dhambi. Yesu huenda zaidi ya chuki. Wala usihukumu, usihukumu hali halisi ya kibinafsi, kijamii ya wengine. Mungu anapenda kila mtu! Usihukumu, wacha wengine waishi na jaribu kuwakaribia kwa upendo”.

Historia ya mwanake hasiye kuwa na jina ambaye tunaweza kujfananisha wote, ni mfano. Maandiko yanasema kuwa alikuwa amefafanya matibabu mengi kwa kutumia mali zake zote bila nafuu labda kuongezeka. Hata sisi ni mara ngapi pia tunajitupa katika tiba mbaya ili kutosheleza ukosefu wetu wa upendo? Tunafikiria kuwa na mafanikio na pesa hutufurahisha, lakini upendo hauwezi kununuliwa. Tunakimbilia kwenye mitandao ya kidigitali lakini upendo ni halisi. Hatujikubali kwa jinsi tulivyo na kujificha nyuma ya kujiremba kijuujuu, lakini upendo siyo wa kijujuu. Tunatafuta suluhisho za waganga na kutumia fedha na bila amani kama mwanamke huyo. Yeye hatimaye alichagua Yesu na kujitupa katikati  ya umati ili kugusa lembo la vazi lake. Mwanamke huyo huyo alikuwa anatafuta mawasiliano ya moja moja ya mguso wa Yesu. Hasa katika kipindi hiki, tumeelewa zaidi ni kwa jinsi gani ni muhimu kuwa na  mahusiano ya karibu. Hayo pia ni sawa na Yesu. wakati mwingine tunaridhika na kufuata maagizo kadhaa na kurudia sala, lakini Bwana anasubiri tukutane naye, ili kufungua mioyo yetu kwake,na, kama mwanamke, kugusa vazi lake ili kupona. Hii ni kwa sababu, katika kuingia urafiki na Yesu, tunaponywa katika mapenzi yetu.

Hilo ndilo Yesu anataka. Tunaona kwa hakika kuwa pamoja na msongamano wa watu, Yesu alitazama huku na kule ili aone aliyemgusa. Ni mtazamo wa Yesu. Kuna watu wengi, lakini yeye anaendelea kutatufa uso na katika moyo uliojaa imani. Hatazami kiujumla, lakini kwa  mtu mjoa mmoja. Hajizuii mbele ya majeraha na makosa ya wakati uliopita, bali anakwenda zaidi ya dhambi na hukumu. Hasimami juu ya ujuu juu, bali anafika moja kwa moja katika moyo. Na anamponya yeye ambaye alikuwa amebaguliwa na wote. Kwa huruuma anamwita mtoto na kumsifu kwa imani yake na kurudishaia imani ile ile, Papa Francisko amefafanua.

Sisi sote tuna historia na kila mmoja wetu, kwa siri yake, anajua mambo mabaya ya historia yake vizuri. Lakini Yesu anawatazama ili awaponye. Badala yake tunapenda kuangalia mambo mabaya ya wengine. Ni mara ngapi, tunapozungumza, tunaingia kwenye gumzo, ambayo ni kusengenya juu ya wengine, "kuwachuja ngozi" wengine. Lakini angalia: huu ni upeo gani wa maisha? Sio kama Yesu, ambaye kila wakati anaangalia njia ya kutuokoa, anaangalia leo, kwa mapenzi mema na sio historia mbaya ambayo tunayo. Yesu huenda zaidi ya dhambi. Yesu huenda zaidi ya chuki.

Papa Francisko kwa kuhitimisha ameomba kuacha Yesu atazame na kuponya mioyo yetu. Ikiwa tayari tumekumbana na mtazampo wa upendo juu yetu, tumuige, tufanye kama yeye. “Tazama pembeni mwako utaona watu wengi ambao wanakuja kwako na wanahisi kujeruhiwa na wako peke yao, wanahitaji kusikia wanapendwa. Yesu anakuomba kuwa na mtazamo ambao haubaki kutazama kijuu juu, badala yake unakwenda moja kwa moja katika moyo. Mtazamo mwema usiohukumu bali unaokaribisha. Kwasababu ni upendo unaotakasa maisha tu. Mama Maria Mfariji wa wanaotaabika, atusaidie kupeleka bembelezo kwa waliojeruhiwa moyoni na  ambao tunakutana nao njiani”, amesema Papa.

27 June 2021, 14:54