Tafuta

2021.06.25 Papa Francesco akipokea patena kutoka kwa Akofu mkuu Panti Filibus Musa,Mwnyekiti wa Shirikisho la Kilutheri Ulimwenguni wakati wa mkutano na wawakilishi. 2021.06.25 Papa Francesco akipokea patena kutoka kwa Akofu mkuu Panti Filibus Musa,Mwnyekiti wa Shirikisho la Kilutheri Ulimwenguni wakati wa mkutano na wawakilishi. 

Papa kwa Walutheri:Kristo anatusindikiza kutoka katika mzozo hadi muungano

Papa Francisko wakati wa kukutana na wawakilishi wa Shirikisho la Kilutheri Ulimwenguni,amewatia moyo wote ambao wanajikita katika mazungumzo katoliki na kilutheri ili kuendelea kwa matumaini katika sala bila kuchoka,mazoezi ya upendo shirikishi na katika mateso ili kutafuta na kuufikia umoja kamili ambao ni mapenzi ya Bwana.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ijumaa tarehe 25 Juni 2021, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuzungumza na Wawakilishi wa Shirikisho la Kilutheri Ulimwenguni. Katika kuanza hotuba y yake amenukuu maneno ya Mtakatifu Paulo kwa Warumi: "Neema na amani ya Mungu Baba wetu na Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi" (Rm 1,7) na kuwasalimia wawakili hao kwa namna ya pekee Mwenyekiti wao Askofu Mkuu Musa na kumshukuru kwa maneno yake, pia na Katibu Mkuu, Mchungaji Martin Junge. Baba Mtakatifu Francisko amewakumbusha jinsi anavyokumbuka ziara yake huko Lund, mji ambao ndimo walianzisha Shirikisho lao. Amesema ni hatua zisizosahulika za kiekumene ambazo walifanya uzoefu kwa nguvu ya kiinjili na upatinisho ambao unathibitisha kuwa kwa njia ya mazungumzo na ushuhuda, wa kushirikisha, na kwamba hatuwezi kuwa na sintofahamu. Na sio wageni bali ndugu. Kwa kutembea kutoka katika mzozo kufikia umoja, katika siku ya kumbu kumbu ya barua ya Augusta, Papa amesema wao wamefika Roma ili kukua katika umoja kati yao.

Amewashuru kwa njia hiyo na kueleza matumaini yake ambayo yanatafakarisha umoja wa kukiri kupitia barua ya 'Kukiri kwa Augsburg, kwa Kilatino 'Confessio Augustana', ni maandishi ya kukiri yaliyoandikwa na Philip Melanchthon na ambayo yalisomwa katika mkutano huo huo tarehe 25 Juni 1530. Kupitia nakala zinazofafanua za Ukiri wa Augustan warekebishaji walijaribu, awali, kuanzisha tena muungano na Kanisa Katoliki. Kwa nia na malengo kwa hivyo ilikuwa hati ya kiekumene. Baadaye, hata hivyo, ikawa maandishi muhimu ya kukiri ya makanisa ya Kiprotestanti yenye asili ya Kiprotestanti na haikuweza kuzuia mgawanyiko wa Kanisa.

Papa Francisko akiendelea na hotuba yake amesema katika matazamio ya miaka 500 ya barua hiyo,kumbukumbu  inayotarajiwa kufanyika tarehe 25 Juni 2030, ni matumaini kwamba inaweza kuleta manufaa katika safari ya kiekumene. “Nilisema “njiani ya kutoka katika mzozo hadi muungano”, na safari hii hufanyika katika shi tu: na ni mgogoro ambao unatusaidia kukomaa kile tunachotafuta. Kuanzia mzozo ambao tumeishi kupitia karne na karne na karne, hadi muungano ambao tunataka, na kwa kufanya hivyo tunajiweka katika shida. Mgogoro ambao ni baraka kutoka kwa Bwana”.  Katika enzi zile za kukiri kwa mujibu wa maandishi hayo Papa amesema yalikuwa yakiwakilisha nia ya kuondoa hatari za kukana ukristo katika nchi za Magharibi. Hapo awali ilikusudiwa kama hati ya upatanisho wa ndani Kikatoliki na baadaye tu ilichukua tabia ya maandishi ya kukiri ya Kilutheri. Tayari mnamo 1980, wakati wa maadhimisho ya miaka 450, Walutheri na Wakatoliki walithibitisha kuwa: "Kile ambacho tumetambua katika kukiri 'Confessio Augustana' yaani katika ukikiri kama imani ya kawaida inaweza kutusaidia kukiri imani hii pamoja kwa njia mpya, pia katika wakati wetu. Ni kukiri pamoja kwa kile kinachotuunganisha katika imani. Papa amekumbuka maneno ya Mtume Paulo aliyondika kuwa "Mwili mmoja, ubatizo mmoja, na Mungu Mmoja (Ef 4,4.5-6). Akiendelea na ufafanuzi huo katka hotuba yake amesema:

