Tafuta

Vatican News
2020.06.11  Papa Francisko akiwa na baadhi ya vijana wa Afrika wakimbizi na wahamiaji. 2020.06.11 Papa Francisko akiwa na baadhi ya vijana wa Afrika wakimbizi na wahamiaji. 

Ujumbe wa Papa,Siku ya 107 ya Wahamiaji na Wakimbizi 2021:Upamoja&utofauti ni utajiri

Katika Ujumbe wa Papa Siku ya 107 ya Wahamiaji na Wakimbizi Ulimwenguni 2021,kilele chake ni 26 Septemba ijayo,anakazia Kanisa litoke nje na kukutana na mgeni,liwe ardhi yenye rutuba kukuza umoja na mazungumzo ya kidini. Ni upamoja ulio mpana zaidi na shirikishi ili familia ya binadamu uweze kujenga mstakabaili wa haki na amani kwa kuhakikisha hakuna anayebaki nyuma.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika Ujumbe wake wa Siku ya 107 ya Wakimbizi na Wahamiaji ulimwenguni 2021, na ambayo itaadhimishwa tarehe 26 Septemba ijayo anaangazia umuhimu wa ujumuishaji na udugu, akisisitiza katika kaumbiu mbiu kuwa “Kuelekeza upamoja ulio mpana zaidi” yaani shirikishi utasaidia kufanya upya familia ya wanadamu, kujenga mustakabali wa haki na amani na kuhakikisha kuwa hakuna anayeachwa nyuma. Papa Francisko anasema kuwa  “katika Waraka wake wa Fratelli Tutti yaani Wote ni ndugu ameeleza wasi wasi na shauku ambayo bado inachukua nafasi muhimu katika moyo wake: Na hiyo ni kwamba “Mara tu shida ya afya ikiiisha, athari mbaya zaidi inaweza kuanguka hata zaidi katika homa ya utumiaji hovyo na aina mpya ubinafsi wa kujilinda. Shauku ya kutaka Mbingu ambayo mwishowe hakuna “wengine”, bali sisi tu (n.35). Kwa maana hiyo Papa Francisko amethibitisha kuwa katika ujumbe wa siku hii amejikita kwenye kauli mbiu isemaye “kuelelekeza  upamoja ulio mpana zaidi”, kwa kutaka kuelekeza namna iliyo wazi ya upeo wa safari yetu ya pamoja katika ulimwengu huu.

Historia ya sisi

Papa Francisko akifafanua amebainisha kuwa upeo huo upo katika mpango wa uumbaji wa Mungu, kwani Mungu aliuumba mtu kwa mfano wake; kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanaume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabariki, na akawaambia, Zaeni, mkaongezeke” (Mw1,27-28). Mungu alituumba wanaume na mwanamke, kuwa tofauti na kukamilishana ili kuunda pamoja ile hatima na kugeuka kuwa upamoja ambao ni mpana zaidi kwa kuongezeka kizazi. Mungu alituumba kwa mfano wake, na mfano wa Kuwa wamoja  na Utatu, umoja katika utofauti. Na kwakutotii kwa binadamu, alikwenda mbali na Mungu.Na hawa kwa sababu ya huruma yake alipenda kuwapatia mchakato wa safari ya upatanisho, si kwa binafsi bali ni pamoja na watu, ambao tuna hatima inayojumuisha familia nzima ya kibinadamu, ya watu wote: “Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. (Uf 21,3).

Historia ya wokovu kwa maana hiyo inatazama umoja wetu, mwanzoni na upamoja wetu mwishoni na katikati kuna fumbo la Kristo, aliyekufa na kufufuka ili  Wote wawe na umoja (Yh 17, 21). Wakati uliopo, lakini unaonesha kwamba ile ya sisi ambayo Mungu aliipenda, imevunjika na kumegeka vipande, vipande, imejeruhiwa na kuharibiwa. Na hiyo imejionesha hasa katika wakati wa mgogoro mkubwa kama ule wa sasa wa janga. Utaifa uliofungwa na fujo (taz Fratelli tutti 11) na mzizi wa ubinafsi( 105), vinaangusha na kugawanya sisi wote ulimwenguni na ndani ya Kanisa. Na gharama ya juu zaidi inalipwa na wale ambao wanaweza kuwa wengine kwa urahisi, wageni, wahamiaji, waliotengwa, ambao wanaishi katika pembezoni mwa maisha. Papa Francisko anaandika kuwa kiukweli sisi sote tupo ndani ya mtumbwi ulio sawa, na sisi tunaalikwa kujikabidhi ili pasiwepo tena kuta ambazo zinatutengaisha, wasiwepo zaidi wengine, bali sisi wamoja, wakuu kama ubinadamu wote. Kwa maana hiyo Papa anatumia fursa ya Siku hii kuzindua miito miwili ya kutembea pamoja kuelekea ile kuwa na upamoja daima ulio mpana zaidi  akiwalekeza awali ya yote waamini wakatoliki na baadaye watu wote wanaume na wanawake ulimwenguni.

