Tafuta

2021.06.26 Papa amekutana na wajume wa Caritas Italia 2021.06.26 Papa amekutana na wajume wa Caritas Italia 

Papa akutana na Caritas Italia:inahitajika kuishi udugu wa kweli!

Papa Francisko amekutana na kuzungumza na wajumbe wa chombo cha kichungaji cha Caritas Italia na kuwashauri watembee katika njia za walio wa mwisho,ya iInjili na ya ubunifu.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Jumamosi tarehe 26 Juni 2021, Papa Francisko amekutana na wajumbe wa Caritas Italia wakiwa katika fursa ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake. Akianza hotuba yake ameshukuru Kardinali Guartiero Bassetti rais wa Baraza la Maaskofu Italia na Mwenyekiti wa Caristas Italia Monsinyo Radelli, kwa maneno yake ambayo ametoa kwenye hotuba yake ya utangulizi kwa niaba ya wote.  Baba Mtakatifu amesema wamekuja kutoka Italia nzima kwa kuwakilisha Caritas 218 za kijimbo na Caritas Italia, na kuonesha furaha yake ya kushirikishana nao Jubilei yao ya miaka 50 ya maisha! Wao ni sehemu hai ya Kanisa, wao ni Caritas yetu, amesema Papa na kama alivyokuwa anapenda kusema Mtakatifu Paulo VI, Papa ambaye kwa matashi yake alianzisha chombo hiki. Yeye aliwatia moyo Baraza la Maaskofu Italia, kuchukua hatua hii ya chombo cha kichungaji ili kuhamasisha ushuhuda wa upendo katika Roho ya Mtaguso wa Vatican II kwasababu jumuiya ya kikristo iweze kuwa ya upendo.

Papa Francisko amethibitisha kazi yao katika mabadilijo ya nyakati, changamoto na matatizo ni mengi na daima yanazidi kuwakumba maskini na taasisi kwa ujuma katika nchi yote. Lakini kama alivyokuwa anasema daima Mtakatifu Paulo VI, Papa kuwa “Caritas zetu zinajitahidi zaidi ya nguvu zetu. (Sala ya Malaika wa Bwana , 18 Januari 1976). Tukio la maadhimisho hayo ni hatua moja ya kushukuru Bwana kwa safari iliyofanyika na kwa kupyaisha msaada wake, shauku na jitihada. Kwa kufafanua hayo, Papa ameelekeza njia tatu za mchakato wa kufauta. Kwanza ni njia ya kuelekea kwa walio wa mwisho. Ni wao ambao ni wa kuanzia yaani wadhaifi na wasio na mliniz. Upendo ni huruma ambavyo inakwenda kutafauta walio wadhaifu zaidi, unaosukumwa kwenda hadi kwenye mipaka iliyo migumu zaidi ili kuwaoka watu kutoka katika utumwa, ambao unawakandamizi na kuwafanya wawe mstari wa mbele katika maisha yao. 

Ni vizuri kupanua njia hizi za upendo, daima kwa kukazia mtazamo juu ya walio wa mwisho wa wakati wetu. Na pamoja nao, mashi yetu yanapaswa kutazama hali halisi yaani historia si kutazama kutoka matarajio ya kishinda, ambayo yanafanya kuonesha uzuri na ukamilifu lakini ni kuanzia na ile ya maskini kwa sababu ndiyo matarajio ya Yesu. Ni maskini ambao wanaweka kidole katika jeraha la mapingamizi yetu na wasi wasi wa dhamiri kwa namna njema wakitualika kubadilika. “Kupanua mtazamo ndio, lakini kuanza na mtazamo wa maskini ambaye yuko mbele yangu. Hapo unajifunza. Ikiwa sisi hatuna uwezo wa kutazama maskini, mtazamo wa machi ya  kuwagusa kwa mkono na kuwakumbatia hatujafanya kitu”, Papa amesema.

Njia ya pili ambayo Baba Mtakatifu Francisko ameelekeza ni ile ya Injili. Hii akiwa na maana ya kuongozwa na Injili. Ni mtindo wa upendo mnyenyekevu, wa dhati lakini ambao siyo wa kujuonesha, ambao unapendekeza na si kulazimisha amesisitiza. Ni mtindo wa upendo wa bure, ambao ambao hautafuti shukrani. Ni mtindo wa uwezekano na huduma kwa kumuiga Yesu aliyejifanya mtumishi wetu. Ni mtindo ambao Mtakatifu Paulo anaueleza anaposema kuwa “upendo unaamini yote, unatumanini yote na kuvumilia yote (1 Cor 13,7). Papa Francisko aidha amesema anashangazwa na neno yote. Upendo nijumuishi haungakii mantiki ya zana tu na wala ile ya kiroho. Wokovu wa Yesu unakumbatia ubinadamu wote. Tunahitaji upendo ambao unajikita katika maendeleo fungamani ya mtu. Upendo wa kiroho, wa zana na wa kiakilia. Ni mtindo fungamani ambao Papa amesema kuwa wameufanyia uzoefu katika baa kubwa kwa njia ya kusaidia na pia kupitia mapacha, uzoefu mzuri wa muungano wa pande zote katika upendo kati ya Makanisa nchini Italia, Ulaya na ulimwengu.

Njia ya tatu ambayo Papa Francisko ameelekeza ni njia ya ubunifu. Utajiri wa uzoefu wa miaka hii hamsini siyo mzigo wa mambo ya kurudia:nii msingi ambao unaweza kujengwa ili kuelekea kwa namna halisi ambazo Mtakatifu Yohane Paulo II aliita ubunufu wa upendo (Novo millenio ineunte,50). Papa Francisko amewaomba wasikate tamaa mbele ya umaskini unazidi kukuana na  umaskini mpya. Waendelee kukuza udugu kuwa ishara ya matumaini. Dhidi ya virusi vya kutokuwa na matumaini, wawe na chanjo ya kushiriki furaha ya kuwa familia kubwa. Katika mazingira haya ya kindugu Roho Mtakatifu, ambaye ni muumbaji na mbunifu, atashauri maoni mapya, yanayofaa kwa nyakati tunazoishi” amesisitiza Papa. Hatimaye Papa ametaka kuwashukuru wote huku akitania kwamba baada ya mahubiri ya kwaresima na hivyo kwa wahudumu, makuhani na watu wa kujitolea.

Wakati uliowekwa kwa vijana haujapotea kamwe, kujikita kuwa pamoja nao na urafiki, shauku na uvumilivu, uhusiano ambao huenda zaidi ya tamaduni za kutokujali na kuonekana, lakini haitoshi kuishi “like”: kwa maana kuna haja ya udugu na furaha ya kweli Papa amesisitiza. Caritas inaweza kuwa uwanja wa mafunzo kwa maisha kuwafanya vijana wengi kugundua maana ya zawadi hiyo, kuwafanya wafurahie ladha nzuri ya kujipatia katika kujitolea wakati wao kwa wengine. Kwa kufanya hivyo, Caritas yenyewe itabaki kijana na ubunifu, itadumisha mtazamo wake rahisi na  wa moja kwa moja, ambao hugeuka bila woga kuelekeza Juu na kuelekeza kwa mwingine  kama  wafanyavyo watoto

26 June 2021, 15:22