"Mungu mmoja. Katika kifungu cha kwanza, 'Confessio Augustana' inakiri imani katika Mungu wa Utatu, akimaanisha sana mtaguso wa Nikea. Imani ya Nikea ni usemi wa lazima ambao imani sio tu kwa Wakatoliki na Walutheri, bali pia kwa ndugu wa Kiorthodox na kwa jumuiya nyingine  nyingi za Kikristo. Ni hazina ya kawaida: kwa maana hiyo iwe fursa ya kuifanyia kazi ili maadhimisho ya miaka 1700 ya baraza kuu lile yatakayoadhimishwa mnamo 2025, itoe msukumo mpya wa safari ya kiekumene, ambayo ni zawadi kutoka kwa Mungu na njia isiyoweza kubadilishwa kwetu".

Ubatizo mmoja.  Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa yote ambayo neema ya Mungu inatupatia, furaha ya kufanya uzoefu na kushinda mgawanyiko, uponyaji wa kumbukumbu, ushirikiano uliyopatanishwa na kindugu kati yetu ambao hupata msingi wake hasa katika "ubatizo mmoja wa ondoleo la dhambi" (Imani ya Nikea -Constantinopoli). Ubatizo mtakatifu ni zawadi asili ya kimungu, ambayo ni msingi wa juhudi zetu zote za kidini na kujitolea yoyote kufikia umoja kamili. Ndiyo maana  ya uekumene na sio zoezi la diplomasia ya kanisa, lakini njia ya neema. Haitegemei upatanisho na makubaliano ya wanadamu, lakini juu ya neema ya Mungu, ambayo hutakasa kumbukumbu na moyo, inashinda ugumu na inaelekeza kwenye ushirika uliosasishwa: sio kuelekea makubaliano ya kushuka au maelewano ya maridhiano, lakini kuelekea umoja uliopatanishwa katika tofauti. Kwa mtazamo huu, baba Mtakatifu amependa kuwahimiza wale wote wanaohusika katika mazungumzo ya Kikatoliki na Kilutheri kuendelea kwa kujiamini katika maombi yasiyokoma, katika kutekeleza misaada ya pamoja na shauku ya utafiti inayolenga umoja zaidi kati ya washiriki anuwai wa Mwili wa Kristo.

Mwili mmoja. Katika hilo, Baba Mtakatifu amessema kuwa Kanuni ya Taize, ina ushauri mzuri isemayo: “muwe na shauku ya umoja wa mwili wa Kristo”. Upendo mkuu kwa ajili ya umoja unaokoa kwa njia ya mateso ambayo yanajitokeza mbele katika majeraha ambayo yameumiza mwili wa Bwana. Ikiwa tunatambua uchungu wa migwanyiko ya kikristo, tunakaribisha kile ambacho Yesu alifanya uzoefu kwa kuendelea kuona mitume wasio ungana na mavazi yake yaliyo raruliwa(Yh 19,23). Papa amewashukuru kwa zawaidi ya Patena ambayo ni ishara ya ushiriki wa mateso ya Bwana. Amewaonesha jinis ambavyo  kwa namna fulani wanaishi mateso mara mbili. “Kiukweli, sisi pia tunaishi aina ya shauku mara mbili: kwa upande mmoja wa kuteseka kwa sababu bado haiwezekani kukusanyika karibu pamoja katika altare ile ile; kwa upande mwingine ni juhudi katika kutumikia sababu ya umoja, ambayo Bwana aliiombea na kutoa maisha yake”.

Bwana msulibiwa na mfufuka atubariki sisi sote hasa mpendwa Mchungaji Junge, ambaye atamaliza utumishi wake kama Katibu Mkuu tarehe 31 Oktoba mwaka huu. Amemshukuru tena kwa moyoni  wote na kwa ziara yake na amwaalika kupmba kwa pamoja, kila mmoja kwa lugha yake wenyewe, sala ya Baba yetu kwa ajili ya kuanzisha tena umoja kamili kati ya Wakristo. Kwa kuhitimisha ameomba kuendelea katika mateso kwenye safari yetu kutoka katika mzozo kufikia umoja. “Hatua inayofuata itahusu uelewa wa uhusiano wa karibu kati ya Kanisa, huduma na Ekaristi. Itakuwa muhimu kuangalia kwa unyenyekevu wa kiroho na kitaalimungu katika mazingira ambayo yalisababisha mgawanyiko, kwa ujasiri kwamba, ikiwa haiwezekani kutengua matukio ya kusikitisha ya zamani na inawezekana kuzisoma tena katika historia iliyopatanishwa.

Mkutano Mkuu wao mnamo 2023 unaweza kuwa hatua muhimu ya kutakasa kumbukumbu na kuongeza hazina nyingi za kiroho, ambazo Bwana ameziacha kwa karne zote. "Mchakato ambao unatoka kwenye mzozo hadi kufikia muungano siyo rahisi lakini hatuko peke yetu. Bwana anatusindikiza".

25 June 2021, 16:13