Kanisa daima katoliki zaidi

Papa Francisko akiwaelekea wajumbe wa Kanisa Katoliki kwa wito huo anasema unajifafanua katika jitihada ya kuwa waaminifu daima wakatoliki katika kutimiza kile ambacho Mtakatifu Paulo alikuwa anawashauri Jumuiya ya Waefeso: “Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu; Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja”. (Ef 4,4-5). Kwa hakika ukatoliki wa Kanisa, ulimwengu wake ni hali halisi ambayo inaomba kuupokea na kuuishi kila kipindi, kwa mujibu wa mapenzi na neema ya Bwana ambaye alituahidi kuwa  nasi daima hadi mwisho wa dunia” (Mt 28,20). Roho yake inatufanya kuwa na uwezo wa kukumbatia wote ili kufanya muungano katika utofauti, kuwa maelewano katika tofauti  na kamwe bila kulazimisha ufananisho ambao unaondao utu. Katika Mkutano na wageni tofauti, wahamiaji na wakimbizi na katika mazungumzo ya kiutamaduni ambayo yamewezekana, kumekuwapo na fursa za kukua kama Kanisa, kuendelea kujitajirisha. Na kila mahali anapokuwapo mbatizwa na haki kamili, ni mjumbe wa jumuiya ya kikanisa mahalia, mjumbe wa Kanisa moja, mkazi wa nyumba moja na mjumbe mmoja katika familia.

Waamini wakatoliki wanaitwa kujibidisha, kila mmoja kuanzia na jumuiya anaoyoishi, ili Kanisa liweze kuwa daima jumuishi, kwa kutoa mwendelezo wa utume ambao aliukabidhi Yesu Kristo kwa Mitume wake. “Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia. Ponesheni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure” (Mt 10,7-8). Kanisa leo hii linaitwa kutoka nje kwenda  kwenye njia za pembezoni mwa maisha ili kutibu aliyejeruhiwa na kutafuta aliyepotea, bila kuhukumu au kuwa na hofu, bila propaganda, lakini utayari wa kupanua hema lake kwa ajili ya kupokea wote. Miongoni mwa wakazi wa  pembezoni, tutakutana na wahamiaji na wakimbizi wengi, waliohamishwa na wathiriwa wa biashara haramu ya binadamu, ambao Bwana anataka waoneshwe upendo wake na watangaziwe wokovu. Wingi wa wahamiaji wa sasa unaunda miundo mipya ya kimisionari, fursa na muafaka wa kutangaza Yesu Kristo na Injili yake bila kuondoka katika mazingira binafsi, kushuhudia kwa dhati imani ya kikristo katika upendo na kwa kina kuheshimu imani za dini ya wengine. Mkutano na wahamiaji na wakimbizi wa madhehebu mengine ya kidini,  kwa dhati ni utajiri anasisitiza Papa. ( Hotuna kwa Wakurugenzi wa kitaifa wa kichungaji kwa ajili ya Whamiaji na wakimbizi, 22 Septemba 2017).

Ulimwengu ulio jumuishi daima

Akiwaelekeza wengine, wanaume na wanawake wa ulimwengu, Papa Francisko amewapa wito wake wa kutembea pamoja kuelekea upamoja daima ulio mpana zaidi, ili kuunda familia ya kibinadamu, kwa ajili ya kujenga pamoja mstakabali wa haki na amani, kwa kuhakikisha kuwa hakuna hata mmoja anayebaguliwa na kubaki nyuma. Wakati ujao wa jamii zetu ni wakati ujao wa rangi, uliotajirishwa na tofauti na uhusiano wa tamaduni nyingi. Kwa maana hiyo lazima kujifunza leo hii kuishi pamoja kwa maelewano na amani. Papa Francisko ameeleza picha ambayo kwa namna ya pekee anaipenda sana ile ya siku ya  ubatizo wa Kanisa, siku ya Pentekoste, ya watu wa Yerusalemu waliokuwa wanasikiliza tangazo la wokovu na kwa ghafla wakashukiwa na Roho Mtakatifu: “Warparthi na Wamedi na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, Uyahudi na Kapadokia, Ponto na Asia, Frigia na Pamfilia, Misri na pande za Libia karibu na Kirene, na wageni watokao Rumi, Wayahudi na waongofu, Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu” ( Mdo 2,9-11).

