Tafuta

2021.06.26 Kitabu kipya cha " AMANI DUNIANI. Udugu unawezkana cha Papa Francisko (LEV) 2021.06.26 Kitabu kipya cha " AMANI DUNIANI. Udugu unawezkana cha Papa Francisko (LEV) 

Ndoto ya Papa ya kuona ulimwengu usio kuwa na vita

Kitabu kipya cha “Amani Duniani.Udugu unawezekana cha Papa Francisko kimechapishwa Julai 27.Ni safu ya kiekumene ya Maktaba ya Uchapishaji ya Vatican:’Kubadilishana zawadi’,ambayo inakusudia kuonesha uhusiano kati ya Wakristo wa imani tofauti.Kitabu ni mkusanyo wa tafakari na hotuba za Papa kuhusu amani na udugu.Utanguli wake ni wa Patriaki Tawadros II.Tarehe 28 Juni kitakuwa katika duka la Vitabu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Makosa ya miaka ya 1900, Vita mbili za kidunia, ubaguzi wa kiyahudi, mauaji ya kimbari, yale mawili ya karne ya XXI, ugaidi, ajali, propaganda za chuki, utafikiri havipitI kamwe kutokana na kuona kwamba mpaka leo hii amani bado imekanyagwa na kuendelea kutazamiwa. Wakati wanaendelea kutathimini vita vya hatari, kuna ubaya ambao wahusika wa kisiasa watajibu mbele ya Mungu na kwa watu. Ni malalamiko ya kina ambayo Papa anaelezea kwenye kitabu kipya chenye jina "AMANI DUNIANI" ikiwa ni katika (kukumbusha historia ya Waraka wa Yohane XXIII), na chenye kichwa kidogo “Udugu unawezekana”.

Safu ya kiekumene ya Maktaba ya Uchapishaji ya Vatican (Lev)

Ni kitabu kipya katika safu ya kiekumene ya Maktaba ya Uchapishaji ya Vatican “Kubadilishana zawadi”, ambacho kinakusudia kuonesha uhusiano kati ya Wakristo wa imani mbalimbali. Vitabu hivyo kwa hakika vinakuja na mchango wa mwakilishi mmoja wa Makanisa na Jumuiya zilizotengwa ambazo kama wakatoliki tuko njiani kuelekea mchakato wa kuanzishwa upya kwa umoja. Wakati huu ni Papa Tawadros II, Patriaki wa Kanisa la Kiorthodox la Kikoptiki huko Alexandria nchini Misri, ambaye amesaini katika utangulizi wa kitabu hicho, ambacho leo hii tarehe 27 Juni 2021 kimetolewa vifungu vya dondoo zake katika gazeti “La Repubblica”. Kuanzia kesho tarehe 28 Juni 2021, kitakuwa katika maduka ya vitabu.

Hatari ya kusahau fundisho la historia

Katika maandishi ya kitabu Papa Francisko anatoa tafakari kuanzia na hali halisi ya sasa, ile ya mamilioni ya binadamu ambao wanatamani amani lakini bado wanataishiwa na vita, wanalazimika kuacha nyumba zao na pigo la vurugu. Hamu hii, halali sana, mara nyingi hukanyagwa au kupuuzwa, anasema Papa Francisko, ambaye anasisitiza ni  jinsi gani na kupotea kwa kizazi kilichoishi kupitia Vita vya Pili vya Dunia na kwamba sisi tunasahau mafundisho hayo ya historia kwa haraka. "Kusahau maumivu ya vita anaandika Papa, hutufanya tuwe salama kwa mantiki ya chuki na inawezesha maendeleo ya vita. Ubaguzi unazuia hamu ya kweli ya amani na husababisha kurudia makosa ya zamani".

Leo vita inaangaliwa kwa upya

Papa Fransisko anakubali kuwa leo hii vita vinaangaliwa kwa upya katika hatari: “vita huchaguliwa kwa urahisi kwa kufanya kila aina ya visingizio vya kibinadamu, vya kujihami au vya kuzuia, hata ikitumia udanganyifu wa habari”. Kwa maana hiyo inaibua maswali kadhaa: “Je! Tunajua mateso ya wengi kwa sababu ya vita? Je! Tunafahamu hatari kwa wanadamu? au “tumevurugwa na kugeukia masilahi yetu?”, tumehakikishiwa kwa sababu vita haituathiri kwa karibu? Haya ni maswali ambayo yanapaswa kuwahangaisha viongozi wa kisiasa ambao watajibu mbele za Mungu na watu kwa sababu ya vita vya muda mrefu”.

Wakimbizi, mabalozi wenye uchungu wa mahitaji ya amani

Papa Francisko amerudi kwenye dhana ya vita vya tatu vilivyo gawanyika vipande vipande, na uhalifu, mauaji, uharibifu “ na anachangamotisha dhamiri ya kila mtu kwamba “Hatuwezi kuishi kwa amani na vita vinavyoendelea kana kwamba ni mbaya. Ingekuwa ni kuziba dhamiri! Kwa bahati mbaya hii hufanyika, hasa katika nchi ambazo haziathiriwi na mizozo, lakini ni kutokana tu na matokeo kama vile ya kuwasili kwa wakimbizi". Papa anasema, wao ni “mashuhuda wa vita, 'mabalozi' wa chungu wa ombi lisilosikika la amani” ambao “hutufanya tujisikie wenyewe kwa jinsi vita kwa hakika sivyo ya kibinadamu. Katika wito wake anasema, “basi tusikilize funzo lao la maisha ya uchungu! Kukaribisha wakimbizi pia ni njia ya kupunguza mateso ya vita na kufanya kazi kwa amani”.

Hakuna kutojali, hakuna kufanya biashara ya silaha

Kwa maana hiyo mwaliko wa Papa sio kutelekezwa na kutokujali badala yake na kujaribu kuchukua hatua kwa ajili ya amani bila kuchoka. Hata ikiwa mtu hawezi kuchukua hatua moja kwa moja kwenye mizozo, maoni ya macho ya umma yanaweza kufanya mengi, Papa amewakikishia kwamba “wanaweza kujitoa nchi yao wenyewe; kutoa shinikizo kwa jumuiya ya kimataifa”. Badala yake, kutojali ni mshiriki wa vita. Baba Mtakatifu Francisko anawashutumu vikundi vya mafia na uhalifu ambao wanaendeleza vita vya kweli leo hii na kuharibu amani kwa ajili ya masilahi yao na anaomba wasijibu vurugu kwa vurugu zaidi, akisisitizia ombi la  kusitisha biashara ya silaha, ambayo haiwezi kuhesabiwa haki pia katika nafasi za kazi. Papa Francisko anasema anafarijika na ukweli kwamba katika tamaduni na dini zote mbegu ya amani imepandwa iliyoshuhudiwa na mkutano ulioitishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II huko Assisi mnamo 1986: “Ulimwengu umebadilika sana tangu 1986. Lakini sisi kama, jana na zaidi ya jana, ya ushirikiano na maombi ya dini,pia kupinga tunapaswa kupinga vurugu kwa jina la Mungu”.

Ndoto ya ulimwengu bila vita

Wito wa mwisho wa Papa sio kujiachia katika vita kama rafiki wa kila siku wa wanadamu na watoto wengi ambao wanakua katika kivuli cha mizozo. Vita  anasema inaweza kukomeshwa kama ilivyotokea na utumwa: “Hatupaswi kuacha kamwe ile ndoto ya ulimwengu bila vita!. Watu wote wa dunia na wafurahie furaha ya amani!" 

27 June 2021, 10:59