Tafuta

Papa Francisko tarehe 18 Juni 2021 amekutana na kuzungumza na Rais wa Georgia pamoja na msafara wake. Papa Francisko tarehe 18 Juni 2021 amekutana na kuzungumza na Rais wa Georgia pamoja na msafara wake. 

Papa Francisko Akutana na Kuzungumza na Rais wa Georgia!

Katika mazungumzo kati ya Baba Mtakatifu na Rais wa Georgia, wameonesha kuridhishwa kwao na uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili na kwa namna ya pekee, ushirikiano unaojionesha katika utamaduni, sayansi na elimu. Kanisa Katoliki nchini Georgia limekuwa na mchango wa pekee kabisa katika ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini Georgia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.  – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 18 Juni 2021 amekutana na kuzungumza na Rais Salomé Zourabichvili wa Georgia, ambaye baadaye amekutana pia na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa mjini Vatican. Katika mazungumzo kati ya Baba Mtakatifu na Rais wa Georgia, wameonesha kuridhishwa kwao na uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili na kwa namna ya pekee, ushirikiano unaojionesha katika utamaduni, sayansi na elimu.

Kanisa Katoliki nchini Georgia limekuwa na mchango wa pekee kabisa katika ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini Georgia. Baadaye, viongozi hawa wawili, wamejielekeza zaidi katika masuala ya Kikanda na Kimataifa, kwa kukazia zaidi umuhimu wa wa kukuza na kudumisha haki, amani na utulivu wa kijamii.

Georgia
19 June 2021, 08:27