Ni wazo la Yerusalemu mpya (Is 60: Mdo ,21 3), mahali ambapo watu wote wanaungana kwa pamoja, katika amani na maelewano, wakisherehekea wema wa Mungu na maajabu ya uumbaji. Ili kuweza kufikia hilo wazo lakini ni lazima kujitihaidi wote ili kuvunja kuta ambazo zinatutenganisha na kujenga madaraja ambayo yanasaidia utumaduni wa kukutana, kwa kuwa na utambuzi wa unganisho la karibu ambalo lipo kati yetu. Katika mtazamo huo, uhamiaji mambo leo unatupatia fursa za kushinda hofu zetu ili kuacha kutajirishwa na tofauti za zawadi za kila mmoja. Ikiwa tunataka hivyo basi, tunaweza kubadilisha mipaka kuwa maeneo muafaka ya makutano, mahali ambamo panaweza kuchanua miujiza ya upamoja daima ulio mpana zaidi na shirikishi.

Kwa wanaume na wanawake wa ulimwengu huu, Papa Francisko anawaomba watumie vizuri zawadi ambazo Bwana wamewakirimia wote ili kuhifadhi na kufanya kazi yake ya umbaji iwe nzuri zaidi. “Mtu mmoja, tajiri, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi. Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja. (Lk 19, 12-13). Bwana atatuuliza kazi yetu!  Na ili nyumba yetu ya pamoja iweze kuwa na usalama  na  haki ya utunzaji, lazima kurudi  kuwa na umoja ambao ni mpana daima, na kuwa wawajibikaji zaidi, katika nguvu ya kuamini kwamba kila wema uliofanyika ulimwenguni, umefanywa na kizazi kilichopo na kile kitakachokuja. Hii ndiyo kazi binafsi na ya pamoja ambayo lazima zingatie na jukumu la kutunza kaka na dada wote ambao tutaendelea kuteseka wakati tunatafuta kutimiza maendeleo endelevu zaidi, yenye msimamo na jumuishi. Ni jitihada ambayo haitofautishi kati ya mzaliwa, na mgeni, kati ya raia na wa wageni, kwa sababu hii ndiyo tunu ya pamoja kutokana na  utunzaji na kama ilivyo kawaida ambayo hakuna yoyote anayebaguliwa.

Ndoto ina mwanzo

Nabii Yoeli alitangaza wakati ujao wa masiha kama wakati wa ndoto na maono yaliyotokana na Roho “Nitamwaga roho yangu juu ya kila mtu na wana wako na binti zako watakuwa manabii; wazee wenu watakuwa na ndoto, vijana wenu watapata maono (Yoeli 3,1). Tunaalikwa kuota ndoto pamoja. Hatupaswi kuwa na hofu ya kuota na kufanya pamoja kama wanadamu na kama wasindikizaji wa safari moja, kama watoto wa ardhi moja ambayo ni nyumba yetu ya pamoja, ya kaka na dada wote (Fratelli tutti 8).

Sala

Baba Mtakatifu na uliyependwa, mwanao Yesu Kristo alitufundisa kuwa Mbinguni kuna furaha kubwa ikiwa mmoja aliyepotea anapatikana, ikiwa mtu aliyebaguliwa na kukataliwa au kutupwa anakaribishwa na sisi ambao tunageuka kuwa upamoja ulio mpana zaidi.   Tunakuomba uwajalie wafuasi wote wa Yesu na, watu wenye mapenzi mema neema ya kutimiza mapendo yako ulimwenguni. Ubariki kila ishara ya makaribisho na huduma ambayo kila mmoja anaweza kupata ndani ya jumuiya zetu na katika Kanisa, ili ardhi yetu iweze kuwa namna ambavyo uliiumba, nyumba yetu ya pamoja ya kaka na dada, amina.

UJUMBE WA PAPA WA SIKU YA WAHAMIAJI NA WAKIMBIZI
06 May 2021, 16:09