Tafuta

Papa Francisko asikitishwa sana na janga la moto chini Poland. Papa Francisko asikitishwa sana na janga la moto chini Poland. 

Papa Francisko Asikitishwa na Janga la Moto Kijijini Nowa Poland

Papa ameungana na wananchi wa Poland, hasa wale waliokumbwa na janga la moto kwenye Kijiji cha Nowa Biała, Kusini mwa Poland, Jumamosi tarehe 19 Juni 2021. Watu watatu walijeruhiwa na kupelekwa hospitalini kwa matibabu. Nyumba 21 ziliteketea kwa moto na majengo mengine 23 kuharibiwa kwa moto. Licha ya hasara kubwa kiasi hiki lakini hakuna mtu aliyefariki dunia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.  – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika salam na matashi mema kwa waamini, wageni na mahujaji waliohudhuria Katekesi yake kuhusu Waraka wa Mtume Paulo kwa Wagalatia, Jumatano, tarehe 23 Juni 2021, ameungana na watu wa Mungu nchini Poland, hasa wale waliokumbwa na janga la moto kwenye Kijiji cha Nowa Biała, Kusini mwa Poland, Jumamosi tarehe 19 Juni 2021. Watu watatu walijeruhiwa na kupelekwa hospitalini kwa matibabu. Nyumba 21 ziliteketea kwa moto na majengo mengine 23 kuharibiwa kwa moto. Licha ya hasara kubwa kiasi hiki lakini hakuna mtu aliyefariki dunia. Baba Mtakatifu amechukua fursa hii kwa ajili ya kuwakumbuka na kuwaombea wale wote walioguswa na kutikiswa na janga hili, ili Mwenyezi Mungu apende kuwafariji na hatimaye, waonje upendo, ushirikiano na mshikamano wa kidugu, wale wote waliopoteza mali zao katika moto huo.

Baba Mtakatifu amewatakia mwanzo mwema wa mapumziko ya Kipindi cha Kiangazi kwa Mwaka 2021. Yawe ni mapumziko yanayopata chanzo na hitimisho lake katika Fumbo la Utatu Mtakatifu. Wakati huo huo. Bwana Mateusz Morawiecki, Waziri mkuu wa Poland Jumapili tarehe 20 Juni 2021 alitembelea Kijiji cha Nowa Biała ili kujionea uharibifu mkubwa uliosababishwa na moto huo. Amesema, Serikali itahakikisha kwamba, kwa kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama waathirika wanapata mahitaji yao msingi. Serikali itasaidia ujenzi wa makazi pamoja na ukarabati wa nyumba za mifugo sanjari na kuwajengea wakulima uwezo wa kununua vifaa na pembejeo tayari kuendeleza shughuli za kilimo na ufugaji wa kisasa. Jambo la msingi kwa wakati huu ni kujenga na kuimarisha: umoja, upendo na mshikamano wa kidugu na wale wote waliokumbwa na maafa haya.

Janga la Moto Poland

 

 

23 June 2021, 14:55